sir mweli
JF-Expert Member
- Feb 8, 2017
- 495
- 572
Habari wadau, naomba wenye fact mje tujadili . Ukiitishwa uchaguzi leo wa usawa na haki kati ya CCM na CDM nani atashinda?
Naomba tuchangie kwa fact, point to point, Jazba, matusi visiwepo kwan hapo itasomeka kama moja ya dalili za kushindwa...Naanza Mimi...
CCM itashindwa.
Naomba tuchangie kwa fact, point to point, Jazba, matusi visiwepo kwan hapo itasomeka kama moja ya dalili za kushindwa...Naanza Mimi...
CCM itashindwa.
- Paka sasa haijatimiza ahadi nyingi ilizoahidi wananchi kama viwanda, mil 50 kila kijiji, pembejeo za kilimo na ujenzi kushuka bei na nyingine nyingi.
- Maslahi ya wafanyakazi yameendelea kuwa duni licha ya hali ya maisha kuwa juu.
- Mikopo kwa wanafunzi iliahidiwa ila wachache ndo walofaidika.
- Wazee ambao ndo tegemeo lao ndo kila kukicha wanalia hali mbaya.
- Mahakama ya mafisadi iliyoahidiwa haipo, mafisadi wenyewe hatuwaoni.
- Serikali imeendelea kulitia taifa umaskini kwa kuvunja mikataba inayoligharimu taifa na kusababisha baadhi ya Mali zilizopo nje kukamatwa.
- Kuzuia bunge live hivyo kuwakosesha fursa wananchi kujua wabunge wao wanajadili nini..
- Kutumia fedha za umma kwa ufedhuli kama kuhonga madiwan ili wajiunge nao.
- Kusitisha ajira kwa wenye Vyeti fake, wakati wengine wakiachwa na ajira zao.
- Kusitisha ajira mpya kwa vijana
- Kuzuia mchakato wa katiba
- Zipo nyingi sana .. .ngoja niwapishe wengine....ila chondechonde matusi hapana tafadhali.