Ubuntu trusty tahr
JF-Expert Member
- Sep 5, 2016
- 322
- 219
dear pesa mimi ni mpambe wako leo ninakutumia ujumbe naona upo bize sana kila mtu anakusaka hata waliokupata bado wanakusaka.Ona umefanya maisha yangu yayumbe ni jana tuu nilikuwa na mpenzi wangu leo kanitosa kisa nimekukosa aliekupata amenizidi umeniletea kizaazaa sina furaha nimezubaa naumia nakosa aamani!!
Dear pesa nawaza ni nani alikuumba kila nikikupata hutulii unatoroka nimetumia mbinu nyingi kukudhibiti lkn sijafanikiwa ama kweli unasumbua sana hata vigogo unawatoa jasho.
Dear pesa jaribu kuwa mtulivu ili tuwe marafiki jisikie vibaya watu wanapoteza maisha hospitalin kwa ajili yako wewe nani mpaka nishindwe kulala kwa ajili yako kila kona unamajina mengi hata ya ajabu ajabu kama mtonyo,jiwe chapaa na mavumba .
Dear pesa ona wanavyokusujudu huku wengine wakijiita mabingwa wa kukutumia wanakesha kwenye kumbi za starehe kwa ajili yako wengine wanapendeza kwaajili yako ona mi nafubaa pia ni kwa ajili yako.
Dear pesa jana nimekusubiri njia panda lakini hujatokea jirani yangu anakusubiri mwisho wa mwezi labda utatokea nasikitika huku mtaani wamenipa majina mengi yakiwemo kapuku na fukara eti kisa nimekukosa .
Dear pesa kwa heri naondoka naenda kujipanga naamini wewe ni kila kitu unaweza kunipa hata faraja...