Dear Crush, leo naona nijiweke huru na nikwambie ukweli huu ambao hapo kabla sikuwahi kumwambia yeyote

josephdeo

Member
Nov 23, 2015
95
196
Baada ya kutafakari kwa kina nimeona leo nitoe siri ambayo nimekaa nayo kwa mda mrefu nafsini mwangu. Siri ambayo hakuna mwingine zaidi yangu na Mwenyezi Mungu anaifahamu. Siri ambayo nimeitunza kwa nguvu, akili na juhudi zangu zote lakini kwa sasa naona sina hata kimoja kati ya hivyo ambavyo nilivitumia hapo awali kuitunza siri hii.

Hivyo hakuna namna naweza tena kuendelea kuitunza siri hii na leo nakwambia wewe siri hii. Sio kwamba nilikuficha siri hii kwa ubaya hapana!

Hakukuwa kwa ubaya ila nilishindwa kukwambia tu na ukiniuliza ni kwanini nilishindwa kukwambia, nitakujibu kuwa ni kwasababu sikuwa na uwezo wa kukwambia kwani hata kukutazama tu ilinibidi kutumia mpaka nguvu za ziada kufanya hivyo. Sasa ningewezaje kukusogelea na kukwambia haya ninayoyataka kukuelezea leo! Nisingeweza kwakweli lakini sifahamu hata ni wapi nimeutoa ujasiri huu leo na kutaka kuvunja minyororo ambayo nilijifunga kwa mda na hata ukuniuliza pia ujasiri huu nimeutoa wapi? Sitakuwa na jibu sahihi zaidi ya kukwambia kuwa nafikiria huu ni wakati sahihi wa wewe kujua.

Nimekuwa kwenye kifungo ambacho sifahamu ni nani alipeleka kesi mahakamani mpaka kuhukumiwa na kuanza kukitumikia kifungo hicho. Lakini leo inaweza kuwa siku yangu ya kuwa huru kwa sababu nataka kukimaliza kifungo changu kwa kusema yale ambayo yalisababishwa nipate hukumu na kikitumikia kifungo hicho. Leo hii nahitaji kuwa huru na naitaji kurudi katika sehemu ya utilivu wa nafsi yangu baada ya kuuondoa kwa muda ambao mpaka sasa siwezi hata kuhesabu.

Leo nakwambia kuwa jasho ambalo nimekuwa likivuja mwilini mwangu ni kwasababu ya kuhakikisha nakupatia furaha. Maumivu ambayo nimekuwa nayapitia pale ambapo ninakuona na mtu mwingine hata kama ni rafiki kwako siwezi kuyaelezea. Nimekuwa nikiteseka na hali hii ambayo siwezi hata kuelezea kwa maneno au vitendo. Mara zote umekuwa ukiufanya moyo wangu kuwa dhaifu sababu ya mapenzi yaliyo jaa ndani yangu.

Sifahamu kama ulishawahi hata kujihisi chochote juu yangu lakini mwenzio ninayo mengi ambayo najihisi juu yako. Na hata moja sijawahi kulielezea kwako au hata kwa mwingine yoyote zaidi ya nafsi yangu ambayo hainisaidii chochote zaidi ya kuniongezea huzuni.

Dear Crush leo naona nijiweke huru na nikwambie ukweli huu ambao hapo kabla sikuwahi kumwambia yeyote yule. Umeufanya moyo wangu kuwa dhaifu na hata kupoteza kujiamini ninapokuwa mbele yako. Akili yangu inapoteza weledi pale unapokuwa umesimama mbele yangu. Na wala hata sijiwezi ninapokutazama na siwezi hata kurudisha neno pale ambapo unanisemesha. Napata usingizi lakini kila nikianza kukufikiria hata usingizi nao unanikimbia. Kila mara ninajisikia fahari sana pale ambapo unataja jina langu hata ikiwa kwa ubaya mwenzio hua nafarijika.

Ubaya ni kwamba yote haya huwa yananikuta pasipo hata wewe kufahamu na leo nimeamua kuwa muwazi kwako na kukwambia kuwa NAKUPENDA SANA na inawezekana kabisa kushindwa kuishi bila wewe.

Sifahamu ni nini maana ya mapenzi lakini moyo wangu unahisia nzito sana za mapenzi juu yako. Kama jukumu la mwanaume alilokabidhiwa na Mungu katika bustani ya Eden kuwa anapaswa kumpenda mwanamke. Basi nami najihisi kukupenda sana, nakupenda kimapenzi.

Nafahamu fika kuwa unayo machaguo na maamuzi yako juu ya nani unapaswa kumpenda. Lakini kabla ya kufikiria hayo naomba uchukue hata dakika moja kufikiria kuhusu mimi. Binadamu pekee niliyejaza mapenzi katika moyo wangu na yote yakiwa ni juu yako. Nakupenda na kwa kuwa siwezi kuonesha hisia zangu kutoka ndani ya moyo wangu nilikuwa naomba kibali kutoka kwako ili nikuoneshe ni kwa kiwango gani moyo wangu umejazwa mapendo juu yako.

NAKUPENDA ndio siri ambayo nilikuwa nayo wakati wote na ndio nilikuwa natumikia kifungo chake na wewe ndie uliyekuwa hakimu ambaye uliruhusu mimi kwenda jela. Naomba leo unifanye niwe huru kama ulivyonifanya kuwa mfungwa kwa kufahamu kuwa NAKUPENDA. Asante!
 
Kama ww sio harmonize basi itakuwa yule mlinzi wake wa karibu umeamua kumfungukia kajala mpaka huku.
 

Similar Discussions

6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom