Deadline ya Sensa haijaisha, Why Watu wanashitakiwa kwa Kutokuhesabiwa??

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,459
29,153
Wadau,

Wote tunafahamu kua wapo watu ambao wamefikishwa mahakamani kwa kugoma kuhesabiwa.
Pia wote tunafahamu kua muda wa kuhesabiana ulikua ni wiki moja (ambayo labda inaisha leo).
sasa kama ndivyo kuna uhalali gani wa kuwashitaki watu kwa kugoma kuhesabiwa wakati siku yenyewe ya mwisho bado??

Serikali haioni kwamba kwa hili inachemka kwa kupoteza muda na nguvu bure kwa kuanzisha kesi ambazo ni wazi hawatashinda? Yaani hawa watu wakisema kwa mujibu wa ratiba zao walipanga kuhesabiwa mwishoni mwa muda but within deadline utawafanyaje? Au wakaja na madai kua kwa serikali kuwaweka rumande ndio kumewakosesha wasaa wa kuhesabiwa majumbani mwao serikali itabisha?

Nafikiri huu ni muendelezo wa kukurupuka na kuchemka kwa serikali katika maamuzi mbalimbali inayoyafanya. Haiwezekani i-conclude kua watu wamegoma wakati muda wenyewe haujaisha.
Shark
 
Last edited by a moderator:
Hao wamewai sana. Mi nimeletewa barua kutoka siri kali ya mitaa wananiita. Ma dc wamesema sensa imefanikiwa kwa asilimia mia moja sasa mbona wamechanganyikiwa?
 
Nafikiri unachukuliwa umekataa kuhesabiwa pale karani wa sensa anapokuja nyumbani kwako wakati ukiwepo lakini ukakataa kumpa ushirikiano........hata kama muda wa zoezi zima haujesha!
 
Ok,
But kama umeniwekea muda wa wiki moja nzima basi why unanikamata sasa hivi?? may be i am not ready kwa sasa due to some reasons but we may scheduling it next time.
Wapo watu waliokua safarini ambao kwa kua kule walikokuwepo hawakuhesabiwa, basi wakaweka appointment na makarani ili wakirudi wahesabiwe na ikawa hivyo!!
 
huenda ikawa kuna baadh ya taarifa sina uhakika NAZO
 
Hivi JK Mbona anakurupuka hivyo, Yaaan eti anasema muda wa kuhesabiwa umeongezwa na wale ambao hawajahesabiwa wajipeleke kwa Makaran ama sivyo watashtakiwa, huu nu ujuha, yaan mie nikajipeleke kwa Karan wa kuhesabu ilhal huo karan kalipwa Fedha za kodi zangu kuja kwangu kunihesabu.

Serikali ya JK na JK wenyewe ni MAJUHAAAAAAAA
 
Ok,
But kama umeniwekea muda wa wiki moja nzima basi why unanikamata sasa hivi?? may be i am not ready kwa sasa due to some reasons but we may scheduling it next time.
Wapo watu waliokua safarini ambao kwa kua kule walikokuwepo hawakuhesabiwa, basi wakaweka appointment na makarani ili wakirudi wahesabiwe na ikawa hivyo!!
Ndio maana nimetumia neno "ushirikiano"! Sote tunajua kunaweza kuwepo dharura au udhuru......lakini sifikirii kama kwa mtu wa namna hiyo atoatoa jibu kama "sitaki" kwa karani.
 
Serikali sio wajinga....wanaokamatwa sio waliokataa kuhesabiwa bali wanaoshawishi watu kukataa kuhesabiwa. Mtu aliyekataa anaweza kuchukuliwa hatua endapo tu ataenda mbali zaidi ya huko kukataa.....sawa na raia mmoja wa morogoro ambae yeye aliamua kuchukua dodoso na kuzichana!! Wanaokataa kuhesabiwa nyumba zao huwa tu zinawekwa alama na sio kukamatwa!
 
Sensa ina utaratibu wake wa kuhesabu, most of time, inakwenda kwa locations ambazo zipo ndani ya ramani ya malengo yao kwa siku. Hizo ramani zao zinahakikisha kila eneo kapangiwa karani muhusika ili kuepusha uwezekano wa watu kuhesabiwa zaidi ya mara moja au kutohesabiwa kabisa. Sasa kama lengo la leo ni kuhesabu Ikulu, Mh JK akakataa kuhesabiwa, itahesabika amekataa kufuata utaratibu wa kisheria wa kuhesabu watu kwa mujibu wa kanuni za Tume inayosimamia sensa.
Zoezi hili lina kasoro zaidi ya 50% ambazo ni nyingi mno, hao walioshitakiwa watashinda kesi kama HAKI ITAFUATWA
 
Serikali sio wajinga....wanaokamatwa sio waliokataa kuhesabiwa bali wanaoshawishi watu kukataa kuhesabiwa. Mtu aliyekataa anaweza kuchukuliwa hatua endapo tu ataenda mbali zaidi ya huko kukataa.....sawa na raia mmoja wa morogoro ambae yeye aliamua kuchukua dodoso na kuzichana!! Wanaokataa kuhesabiwa nyumba zao huwa tu zinawekwa alama na sio kukamatwa!

Fuatilia kwa umakini taarifa za sensa utagundua kwamba watu wengi wameshtakiwa kwa kukataa kuhesabiwa.
Wangekamatwa wanaohamasisha kususia sensa sheikh Ponda angekuwa wa kwanza kukamatwa na kushtakiwa.
 
Mi nawashangaa sana watu.Mfano Bukoba waislam wameshauriwa na mashehe na viongozi wao kugoma kutoa ushirikiano wa kutokuhesabiwa na baadhi wakafanya hivyo.Sasa cha kushangaza,hata viongozi wao walihesabiwa vizuri kabisa kwa ushirikiano na makarani vizuri tu.Maskini wale ambao WALIKUWA WATIIFU KWA VIONGOZI WAO,yaani kutokubali kuhesabiwa wakapelekwa mahakamani cha kushangaza wale viongozi waliowaambia WASIHESABIWE,halafu wao WAKAHESABIWA,waliandamana kupinga kukamatwa kwa wale waliohesabiwa.Hivi kweli ndgu hapa kuna nini?Kutumia ujinga wa watu kupata umaarufu na kufanya fujo.Mashehe karibia wote waliokuwa wanahamasha ,hata akina Farid kule Zanzibar sijasikia aliyekamata maana wamehesabiwa.Tuwe makini na viongozi hawa wanatumia hekima zao kuwadanganya wasio na elimu kunyanyasika...!
 
Bosi wa sensa amesema waliokuwa wanagomesha wenzao walikubali kuhesabiwa, wafuasi wameishauzwa!
 
Back
Top Bottom