DCP Msangi atolewa Mwanza na kupelekwa Makao Makuu kuwa Kamishna wa kitengo cha makosa dhidi ya binadamu

Hakunaga mtu anayependa kupelekwa hapo makao mkuu maana huko ni kusoma magazeti tu na media hauonekani

Ova
 
Hii inamana amepanda cheo kutoka assistant commisioneř to commisioner
Huyo alikua DCP hawezi kupanda tena akipanda hapo ujue anakua Full Commissioner!

Makamishina wanatakiwa kimuundo wawe wa 4 tu...

Sasa hivi wako wa5 maana kuna yule mameno CP Mussa wa Zanzibar yupo anaranda randa kwenye viunga vya Makao Makuu baada kuondolewa kule Zanzibar huku umri wa kustaafu bado...

so Msangi hawezi kupanda sasa hivi labda mmoja afe ama ateuliwe kuongoza kanda maalum ambayo sasa hivi iko chini ya SACP
 
Ulimboka akimsikia huyo makalio na roho inamuuma..bingwa wa utesaji huyo tangu Chuga! halafu physical appearance yake na matendo vitu mbili tofauti..na ile rav 4 yake akiwaga dar anayo pigia misele!
Huyu jamaa namkumbuka sana kwa roho yake ilivyo, tangia akiwa mkuu wa upelelezi wilaya kituo cha usariver.
Ila machoni kama binadamu vile.
 
Amehamishiwa Makao Makuu na kuwa kamishna wa kitengo cha makosa dhidi ya binadamu.

----
Mkuu wa Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amefanya mabadiliko madogo kwenye jeshi hilo na kumuondoa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza (DCP) Ahmed Msangi na kumhamishia makao makuu ya jeshi hilo.

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatano Agosti 15, 2018 na Msemaji wa polisi, Barnabas Mwakalukwa imeeleza kuwa Msangi amehamishiwa makao na kuwa Mkuu wa kitengo cha makosa dhidi ya binadamu makao ya upelelezi Dar es Salaam.

Mwakalukwa amesema nafasi ya Msangi imechukuliwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jonathan Shana.

“Nafasi wa Shana imechukuliwa na Kamanda Wankyo Nyigesa aliyekuwa mkuu wa operesheni kanda maalumu ya Dar es Salaam,” amesema Mwakalukwa.

Kwa mujibu wa Mwakalukwa mabadiliko ya uhamisho huo ni ya kawaida yanatokea ndani jeshi la polisi katika kuongeza ufanisi kwenye utendaji kazi.

Chanzo: Mwananchi
Bora aondoke tupumue, hebu jiulize kutoka geita sengerema mwanza kulikuwa na trafik 42 na check point saba kweli? walikuwa wanakagua nini cha zaidi? kutoka mwanza magu hadi nyashimo kulikuwa na trafik 36 na vituo nane vya ukaguzi wa magari ni nini kilichokuwa kinatafutwa? kama sio kubambika watu makosa ya barabarani?
 
Bora aondoke tupumue, hebu jiulize kutoka geita sengerema mwanza kulikuwa na trafik 42 na check point saba kweli? walikuwa wanakagua nini cha zaidi? kutoka mwanza magu hadi nyashimo kulikuwa na trafik 36 na vituo nane vya ukaguzi wa magari ni nini kilichokuwa kinatafutwa? kama sio kubambika watu makosa ya barabarani?
Kwa hiyo unamaanisha kuondoka kwake na hayo uliyoorodhesha anaondoka nayo?
 
Wakitaka kukunyamazisha ni rahisi tu , huyu jamaa hata kwenye magazeti tena haonekani , Dah !
 
Back
Top Bottom