News Alert: DCJ: Philomena Mwilu: Kesi ya Naibu Jaji Mkuu yasimamishwa Kenya

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
_103213137_41a528f5-1bdc-42fc-84b0-c7784904e135.jpg


Mahakama Kuu Kenya imesimamisha uendeshaji wa kesi ya ufisadi dhidi ya Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu.

Mwilu amewasilisha ombi katika mahakam hiyo akiomba asijibu mashtaka ya ulaghai, utumiaji mbaya wa mamlaka na kukwepa kulipa kodi, kesi iliyowasilishwa dhidi yake hapo jana na mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma.

Kupitia wakili wake, Okongo Omogeni, Mwilu ameambia Mahakama Kuu leo asubuhi kwamba kesi hiyo iliyowasilishwa dhidi yake ina hila na ni njama dhidi yake.

Katika ombi lake mahakamani, alikuwa amewashtaki mkurugenzi wa mashtaka ya umma, Idara ya Uchunguzi wa Jinai, Mwanasheria Mkuu na Hakimu Mkuu anayeangazia kesi za ufisadi.

Mahakama ya juu sasa imeamua kusitisha kesi ya uhalifu inayomkabili Mwili kukisubiriwa kuamuliwa masuala ya kikatiba yanayotokana na ombi alilowasilisha Okotoba 9.

Jaji Chacha Mwita wa mahakama kuu ameeleza kwamba ombi hilo la Mwilu linazusha masuali makuu.

Naibu jaji mkuu huyo anakabiliwa na mashtaka kadhaa yakiwemo kutumia vibaya mamlaka yake, na kutolipa ushuru.

Inadaiwa kuwa jaji huyo alikiuka sheria ya uongozi na maadili kwa kupokea mkopo wa kibinafsi wa thamani ya takriban $120,000 kutoka kwa benki ya Imperial.

Mwilu hatahivyo amejitetea kwa kusema mkopo huo ulitokana na makubaliano ya kibiashara.

Mahakama hiyo kuu imeamua sasa kwamba kuna masuala ya kutathminiwa kikatiba kubaini iwapo makubaliano ya kibiashara baina ya mtu na taaisis ya kibiashara yanaweza kutazamwa kama mashtaka ya uhalifu.

Kwa sasa kesi hiyo ya uhalifu imesimamishwa hadi Oktoba 9.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom