Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura amedai kuwa uchunguzi uliyofanywa na Jeshi la Polisi umebaini kwamba Hamza Mohammed alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga.

Hamza aliuawa na polisi Agosti 25, mwaka huu baada ya kuwaua kwa risasi askari wanne, watatu kati yao wa polisi na mmoja wa kampuni binafsi ya ulinzi jirani na ulipo ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Alhamisi Septemba 2, 2021 jijini Mwanza na waandishi wa habari Wambura amesema uchunguzi huo ulijikita katika mambo makuu matatu ambayo ni kutaka kutambua Hamza Mohammed ni nani, nini kilimsukuma Hamza kwenda kufanya tukio lile na kutaka kutambua mshiriki mwingine katika tukio hilo.

Wambura amesema katika uchunguzi huo polisi imebaini kwamba Hamza alikuwa akiishi kisiri huku akiwa amegubikwa na viashiria vyote vya ugaidi.

"Amekuwa akijifunza mambo mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii ambayo kwa kipindi kirefu amekuwa akijifunza mambo ya kigaidi kwa kuangalia mitandao ambayo inaonyesha matendo ya Al-Shabab na makundi kama ISIS yanayoendelea na wagaidi wengi hujifunza kupitia mitandao hiyo," amesema Wambura.

Amesema kwamba kitendo alichokifanya Hamza kilikuwa ni cha ugaidi wa kujitoa mhanga.

"Tabia na matendo ya Hamza aliyapata kupitia mawasiliano aliyokuwa nayo na watu wanaoishi katika nchi zenye matendo ya kihalifu ikiwemo ugaidi hasa wa kupitia mtandao yanayojulikana kama "Radicalisation through social media)," amesema Wambura.

Kuhusu taarifa zinazodai kwamba Hamza aliwashambulia askari hao kwa sababu walimdhulumu madini yake, Wambura amekanusha na kusema katika uchunguzi huo wamebaini kwamba Hamza hakuwa na madini wala fedha katika mazingira yale.

"Hamza hakuwa na madini wala pesa na hakuwa katika nafasi yoyote ya kumiliki madini wala pesa mbali ya kwamba watu wengi wameongea kwamba alikuwa anamiliki migodi ya madini kule Chunya na maeneo ya Makongolosi uchunguzi wetu umebaini hali hiyo ya maisha ilikwisha simama muda mrefu," ameongeza Wambura.

Wambura ameongeza kuwa taarifa ya uchunguzi huo pia imebaini kwamba Hamza alikuwa kwenye kundi la magaidi wanaoamua kuifia dini.

Chanzo: Mwananchi
DCI wambura, watanzania siyo wajinga Kama unavyowachukulia.Uchunguzi wako ni very shallow. Heri ya Police jamii anaweza kujieleza vizuri katika swala hili nakuwasadikisha wananchi kuliko wewe
 
Ndiyo haya tu? Kisa kishaisha hicho, duh! Hilo hitimisho ndo kali ya yote 😂
 
Bunduki haishikwi vile kwa mtu asie ijua.
Huyo dogo alikuwa "Brainwashed" na alipata abc za matumizi ya silaha za kivita.
 
Hamza's target: Police only.

WHY?

The unsolved question that will remain unaddressed ever!

-Kaveli-
 
Hilo halina Ubishi.
Hamza alikuwa Gaidi namba 2.
ndio maana karibia wafuasi wote wa Chadema walimtangaza Hamza kama shujaa wao, inathibitisha kuwa Chadema wanaunga mkono kwa 100% vitendo vya kigaidi.
Wewe gaidi rudisha madini yake na pesa zake milion 400 ni gaidi gani hashambulii wapita njia? Gaidi huwa hachagui pa kushambulia
 
Huu ubambikaji mpaka kwa maiti isiyoweza kujitetea unashangaza Sana. Wameamua wenyewe kwa vinywa vyao kuuleta ugaidi Tanzania ambao kimsingi haukuwepo.

Makofi kwa DCI
Polisiccm na CCM wanaichafua Nchi kwa kuitangaza kuwa ina magaidi watazorotesha uchumi kwa kukosa watalii
 
Chini ya wiki moja wamekwisha chunguza maisha ya Hamza Chunya na Dar! Bado wanatafakari namna ya kuunganisha washirika wake, naona kama vile kesi ya Mbowe inaongezwa nyama.
Familia ukoo wa Hamza sasa wanataabika wamekuwa wahanga wa tukio la Hamza ni fursa kwa Polisiccm kuwabambikia kesi
 
Duh kuna watu wana bahati sana. Mwanangu junia na darasa lake la sita B hawezi kuandika taarifa ya kipopoma kama ya huyu anayeitwa dci. Hii ni taarifa ya uchunguz au mpasho?
Hakuna uchunguzi hapo bali wameibambikia Maiti tuhuma feki za ugaidi
 
Ni kama vile analeta wasiwasi flani hivi wa dini flani ili ichukiwe?
Nadhani haikuwa bora sana kutamka hili la dini,
Linaweza kuamsha wengine kwa hasira tu
Sio kauli njema kwa kweli
Polisiccm wamejidhalilisha sana
 
Na wenyewe polisi waache uonevu, unyanyasaji, rushwa, mauaji ya kiholela ya watuhumiwa, kubambikia watu kesi, kutumiwa na wanasiasa wa ccm, nk. ili na sisi raia wema tuweze kuwaamini kwa 100%!
Kuweka watu vituoni zaidi ya saa 48 pasipo kuwafikisha mahakama ni
 
Seleman 0787132277 au 0715132277 ni rafiki mkubwa wa marehemu Hamza mpigie usikie maneno yake juu ya marehemu Hamza na Polisiccm
 
Wewe gaidi rudisha madini yake na pesa zake milion 400 ni gaidi gani hashambulii wapita njia? Gaidi huwa hachagui pa kushambulia
kwa nini mwaka 1998 Magaidi walishambulia na kulipua Ubalozi wa marekani wakaacha balozi zingine ambazo zilikuwa pembeni?
pia jiulize kwa nini inadaiwa Mbowe alikusudia kuwauwa viongozi wa Serikali na kulipua vituo vya mafuta?
Hiyo ndio nia ya Magaidi hushambulia pale au yule wanaye muona ni kikwazo kwao, asiye na kikwazo hawana habari naye.
Hamza aliwashambulia Maaskari kwa kuwa ndio walikuwa kikwazo kwake kwa nia yake ovu.
 
Je, alikuwa pekeyake? yuko mwenyewe?
Je, kwanini hasira ni kwa polisi?
Je, mmejifunza nini?
Mtu akiua polis ndio anakuwa gaidi?
 
Back
Top Bottom