Ndugu wa shujaa Hamza warejeshewe dhahabu zilizo porwa na mapolisi, tuanzie hapo.
kama kweli unazijua hizo dhahabu njoo polisi utoe maelezo fasaha, vinginevyo na wewe ni Gaidi uliyekuwa unashirikiana na Gaidi Hamza.
Hamza alifilisika kitambo alikuwa anaganga njaaa tu, Migodi yenyewe ni migodi ile au matuta ya viazi?!
Jeshi letu la Polisi Chunguzeni na mfuatilie nyenendo za baadhi ya wafuasi wa Chadema baadhi yao ni Magaidi. Mwenyekiti wao alisha wafundisha ugaidi
 
Hii inaitwa funika kombe mwanaharamu apite! Mbowe tunaemjua tunaambiwa ni Gaidi, sembuse marehemu Hamza tena ana asili ya Kisomali! 🤣
Nahisi mapolisi wana hamu ya kuona ugaidi halisi kama ktk nchi za wenzetu
 
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura amedai kuwa uchunguzi uliyofanywa na Jeshi la Polisi umebaini kwamba Hamza Mohammed alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga.

Hamza aliuawa na polisi Agosti 25, mwaka huu baada ya kuwaua kwa risasi askari wanne, watatu kati yao wa polisi na mmoja wa kampuni binafsi ya ulinzi jirani na ulipo ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Alhamisi Septemba 2, 2021 jijini Mwanza na waandishi wa habari Wambura amesema uchunguzi huo ulijikita katika mambo makuu matatu ambayo ni kutaka kutambua Hamza Mohammed ni nani, nini kilimsukuma Hamza kwenda kufanya tukio lile na kutaka kutambua mshiriki mwingine katika tukio hilo.

Wambura amesema katika uchunguzi huo polisi imebaini kwamba Hamza alikuwa akiishi kisiri huku akiwa amegubikwa na viashiria vyote vya ugaidi.

"Amekuwa akijifunza mambo mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii ambayo kwa kipindi kirefu amekuwa akijifunza mambo ya kigaidi kwa kuangalia mitandao ambayo inaonyesha matendo ya Al-Shabab na makundi kama ISIS yanayoendelea na wagaidi wengi hujifunza kupitia mitandao hiyo," amesema Wambura.

Amesema kwamba kitendo alichokifanya Hamza kilikuwa ni cha ugaidi wa kujitoa mhanga.

"Tabia na matendo ya Hamza aliyapata kupitia mawasiliano aliyokuwa nayo na watu wanaoishi katika nchi zenye matendo ya kihalifu ikiwemo ugaidi hasa wa kupitia mtandao yanayojulikana kama "Radicalisation through social media)," amesema Wambura.

Kuhusu taarifa zinazodai kwamba Hamza aliwashambulia askari hao kwa sababu walimdhulumu madini yake, Wambura amekanusha na kusema katika uchunguzi huo wamebaini kwamba Hamza hakuwa na madini wala fedha katika mazingira yale.

"Hamza hakuwa na madini wala pesa na hakuwa katika nafasi yoyote ya kumiliki madini wala pesa mbali ya kwamba watu wengi wameongea kwamba alikuwa anamiliki migodi ya madini kule Chunya na maeneo ya Makongolosi uchunguzi wetu umebaini hali hiyo ya maisha ilikwisha simama muda mrefu," ameongeza Wambura.

Wambura ameongeza kuwa taarifa ya uchunguzi huo pia imebaini kwamba Hamza alikuwa kwenye kundi la magaidi wanaoamua kuifia dini.

Chanzo: Mwananchi
Kama Taifa tunalenga wapi?Mama yuko busy kupiga mapicha ili kuitangaza nchi ya Tanzania,kuvutia watalii na wawekezaji,huku, Polisi wako busy kuichafua nchi kwamba Mbowe alitoa tshs laki 6 kufadhili ugaidi na Hamza alikua gaidi , huyu ni mmiliki halali wa silaha 😃😃😃
 
Polisi ni waongo sana, ile video baada ya Hamza risasi kuisha alinyoosha mikono, kwa askari wenye mafunzo kama ambavyo huwa wanajitapa, wangeweza kumkamata mzima mzima... cha ajabu waliendelea kulenga hewa tena wapo wengi... yaani ni aibu..
Wangemkamata na kumhoji, lakini walikuwa na nia ya wazi kupoteza ushahidi... wakaamua kummaliza

Askari hata shabaha hawana, kaanguka chini bado kwa uoga wakaendelea ku shoot kama hawaamini vile...

Yaani Hamza ukitizama alikuwa highly trained na umakini sana, angekuwa na magazine za kutosha angewalaza sana kwa sababu ya ujinga... lile askari lingine linafikiri sifa kusogea karibu na hatari kiasi kile... yaani ni vituko vitupu...

Hivi hawa polisi wana shida gani
Hakuna polisi atakaye hatarisha maisha yake - eti akukamate hai wakati umeua polisi mwenzake. Polisi hawawezi kukuamini kama utawaacha salama.
 
Hakuna polisi atakaye hatarisha maisha yake - eti akukamate hai wakati umeua polisi mwenzake. Polisi hawawezi kukuamini kama utawaacha salama.
Hamza aliwaua Polisiccm wawili tu wale wengine waliuana wenyewe kwa wenyewe kwa mjibu wa seleman 0715132277 msiri mkubwa wa Polisiccm mpigie atakupa story mwanzo mwisho
 


1631170835103.png

VIDEO: DCI asema uchunguzi wao umebaini Hamza alikuwa gaidi


Ndugu wa Hamza washangazwa na uchunguzi wa Polisi

Alisema hilo limebainika kupitia uchunguzi wao uliofanyika kwa kuzingatia mambo matatu ambayo ni kutaka kutambua Hamza Mohammed ni nani, nini kilimsukuma kufanya tukio lile na kutaka kutambua mshiriki mwingine katika tukio hilo.

“Na katika uchunguzi huu, polisi ilibaini Hamza alikuwa akiishi kisiri huku akiwa amegubikwa na viashiria vyote vya ugaidi,” alidai Wambura.

“Amekuwa akijifunza mambo mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii ambayo kwa kipindi kirefu amekuwa akijifunza mambo ya kigaidi kwa kuangalia mitandao inayoonyesha matendo hayo na magaidi wengi hujifunza kupitia mitandao hiyo.”

Hata hivyo, Wambura pia alikanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinazodai kwamba Hamza aliwashambulia askari hao kwa sababu walimdhulumu madini yake na kusema katika uchunguzi huo, wamebaini Hamza hakuwa na madini wala fedha.

“Hakuwa katika nafasi yoyote ya kumiliki madini wala pesa, mbali ya kwamba watu wengi wameongea kuwa alikuwa anamiliki migodi ya madini kule Chunya na maeneo ya Makongolosi.

Uchunguzi wetu umebaini hali hiyo ya maisha ilikwisha simama muda mrefu,” alisema.
 
Back
Top Bottom