DCI Manumba: mbunge wa arusha hakuguswa ni propaganda za Chadema tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DCI Manumba: mbunge wa arusha hakuguswa ni propaganda za Chadema tu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Malaria Sugu, Dec 26, 2010.

 1. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Eti kauli hii ya DCI manumba kwamba mbunge wa arusha mjini hakuguswa na polisi yaani kupigwa kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari, isipokuwa ni propoganda za chadema tu.
  pia Star tv waliporusha tukio lile kama kuwakumbusha watizamaji hata mimi sikuona sehemu ambayo mbunge yule alipata mkongoto bali nilimuona yeye akirusha ngumi kumpiga mkuu mmoja wa polisi. jee lipi liwe kweli?
  na kama alipigwa manumba kwanini asipeleke malalamiko yake Polisi

  source: star tv mjadala
   
 2. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Je kuna mtu aliyemwuliza huyo mbunge aliyepigwa? hizo source za mahojiano ya watu ambao hawakuwa kwenye tukio wala si wahusika haziaminiki. Mbunge bado yupo kwanini hakuna anayetuambia kuwa ameongea na mhusika na akatupatia ukweli?
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  CCM oyeeeeeeeeeeeee! teh... hauhitaji kumuona akiwa na kadi ya ccm ili umtambue.
   
 4. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2010
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Ulitegemea DCI aseme kwamba Lema alipata kichapo? Watanzania bado hatuna hulka ya kukubali makosa. Vyombo vyetu vya dola vipo kwa ajili ya watawala na si wananchi. Unapotamka kuwa lema hakuguswa unatukana wengi sana nakuchafua taaluma za watu wakiwemo madaktari waliopumzisha hospital
   
 5. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #5
  Dec 26, 2010
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  We are thinking in the same boat..madaktari waliomlaza na wao walifanya propaganda?? Mt Meru si hospitali kuu ya Mkoa??..Manumba nilikuwa nakuheshimu ila nimekushusha hadhi sana kwa hii kauli ya kibazazi.
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Dec 26, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Nani kasema kwamba monopoly ya kufanya propaganda ni ya CCM pekee??? Vyama vingine navyo vina haki pia kufanya propaganda!!!
   
 7. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #7
  Dec 26, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  SOMA HAPA-POLISI NI WALEWALE CCM TU-http://www.mwananchi.co.tz/component/content/article/37-tanzania-top-news-story/7550-mbunge-chadema-apigwa-na-polisi.html
   
 8. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #8
  Dec 26, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kati ya Manumba aliyoko Dar es salaam na RPC aliyo Arusha tukio lilipotokea tumwamini nana? Maana RPC wa Arusha alidhibitisha kuwa Mlema alipigwa kutokana na kukahidi maagizo ya polisi.
   
 9. m

  mams JF-Expert Member

  #9
  Dec 26, 2010
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hakyanani, kila kitu mnachakachua. Itafika zamu yenu muanze kujichakachua wenyewe!
   
 10. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #10
  Dec 26, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  unaweza ukakamatwa kwa nguvu kwa kukiuka amri halali ya kipolisi ya kujisalimisha na kutulia.....halafu wewe ukaleta vurugu....pale hupigwi bali unapunguzwa nguvu za kukaidi amri halali
   
 11. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #11
  Dec 26, 2010
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni jambo la aibu kwamba DCI Manumba na RPC wa Arusha hawakuwasiliana kabla ya Manumba kutunga hadithi yake hii eti Mbunge wa Arusha hakupigwa na Polisi.

  Sisi wakazi wa Arusha tumemsikia huyu RPC wetu akitamka kwamba Lema anachochea vurugu na tuliona Polisi waliopelekwa ukumbini mwa Halmashauri ya Manispaa wakimpiga Mbunge wetu. Tulimwona Mbunge wetu akiwa Hospitali ya Mkoa, Mt. Meru, akitibiwa. Hata Mganga wa hiyo hospitali alisema Lema amepigwa lakini anapata unafuu. Sisi tuliona ktk TV, polisi wakimkwida Lema.

  Sasa kama baada ya haya yote, Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Taifa, anatamka "Mbunge wa Arusha hakuguswa; ni propaganda za Chadema tu" sisi wananchi tutakuwa na imani na Polisi? Ni lazima Polisi waache ushabiki wao kwa CCM, wasibebe chama chochote cha siasa, kama wananuia kweli kutekeleza wajibu wao wa kuhakikisha haki na usawa kwa wananchi wote.

  This country will degenerate into chaos and violent conflagration, if the Police Force will continue with this kind of bias and one-sidedness. Woe unto us Tanzanians, if urgent steps are not taken to arrest this trend.
   
 12. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #12
  Dec 26, 2010
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Polisi wenyewe wamekiri kumupiga kawa maelezo kwamba wanaleta utulivu
  polisi wakumbuke kwamba pasipo haki hapana amani
  kama mtu asiye sitahili haki anapewa nayule anayesitahili ananyimwa mbele hiko ni hatari kwa poilisi!!!!!
   
Loading...