DCI Manumba: Kuna tishio la al-shabaab kushambulia Tanzania...

Status
Not open for further replies.
Amewaomba watanzania wawe macho na tishio la kushambuliwa kwa nchi yetu...bila kusema tujihami vp tukae nyumbani tu au tufanyaje....

Kama ni kweli ni taarifa muhimu otherwise isijekuwa wamepata kichaka kingine kuzuia maandamano ya katiba Oct 10!Just curious.
 
Amewaomba watanzania wawe macho na tishio la kushambuliwa kwa nchi yetu...bila kusema tujihami vp tukae nyumbani tu au tufanyaje....

Nashukuru kwamba Manumba ameliona hili, si kama hao "mbuni" wanaoweka vichwa vyao ardhini na kutuambia tuko salama, huku miili yetu iko exposed! WIZI MTUPU.

Manumba si mtu wa "usalama wa taifa". Wenye mamlaka hayo hawajachukua hatua stahiki kwa kuwa HAWAKUFUNDISHWA kuifanya kazi hiyo ipasavyo. Wao wanachojua ni kuulinda utawala; nchi ijilinde yenyewe. Bila kuwashirikisha wananchi, nchi itajilinda kwa namna gani?

Serikali yetu "ya kihuni" imekuwa ikiwapiga na kuwanyanyasa raia; ona Operation Kimbunga ilivyoendeshwa. Watu wanaporwa mali zao kwa kuwa tu ni washukiwa wa uhamiaji haramu. Watu wanakamatwa, wanafungwa, wanawekwa mahabusu, bila hata kupewa nafasi za kujitetea.

Halafu tunasema nchi ina amani?!

Kwenye suala zima la "usalama wa taifa" kuna matishio makuu mawili; tishio la ndani na tishio la nje. Tanzania tumeimarisha matishio yote; kwa upande wa ndani, wananchi hawaipendi tena nchi yao, hawaijali, hawaithamini, wanajiona heri kuhamia kwingine kuliko kuwa Mtanzania. Uzalendo umekufa. Kwa upande wa nje, mambo ni yale yale. Hakuna mwenye kupenda, kudiriki au kuthubutu kuilinda mipaka yetu. "Ni kazi ya Serikali", wanasema.

Mambo mengine ukiyasema unaambiwa we mchochezi. Wakubwa hawataki kuambiwa wala kusikia ukweli!

Mungu tunusuru!
 
hata raia wamechoka na serikali kiziwi na kipofu iliyojaa dharau na kejeli kila kitu chama tawala hata wakiambiwa mambo ya maana wanapinga tu,haya sasa wameanza na kodi ya sim card,je nani ataipenda serikali endawazimu?
 
Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Nchini, DCI Manumba amesema kuwa Al-Shabaab hawawezi kuishambulia Tanzania kwa sababu ina jeshi imara na mfumo bora wa intelijensia. Lakini pia amewataka wananchi kutoa ushirikiano pale wanapoona hali ya usalama inatishiwa na watu wasiofahamika.
Manumba amesema hayo kufuatia mashambulizi ya mfululizo ya wanamgambo wa Al-Shabaab yanayofanywa nchini Kenya.
Source:TBC News buletin,0800Pm

Je, kauli hii ya Manumba ina umakini wowote,na ni ya kuitumaini kwa kiasi gani?
Huyu manumba si ni yule aliyewahi kushambuliwa na vijidudu 500 wa malaria? Kapona kweli?
 
Wtz tunakuwa wapumbavu mpk kwenye vyombo vya habar vinataja mpk maeneo yatakayoshambuliwa na alshabab hapa tz. huu ni ujinga mkubwa kwa magazet haya ya tz. serikal inafaa walichukulie hatua kali gazet na mmiliki wake
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom