DC: Wanafunzi waongoza kwa maambukizi

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, amesema kundi lililoathirika na virusi vya Ukimwi kwa kiwango kikubwa wilayani humo ni vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 22.

Mushi alisema waathirika wengi katika kundi hilo ni wanafunzi wa sekondari na vyuo vikuu, huku akilitaka kundi hilo kujihadhari na ugonjwa huo.

Mushi alitoa taarifa hiyo katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

Alisema takwimu hizo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni ambapo Wilaya ya Ilala ina kiwango cha maabukizi ya VVU kwa asilimia 8.3.

“Manispaa ya Ilala imeadhimisha kwa kuruhusu kushirikisha watu na asasi mbalimbali za kiraia ili kila mwenye uwezo wa kutoa mchango au maoni awe wazi,” alisema.

Alisema katika kazi inayofanyika katika wilaya yake hivi sasa ni kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi mapya, kupunguza unyanyapaa na kukemea unyanyasaji kwa watu wanaoishi na VVU.

“Ni vema wananchi tuzingatie ushauri nasaha na kupima VVU kwa hiari, kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

“Kwa juhudi za kitaifa tumegundua njia za kuepukana na ugonjwa huu na kuudhibiti ni kutofanya tendo la ndoa, tuwe na uaminifu kwenye ndoa au kutumia kondomu,” alisema.

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, ikishirikiana na wadau mbalimbali walio katika mapambano dhidi ya UKIMWI, imeendelea kutekeleza kauli mbiu ya maadhimisho inayosema:

“Tanzania bila maambukizi mapya ya UKIMWI na unyanyapaa na vifo vitokanavyo na UKIMWI inawezekana”.
 
Hili suala lishakuwa na utata. Badala ya kupunguza maambukizi yanaongezeka. Pamoja na elimu yote wanayotoa.? Mi nadhani wakati umefika kuwakabidhi vitengo wale walioathirika ndo wasaidie kupunguza hili janga. Kwani pesa nyingi za miradi na elimu ya ukimwi zinaishia kununua magari yenye viyoyozi, kujenga nyumba za wajanja na waathirika wakikosa dawa au kuletewa dawa feki. Imagine ungekuwa wewe umeletewa dawa feki na Y ambaye unajua anga zake ungefanyaje? Mama yangu mi ningeenda kuwaambukiza kwa makusudi ili na ye aonje kadhia yake.
 
Back
Top Bottom