DC wa zamani hoi kitandani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DC wa zamani hoi kitandani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Nov 8, 2010.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,497
  Likes Received: 19,910
  Trophy Points: 280
  DC wa zamani hoi kitandani Send to a friend Monday, 08 November 2010 01:13 0diggsdigg

  [​IMG] Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbalali, Mkoani Iringa Hawa Ngurume, akizungumza na waandishi wa habari wa gazeti hili, nyumbani kwake Goba Kinzidi, Dar es Salaama jana, kuhusu maradhi ya figo yanayomsumbua. Picha na Venance Nestory

  Raymond Kaminyoge
  ALIYEKUWA mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Hawa Ngulume yuko katika hali mbaya nyumbani kwake, Goba Kinzudi jijini Dar es Salaam akisumbuliwa na ugonjwa wa vichomi na mapafu.

  "Nimeona nitumie chombo cha habari kufikisha ujumbe (wa ugonjwa) kabla sijafa," alisema mkuu huyo wa zamani wa alipoongea na Mwananchi.

  Akizungumza na Mwananchi nyumbani kwake jana, Ngulume alisema kwa miezi mitatu sasa yuko hoi na hawezi kutembea bila kusaidiwa na hivyo anaiomba serikali imsaidie aweze kwenda kutibiwa nje ya nchi.
  Alisema ameamua kutumia gazeti hili kufikisha ujumbe kwa serikali na CCM kuhusu maradhi yanayomsumbua baada ya njia nyingine kushindikana.

  "Nilipeleka taarifa kwnye chama changu kwamba ninaumwa nahitaji msaada, lakini sikujibiwa; pia nimefanya juhudi za kutaka kumwona Waziri Mkuu ili anisaidie, lakini juhudi hazikuzaa matunda. Nimeona nitumie chombo cha habari kufikisha ujumbe kabla sijafa," alisema.

  Ngulume, ambaye ni kada maarufu wa CCM aliyetumikia nafasi ya ukuu wa wilaya kwa miaka 18, alisema maradhi hayo yalianza kumsumbua baada ya kumalizika kwa mchakato wa kura za maoni za chama hicho.

  Alisema aliomba ridhaa ya chama hicho kimsimamishe kuwa mgombea ubunge katika Jimbo la Singida Mjini.
  "Katika mchakato ule Mohammed Dewji alishinda, na mimi nikawa mshindi wa pili. Niliporudi Dar es Salaam nikaanza kujiandaa kwenda kumpigia debe mshindi kama ulivyo utaratibu wa chama chetu, ndipo nikaanza kuumwa ghafla," alisema.

  Mkuu huyo wa zamani wa wilaya ambaye amewahi kushika wadhifa huo kwenye wilaya mbalimbali zikiwemo za Bagamoyo, Ilala na Kibaha, alisema amekuwa akitibiwa katika hospitali za Lugalo, IMTU na Ocean Road
  "Kuna kipimo ambacho nilitakiwa kuwekewa kwenye kinywa katika Hospitali ya Ocean Road ili kiweze kubaini kama kwenye mapafu kuna maji au la, lakini ilishindikana kwa sababu ya kukosa pumzi, na hawana kipimo cha aina nyingine," alisema.

  Alishauriwa kwamba aendde India ambako kuna vipimo vya aina nyingi ambavyo havihitaji kuwekwa katika kinywa na kwamba vipimo hivyo vingemfaa kutokana na matatizo yake ya pumzi.

  Alisema katika kuhangaika alifika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, lakini cha kushangaza alikaa kuanzia saa 8.00 mchana hadi saa 11.00 jioni bila kuhudumiwa.

  "Ndipo mtu mmoja anayenifahamu aliyekuwa akipita nilipoketi, akanisalimia kwa kuniita mheshimiwa. Muuguzi mmoja jina ninalihifadhi akaja kutaka kunihudumia, nikamwambia ina maana siwezi kupata huduma hadi niwe mheshimiwa, nikaondoka kwa hasira," alisema.

  Alisema baada ya kutelekezwa na kunyanyapaliwa Muhimbili, amekuwa akipata matibabu kwenye hospitali za binafsi kwa ajili ya kutuliza maumivu.

  "Maumivu ninayoyapata ni makali sana, nina vichomi utadhani kuna msumemo unaokata viungo vyangu ndani ya tumbo. Ninalia usiku kuchwa kwa maumivu, wanaonisaidia ni majirani tu ambao hufika kila mara kunijulia hali," alisema.
  source:mwananchi

  hili limenishtua ..lakini hii ndio picha halisi
   
 2. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Dah hii habari inasikitisha saana

  Kimsingi wanasiasa wanapostaafu wanakuwa na hali ngumu saana,,Sipati picha kama na cheo umeshindwa kuwasiliana na PM je mwananchi wa kawaida itakuwaje????

  ukitafakari saana wanasiasa wengi wanajitahidi kujilimbikizia mali kwa namna yeyote ili hali kama hii isije ikawapata,,

  Pole saana Mama Ngulume,, Mungu yu mwema atakusaidia
   
 3. Kagemro

  Kagemro JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2010
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  malipo ya Mungu ni hapahapa duniani,wakati ananguvu alikuwa anatoa maneno machafu mdomoni hakujua siku moja ataijua taabu,Eeeeeeeeeeee Mungu libarikiwe jina lako.
  Wewe ni Mungu wa Kisasi.AMEN
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Pole mama umeugua kipindi kigumu waheshimiwa walikuwa bize kuchakachua matokeo ..labda kwa sasa watakusikia na kukusaidia..Lakini kweli huna hata namba ya simu ya Mkwere?aaaah mamaaaaa usiniangushe hivo bana.Maana hata ukituma meseji huwa anajibu
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Nov 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,497
  Likes Received: 19,910
  Trophy Points: 280
  huwezi kutoa maneno kama hayo bro!!!kwanza hayaendani na status yako lol!!
   
 6. M

  Mutu JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa nn asifanye kama watu wengine apitishe bakuri ,waziri mkuu atafanya nn ?

  Kwa kweli namuombea afanikiwe atibiwe ila notion ya kwenda kwa waziri mkuu naona si nzuri .
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Nov 8, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  wilaya ya Mbarali iko Mbeya, sio Iringa! Pole sana mama, mafisadi huwa hawana shukrani, hata kama mlisaidiana kuchakachua kura za maoni, they don't care!
   
 8. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #8
  Nov 8, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,792
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  Bora ujionee mwenyewe uzuri wa ccm!ndio maana wanahakikisha na watoto wao waendelee kwenye system.
   
 9. g

  grandpa Senior Member

  #9
  Nov 8, 2010
  Joined: Aug 24, 2008
  Messages: 185
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Chickens have come home to ...............
   
 10. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #10
  Nov 8, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nakupa sanksi kwa kumjua mi binafsi nimewahimtukana akiwa kinondoni ka dc.
  Majivuno kwa sana ndo maana nadhani kasuswa
   
 11. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #11
  Nov 9, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa ujeuri haka ka binti kalikuwa kajeuri saaana, dharau dharau hivi na majibu magumu magumu but anyway anahitaji msaada maana hakuna mwanadamu asiye na kasoro any way......
  Hawa....MUNGU KWETU SISI NI KIMBILIO NA NGUVU
  MSAADA UTAKAOONEKANA TELE WAKATI WA MATESO (Zaburi 46:1)
  Ukikimbilia wanadamu wana dis appoint saaaana kwani wao 'hawajajaa rehema, si wenye huruma nyingi na ni wepesi wa hasira.......
  Badilisha kimbilio nawe utapona.......

  mix with yours
   
 12. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #12
  Nov 9, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Sikupenda Leadership style yake huyu mama, she was too arrogant kiasi alipokuwa akitokea kwenye TV nilikuwa nazima. Lakini life is a cycle. Na wenye hekima hukimbilia utimilifu wa cycle hiyo.

  Ina maana haku-fisadi akaweka akiba au pesa zote aliziwekeza singida kupambana na dewji?
   
 13. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #13
  Nov 9, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ..nadhani angeenda pia radio RFA kuna kile kipindi cha kila siku ya jumapili watu wenye matatizo hujieleza kutafuta msaada. Hilo wazo la kwenda kwa waziri mkuu amenitia kichefu chefu sana ina maana hata wale wadanganyika wanaokosa huduma za afya na kuishia kuhangaika nao waende kwa waziri mkuu???:nono::nono:
   
 14. M

  Matarese JF-Expert Member

  #14
  Nov 9, 2010
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kweli dunia duara! Wandugu wenye moyo wamsaidia jamani kwani ndiyo dini safi, ila pia hili liwe funzo hasa kwa wale waliopo madarakani,
  that " BE NICE TO PEOPLE ON YOUR WAY UP BSE YOU MIGHT MIGHT THEM ON YOUR WAY TO THE BOTTOM".
   
 15. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #15
  Nov 9, 2010
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mama ngulume pole sana , lakini nakusihii kumbuka kutubu mbele za mungu kwani hakuna asiye na makosa.
  Zipo taarifa kuwa ulimpiga kibao muwakilishi wa kijiji wilayani mbalali aitwaye ofledi mkemwa mbele ya kamati ya bunge na alikushitaki.
  Mama tubu hiyo ndo safari usione aibu mafisadi hawana huruma!!!!
   
 16. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #16
  Nov 9, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mimi naomba yeyote aliye na mawasiliano na ndugu wa huyu Mama ngulume awashauri wampeleke kwa watu wa Mungu. Wapo wengi sana KAKOBE,GWAJIMA, MAMA LWAKATARE, MZEE WA UPAKO nk. Mungu atamponya. Hata kama yeye ni Muislam aamini tu kuwa Yesu anaponya Asinganganie dini afu akapoteza afya. Mimi nampa pole sana mama Ngulume, lakini nazidi kumsihii akumbuke kutubu mbele za mungu kwani hakuna asiye na makosa.
  Kama kuna mabaya mama Ngulume ulifanya tubu okoka mrudie Mungu hatakuacha!
   
 17. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #17
  Nov 9, 2010
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,111
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180

  mungu amponye maana tusirudishe visasi
  ila huyu mama jamani anaongea anajibu kama ****** akiwa mkuu wa wilaya kumwona majibu yake kkaribu na kumvua mama yako nguo wewe ni mungu unayeponya ukamponye mama huyu na shida zake hasa kipindi hiki kigumu
   
 18. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #18
  Nov 9, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,860
  Trophy Points: 280
  Alimpiga makofi mtendaji mmoja kule Mbarali...labda haya ndio malipo yenyewe...si aliolewa na kaka wa JK huyu?Na mbona Sheikh wa CCM hamsaidii ?
   
 19. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #19
  Nov 9, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Yule aliyemtandika kofi kule Mbarali - kama yupo hai atakuwa anajisikia auheni -I thought yule mwekezaji "muhindi" angemsaidia kumpeleka India?

  CCM ina wenyewe! Ukitoka kwenye mduara you are dead and forgotten! Hivi Mzee Philip (Former CCM Party Chairman) umemwona sehemu yoyote katika mchakato wa uchaguzi ulioibwa? Ameshaulika as if he never existed on this country!

  Kwahiyo wewe uwe ni fundisho kwa wale wote wanaosimama kwenye majukwaa na kuhubiri maisha bora - uliyokutana nayo Muhimbili ni order of the day kwetu sisi - Wengine tumeshawazika Wapendwa wetu wengi tu kwa kukosa pesa ya operation ya Apendiksi!
   
 20. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #20
  Nov 9, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,860
  Trophy Points: 280
  Wewe hujakumbana nae enzi zake huyu...pole

  Huyu mama alikuwa mfagizi pale Tanzania Audit Corporation enzi za Chama kushika hatamu...halafu akawa kiongozi wa UWT na baadae akawa kingozi wa mbio za mwenge miaka ya 1980s ndio akakutana na tingatinga likampandisha kuwa DC baada ya kumegana...hata darasa la nne hajafika
   
Loading...