DC wa Wilaya Mpya atuhumiwa kuhongwa ‘Shangingi’ na Mwekezaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DC wa Wilaya Mpya atuhumiwa kuhongwa ‘Shangingi’ na Mwekezaji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 20, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  Na Happiness Mtweve, Dodoma

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  MKUU wa Wilaya mpya ya Momba, mkoani Mbeya, Abiud Saideya, ametuhumiwa kuhongwa gari la kifahari na mwekezaji mmoja ili akubali kuwahamisha wananchi waliokuwa wanaishi karibu na maeneo yaliyotengwa kwa ajili hifadhi (WMA) katika Wilaya ya Meatu.


  Akiuliza swali la nyongeza bungeni jana, Mbunge wa Meatu, Meshack Opulukwa (CHADEMA), alidai kuwa Saideya alipokea hongo hiyo kwa ushirikiano na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ambaye hata hivyo hakumtaja jina.

  Huku akisikilizwa kwa makini, mbunge huyo aliendelea kudai kuwa tukio hilo lilitokea mwaka 2007 lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na serikali licha ya taarifa mbalimbali kutolewa.


  “Mheshimiwa Naibu Spika, naitaka serikali kutoa majibu ya kina hapa. Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Meatu kwa kushirikiana na OCD, alihongwa gari aina ya Land Cruiser GX T 147 ASX na mwekezaji anayefahamika kwa jina la Mwiba Holding Ltd, ili kuwahamisha wananchi waliokuwa wanaishi karibu na maeneo ya WMA, huu ni uzembe mkubwa kwa kiongozi lakini serikali iko kimya,’’ alisema Opulukwa.


  Alidai kuwa Saideya aliwatetea wawekezaji hao wakati akiwa mkuu wa wilaya hiyo kabla ya kuhamishiwa Wilaya ya Mombo.


  Baada ya Opulukwa kutoa tuhuma hizo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, aliomba mwongozo wa spika na aliposimama alimtaka mbunge huyo kuthibitisha kauli yake kwa kumtuhumu mtu ambaye hawezi kujitetea bungeni.


  Akitoa mwongozo huo, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alimtaka mbunge huyo kutoa uthibitisho kwa spika katika kipindi cha siku saba kuanzia jana ili kuona kama tuhuma hizo ni za kweli au la.


  Akizungumza nje ya ukumbi wa Bunge, Opulukwa alisema kuwa taarifa hizo ni za kweli na kwamba alishawahi kumpa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, tangu Februari mwaka huu lakini hajazifanyia kazi.


  Alisema Pinda aliahidi kuunda tume kuchunguza tuhuma hizo lakini cha kushangaza hadi leo hajafanya hivyo.


  “Nimeshangazwa wiki iliyopita katika maswali ya papo kwa hapo, Waziri Mkuu alisema kuwa jambo hilo linaonekana kupoa, linapoaje wakati hajatuuliza mimi na mbunge mwenzangu, Mpina, kama kweli lilishapoa?” alihoji.


  Katika swali la msingi, Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) alilolielekeza Wizara ya Maliasili na Utalii, aliihoji serikali kama inafahamu matatizo na migogoro iliyopo katika Pori la Akiba Maswa na kama inajua watu wangapi walikufa katika migogoro hiyo.


  Naibu Waziri wa Maliasi na Utalii, Lazaro Nyalandu, alisema kumekuwa na migogoro mikubwa katika pori hilo ambayo imesababisha vifo vya watu sita, kati ya hao watatu ni askari wanyamapori katika kipindi cha mwaka 2005 hadi sasa.


  Alisema tayari serikali imeunda tume huru ya uchunguzi itakayofanya kazi kwa muda wa siku 30 kabla ya kutoa majibu yake kwa hatua zaidi.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  How nice... NI Mkuu wa Wilaya Mpya kaisha pata Ulaji? Shangingi Mpya Hiyoo...
   
 3. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  ndio maana wabunge walimkomalia pinda hana maamuzi kuhusu wateule wa rais!

  :
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  pinda anasema suala hilo lilishapoa, khaa kweli serikali dhaifu mno
   
Loading...