DC wa Tunduru Julius Mtatiro, asimamia upigaji viboko kwa watoto Watoro Issa na Farid

pantheraleo

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
691
878
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Ndg. Julius Mtatiro ameendeleza kampeni ya kiwilaya ya kupambana na utoro sugu, nidhamu za wanafunzi na mimba za utotoni wilayani Tunduru, na leo amewaelekeza walimu kuwaadhibu watoro sugu mbele ya wazazi wao na amezionya pande zote zinazohusika na uzembe huo.

Katika kampeni hiyo Ndg. Mtatiro ameelekeza wazazi wa wanafunzi sugu kwa utoro na watoto wao wajisalimishe kwenye shule zote za Sekondari na Msingi katika wilaya hiyo.

Katika kutekeleza agizo hilo watendaji wa kata, waratibu elimu kata na walimu wa shule zote wameendelea kutoa adhabu kwa wanafunzi hao na kuwaonya wazazi ambao wameshindwa kuwasimamia watoto.

Akiwa katika Shule ya Sekondari ya Ligoma iliyoko tarafa ya Namasakata Wilayani Tunduru Ndg. Mtatiro amewaonya wazazi wa watoto sugu kwa utoro kuwa hatua zinazoendelea kuchukuliwa katika wilaya nzima ni kali mno dhidi yao. "Rais Magufuli na serikali yale anatenga Shs Bilioni 23.6 za kitanzania kila mwezi ili msome bure, nyinyi na wazazi wenu mnachekeana na kupuuza masomo, mnalifanya taifa linapoteza fedha nyingi na Rais anahangaika kutumia kodi za watanzania ili watoto wenu wapate elimu wawe na maisha bora lakini mnapuuza juhudi hizo", ameeleza mhe. Mtatiro.

Ndg. Mtatiro amewaelekeza maafisa wote wanaosimamia elimu na utawala katika vijiji na kata za Tunduru kuendelea na msako mkali kuhakikisha watoto wote wanaendelea na masomo na ikibidi wazazi wachukuliwe hatua kali, maelekezo hayo yameanza kutekelezwa na wazazi wengi ambao wanawasalimisha watoro sugu kwenye shule zao.
 
Hapo juu umesema kuwa ni watoto wa wanyonge kwahiyo na wewe ni mnyonge?
 
Watoto wa wanyonge wana haki ya kutokwenda shule sio then mbona hajawapiga wamepigwa na mwalimu wao yeye akiwa pembeni
 
Viboko vinaumiza au vinafundisha?,jibu ni vinafundisha,watoto wa siku hizi ni manunda Sana,wazazi kuwapenda Sana watoto wao ,bila kuwaadhibu wanapokosea,ni kuwaharibu watoto
 
Mtoa mada, zamani mtoto alikuwa wa wote, yaani mzazi/mlezi/mtu yeyote alikuwa na uwezo wa kumuadabisha mtoto wa mtu yeyote na mahali popote hata iwe njiani bila kujali ni mtoto wa nani ili mradi kafanya makosa yasiyokubalika, leo wazazi mnaanza stori za eti mtoto wangu achapwe na mtu fulani ila asichapwe na mtu fulani. Nyie ndiyo wazazi mnawafuata walimu kuwahoji kwanini wamewaadhibu watoto wenu. Hii tabia ni ya kukemea, mbali ya kwamba huyo Kiongozi kaamuru watoto wachapwe kwa kutumia cheo chake lakini kwa upande mwingine huyo anaweza kuwa kama mzazi au mlezi. Lakini kwa upande wa pili we mtoa mada unaona ni sahihi watoto kuendelea kuwa watoro? Wakati mwingine wazazi tunaweza kujikuta tunaharibu watoto wetu wenyewe. Mi kama mzazi na mlezi napendezwa sana na mzazi/mlezi kumuadhibu mwanangu mahali popote na wakati wowote pale anapofanya mambo amabayo hayaruhusiwi ikiwa ni pamoja na masuala ya utovu wa nidhamu.
 
Mtatiro anakuwa kama hajaenda shule. Anashindwa kukaa na wazazi na kujadili sababu zinazopelekea watoto kutoroka. Akiwa kama muakilishi wa rais watafute uvumilivu.

Viboko alitumia Mjerumani ili tulime mkonge
 
Mtoa mada, zamani mtoto alikuwa wa wote, yaani mzazi/mlezi/mtu yeyote alikuwa na uwezo wa kumuadabisha mtoto wa mtu yeyote na mahali popote hata iwe njiani bila kujali ni mtoto wa nani ili mradi kafanya makosa yasiyokubalika, leo wazazi mnaanza stori za eti mtoto wangu achapwe na mtu fulani ila asichapwe na mtu fulani. Nyie ndiyo wazazi mnawafuata walimu kuwahoji kwanini wamewaadhibu watoto wenu. Hii tabia ni ya kukemea, mbali ya kwamba huyo Kiongozi kaamuru watoto wachapwe kwa kutumia cheo chake lakini kwa upande mwingine huyo anaweza kuwa kama mzazi au mlezi. Lakini kwa upande wa pili we mtoa mada unaona ni sahihi watoto kuendelea kuwa watoro? Wakati mwingine wazazi tunaweza kujikuta tunaharibu watoto wetu wenyewe. Mi kama mzazi na mlezi napendezwa sana na mzazi/mlezi kumuadhibu mwanangu mahali popote na wakati wowote pale anapofanya mambo amabayo hayaruhusiwi ikiwa ni pamoja na masuala ya utovu wa nidhamu.
Hao watoto waliochapwa na watu wote si ndiyo wamekuwa viongozi aina ya Kim Jong, hawana confidence na upinzani umekuwa uadui.
 
Hivi huyu mtoa mada alikuwa na lengo lipi? Je, anatetea utoro? Je, anadhani mtoto akifeli ni hasara kwa nani? Hivi huyu pantheraleo ana akili timamu hasa ukiangalia title na maelezo yake? Mirembe inawangojea wengi itabidi ipanuliwe siku zijazo
 
Wapi wale wazee wa moshi ufukao...

Anyway, watu wa kusini jioneeni huruma himiza watoto waende shule muikomboe kanda yenu maana ipo nyuma sana kimaendeleo
 
Kulikuwa na haja gani kuandika majina ya hao watoto kwenye heading badala ya kwenye babari yenyewe
 
Zamani babu zako walikuwa wanavaa ngozi za wanyama na magome ya miti kama nguo

Back
Top Bottom