DC wa Tabora Mjini anafanya kazi kwa kufuata miongozo na maadili ya kazi na kiapo cha maadili ya utumishi wa umma

Nyasa Girl

Member
Jul 11, 2017
10
19
Ndugu wana JF

Mitandao ya kijamii ,hasa mtandao unaoheshimika Tanzania wa Jamii Forums ,umekuwa ukitumika na watu mbalimbali wenye nia njema na watu wenye nia ovu, lakini tuhuma zinapotokea lazima zijibiwe ili kuweka rekodi sawa dhidi ya upotoshaji na uchafuaji wa viongozi unaofanywa na wazandiki wachache Wanaopenda kuchafua taswira ya viongozi mbalimbali nchini.

Turudi kwenye mada ya kuleta bandiko hili, Leo Kumetokea tena andiko liliandikwa na watu walewale na kakikundi kalekale katika wilaya ya tabora na sisi hatutachoka kujibu uzushi kwa ustawi wa wilaya ya tabora Mjini, andiko hilo ambalo linamtuhumu Dc wa tabora mjini ,Mh. Komanya Kitwala kwa mambo yahusuyo elimu, mwanzo walileta tuhuma tukajibu na leo tunajibu kwa ushahidi wa jukwaa la viongozi wa elimu mkoa wa tabora (TAHOSSA) , kiufupi hayo mambo ni ya kutunga na uzushi mkubwa ambao unazushwa na wanufaika wa ufisadi na watu waliozoea kufanya kazi kwa mazoea.

Uzi wa tuhuma huu hapa

Umoja wa Wakuu wa Shule Manispaa watangaza Mgogoro na DC wa Tabora Mjini Mh. Eric Komanya Kitwala.

UKWELI HUU HAPA FUATANA NAMI;

1: DC wa tabora Mjini Anafanya kazi kwa kufuata miongozo na maadili ya kazi na kiapo cha maadili ya utumishi wa umma , hafanyi kazi kwa kiki , maana yeye sio msanii wa bongofleva bali ni mtumishi wa umma, hivyo watumishi wa umma wanatambua miiko ya kazi na hivyo watafanya kazi na wataendelea kufanya kazi kwa viapo vya kazi zao.

2: Shughuli za kielimu zinafanywa kwa Utaratibu , kwa masuala ya elimu kuna chama cha walimu wilaya (CWT), CWT hawana taarifa za uzushi huo , hawajakaa kikao chochote cha maamuzi ,hili linalofanya hivi ni genge la wahuni tu ,ambao wanakwamisha maendeleo ya elimu wilaya ya tabora.

3: Umoja wa TAHOSSA, hauna habari zozote kuhusu kakikundi haka kakupinga maendeleo ambako kalikuwa kananufaika na wizi kudhibitiwa na muda si mrefu katafahamika maana kanafanya hujuma dhidi ya serikali na kuingiza taasisi zisizo husika katika njama zao.

4: Mkuu wa Wilaya hajawahi kutoa lugha ya dhihaka kwa Mkurugenzi hata siku moja ama kumdhalilisha hizi ni njama za watu hawa waovu kuendelea kuleta ugomvi kati ya DC na Mkurugenzi kwa manufaa yao na viongozi hawatakubali kugawanyika, lengo ni kuwatumika wana tabora mjini na kuwaletea maendeleo.

5: Mkuu wa Wilaya ametuhumiwa kuwa yeye anasimamia ujenzi wa madarasa wakati sio kweli. Ipo Kamati ya Ujenzi inayosimamiwa na ndugu Ndamayape na akaunti ya malipo inaingia Manispaa ya Tabora, Mkuu wa Wilaya ama Ofisi yake haijawahi kupokea mchango wowote wa ujenzi.

6: Kuhakikisha hawa watu ni wahuni na wachonganishi nanukuu maneno ya Mwenyekiti wa TAHOSSA wilaya ya tabora pia, kuelezea Ukweli wa hawa wahuni ,Maneno ya Mwenyekiti wa TAHOSSA, Ndugu Lydia Mwampamba anasema “ Wandugu naheshimu sana viongozi wangu kwa kuwa ndio wanaoninifanya niwe hivi nilivyo, kama ningekuwa na ugomvi na mheshimiwa DC ningemfuata private, Ninadeclare kuwa mimi ni Mwenyekiti wa shule za sekondari, kikao kilichokaa kujadili kutompa ushirikiano wa kikazi DC sikijui naomba ndugu wana tabora mpuuze huo uzushi ambao umeandikwa Jamii forum,mimi Mwenyekiti wa TAHOSSA sijaitisha kikao chochote cha kumjadili DC. Hivyo hizo tuhuma zipuuzwe pia huyo mtu au hilo genge litafutwe na kuchukuliwa hatua za kinidhamu maana wanachonganisha viongozi” MWISHO WA KUNUKUU

Maneno haya Mwenyekiti wa TAHOSSA ameyaandika leo, saa 5: 17 jioni ,katika group la whatsaap la viongozi wa tabora Mjini kujibu andiko lililoletwa na ndugu King kasala, aliye share kutoka Jamii forum.

Ndugu wanatabora tuendelee kushikana na DC ili kuleta maendeleo ya wilaya yetu, sisi kama wana tabora tunasimama na DC ,maana tunafahamu hii vita ni chuki kwa sababu ya kuziba mianya mingi ya rushwa na hivyo kupelekea genge la waliobanwa kukimbilia mtandaoni ili kuchafua taswira ya DC na wana tabora kwa ujumla, maana walizoea kujiapa tenda, na kazi mbalimbali bila kufuata utaratibu sasa wana tafuta namna ya kumchafua DC ili akate tamaa, lakini tutampa DC moyo wa kuendelea kuiongoza tabora maana kazi yake ni kubwa kwa muda mfupi na changamoto anazitatua kwa haraka sana zikiwamo kuongeza madarasa na madawati kwa wanafunzi
 
Mkuu!

Unachofanya hapa ni kuzidi kuchafua image ya DC. Natoa "pro bono" on image building next time utalipia kidogo.

1. Lazima ujuwe kuwa watu hawatasoma hiki ulichoandika zaidi wata criticize nakuona ni upupu.

What to do?

Hapa tumia CSR ( Corporate social Responsibility) yaani wao wamekuchafua wewe nenda kwa jamii na media zako tatu kama Millard ayo, Mwanachi na ITV walipe vizuri hakikisha taarifa inatoka.

Au laa

Just fanya tukio la kijamii lakini hakikisha linaonekana na jamii nzima kwa maana Local Radio za Tabora nk.

2. Omba interview kwenye morning talk ya Local Radio kuelezea miradi yako miwili au mmoja kwa namna gani unawaomba wana Tabora wa wilaya yako sasa wakuunge mkono wewe na of course JPM.

3. Hakikisha haurudii hii mistake ya kutuma watu au wewe mwenyewe kujielezea kwenye mitandao "ni utoto" na unazidi kujipaka matope.

4. Kwa uchache ni haya kwa zaidi unaweza kuja DM tukayajenga.
 
Wewe acha uongo huyo Pimbi Komanya hamna DC hapo ni kwa sababu tu kuwa na udugu na jiwe ,kwa sababu ni uvccm aliyeingizwa usalama wa taifa,Jiwe anamlinda ni Pimbi wa kutupa,Kila alipoenda Tabora na kuitisha kikao hapo Tabora ameongea lugha za ajabu,matusi na hakuna kikao hata kimoja amewahi kukimaliza salama anamfokea mpaka kumtukana mkuu wa mkoa mbele ya watumishi wa mkoani,yaani huyo ni empty head , tabulalasa,premature imbecile .Hata ubabe basi tumia na akili.Wewe mleta mada bisha tushushe video zake.Ccm mjifunze sio kila anayeshinda kura za maoni anafaa kuwa rais,mmesukumiza lihutu limezalisha wakuu wa mikoa na wilaya wahutu wengi sana akiwemo Komanya.
 
Daaah, umeenda mbali sana.
 
Hebu rudia hiki kipande kwanza, yani DC anamfokea RC? Ni ngumu kuliamini hili na RC mwenyewe yule sukuma ndani? I don't buy this story.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe acha uongo huyo Pimbi Komanya hamna DC hapo ni kwa sababu tu kuwa na udugu na jiwe ,kwa sababu ni uvccm aliyeingizwa usalama wa taifa,Jiwe anamlinda ni Pimbi wa kutupa,Kila alipoenda Tabora na kuitisha kikao hapo Tabora ameongea lugha za ajabu,matusi na hakuna kikao hata kimoja amewahi kukimaliza salama anamfokea mpaka kumtukana mkuu wa mkoa mbele ya watumishi wa mkoani,yaani huyo ni empty head , tabulalasa,premature imbecile .Hata ubabe basi tumia na akili.Wewe mleta mada bisha tushushe video zake.Ccm mjifunze sio kila anayeshinda kura za maoni anafaa kuwa rais,mmesukumiza lihutu limezalisha wakuu wa mikoa na wilaya wahutu wengi sana akiwemo Komanya.

Mhhhh! 🙊
 
Back
Top Bottom