Dc wa korogwe asweka watendaji wa halmashauri ya wilaya ya korogwe polisi. Je ni haki? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dc wa korogwe asweka watendaji wa halmashauri ya wilaya ya korogwe polisi. Je ni haki?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by asanteni, Jul 8, 2012.

 1. a

  asanteni New Member

  #1
  Jul 8, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli inasikitisha sana kwa utendaji wa aina hii wa viongozi wa Serikali! Unavunja nguvu watumishi na hivyo kuzorotesha utendaji.

  Mnamo juzi 5 julai 2012 kama sikosei ni siku ya alhamisi DC wa Korogwe (Mrisho Gambo) alimsweka ndani mhandisi wa maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe eti kisa ni kuandaa BQ (Bill of Quantity) mbili ambazo moja inaonyesha gharama ya kurekebisha kabisa sehemu ya barabara na mabomba yaliyoharibiwa kutokana na kutengeneza barabara ktk eneo la hale (major repair) kiasi kama cha Tshs 81m, na BOQ nyingine iliyoandaliwa ni ya kurudishia mabomba hayo katika kiwango cha minor repair kiasi kama cha Tshs. 30m.

  Sasa mh. DC baada ya kuisoma BOQ hiyo ya 81m ukawa ugomvi mkubwa na mhandisi wa maji kuwa kuna uwizi umefanyika. Sasa sijui DC huyo kwa kuwa ni mgeni na asiyependa kujifunza taratibu za Serikali n.k akatumia vibaya power aliyopewa kumweka ndani Mhandisi eti wizi umefanyika! Kwa mujibu wa taratibu wizi gani umefanyika wakati hata tenda haijatangazwa, kazi haijafanyika na fedha haijalipwa? Pia alimsweka ndani kwa sababu alikuta eti mhandisi huyo amesafiri kwenda Arusha na hivyo hakumuheshimu na amemkimbia baada ya kufanya ubadhirifu huo wakati kiukweli mhandisi huyo alipewa ruhusa na Mkurugenzi, na DC huyo alielezwa hivyo lakini kwa kuwa ni mbabe/dikteta akaamua kumweka ndani.

  Pia DC anatakiwa kumweka ndani mwananchi yeyote endapo anahatarisha amani ya wilaya yake. Sasa najiuliza ni amani ipi aliyohatarisha mtumishi huyo? Kama mtumishi huyo alipofanya kosa hilo na tuhuma zinakaletwa kwa DC, kama mtumishi ni wa Halmashauri ilitakiwa awasiliane na Mkurugenzi wa Halmashauri ili kupata ukweli, na Mkurugenzi kwa kutumia Afisa Utumishi(msimamizi wa nidhamu na sheria za utumishi), Mkaguzi wa Ndani, Mhandisi Mkuu (mkuu wake wa idara), Mchumi(Msimamizi wa miradi) n.k angewaagiza wafanye uchunguzi. Kama ikithibitika basi mtumishi huyo angechukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria za utumishi ambapo maamuzi hayo yangebarikiwa hubarikiwa na baraza la madiwani ambalo DC ni mjumbe wake. Au kama DC hana imani na Kkurugenzi wa Halmashauri angelifikisha suala hilo ktk kamati yake ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ambayo kwa pamoja wangeiomba TAKUKURU, Usalama wa Taifa (ambao ni wajumbe wa kamati hiyo) wafanye uchunguzi then kama ingeonekana ana kesi ya kujibu wangepeleka kwa State Attorney naye angepitia na mwisho kama State Attorney angeona inafaa kwenda mahakamani angekamatwa na polisi tayari kwa kupelekwa mahakamani ambapo napo angepewa au asingepewa dhamana na kesi ingeendeshwa na mwisho kama ingethibitika ana kosa ndipo angehukumiwa na mahakama.


  Sasa cha kustaajabisha kakiuka taratibu zote hizo na kukurupuka kumweka ndani mtumishi huyo. Je, DAS(ambaye ni katibu tawala wake wa wilaya na mshauri mkuu wake) hakumshauri asifanye hivyo na kumfundisha taratibu au nae aheshimiwi na DC? Pia wiki moja kabla alitaka kumweka ndani Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo akatuma polisi wakamakamate ofisini kwake wakakuta hayupo. Mkurugenzi nae aliposikia hilo akawa na hasira sana na DC huyo na uadui ulioanza (kati ya DC na Mkurugenzi) kwa kubughudhi watumishi wa Halmashauri ukawa mkubwa. Je, kwa stahili hiyo kutakuwa na mahusiano mazuri kati ya watendaji wa Halmashauri na DC? Kweli maendeleo yatakuja kama kuna migogoro? Je, huo ndio utawala bora? Je, baraza la madiwani la Halmashauri hiyo litakubaliana na upuuzi huo? Kitakachotokea ni DC huyo kususiwa au kutopewa ushirikiano na Mkurugenzi na Baraza la Madiwani na pia maamuzi yake yote kupuuzwa au kutotekelezwa au kutekelezwa bila moyo na yeye na chama chake kudharauliwa na waliomteua kuonekana sio makini na ilani ya chama tawala kutotekelezwa ipasavyo na hivyo wananchi kukosa maendeleo na kuathirika na mwisho chama chake kukosa kura.

  DC huyo alipogundua amelikoroga na watumishi wa Halmashauri wamechukia na vyama vya wafanyakazi vimechukia kutokana na ubabe wake na uvunjaji wake wa taratibu, kanuni na sheria na udhalilishaji huo na kuhisi kushtakiwa mbali kwa Rais na mamlaka za juu akaitisha press conference na waandishi wa habari akawaambia eti alimtia ndani mhandisi huyo kutoakana na kuwa na viashiria vyote vya rushwa. Sasa sijui ni viashiria vipi wakati hata tenda haikutangazwa? Na kama kulikuwa na viashiria hivyo mbona hakuwaambia TAKUKURU wafanye uchunguzi? Amemhuhukumu mtumishi huyo na kumchafulia jina yeye na mkurugenzi bila kosa kuthibitika mahakamani. Je polisi ndio wanaochunguza masuala ya watumishi? Je hiyo siyo misuse ya resources? Je huko ndio kujenga mahusiano mazuri na Halmashauri? Je, huo ndio utawala bora au utawala wa kimabavu na kidikteta? Habari hiyo ilirushwa siku ya jumamosi tarehe 7 Julai 2012 ktk taarifa ya habari ya ITV na kumpatia ujiko DC huyo huku ikiwa imepotoshwa na akaongea kujitetea lakini bila kujua alivunja taratibu ktk kumweka ndani mhandisi huyo. Eti amewaagiza polisi kumhoji, hivi polisi ndo wanahoji watendaji wa halmashauri badala ya mkurugenzi? Alimuona Mkurugenzi hana uwezo huo au ndo kutokujua taratibu au ndo kuonyesha ubabe? Sikwizi kwa ugomvia alionao na mkurugenzi eti akitaka kupata ufafanuzi au kutoa agizo fulani linalohusu watendaji wa Halmashauri hiyo huwa anapiga simu direct kwa mhusika badala ya kuwasiliana kwanza na Mkurugenzi wa Halmashauri ambaye ndiye Accounting Officer wa Halmashauri na ayewajibika kwa lolote litakalotokea Halmashauri. Sasa mambo yakiharibika je Mkurugenzi ndiye atakayejibu au DC?

  Inasemekana DC huyo ili kuendeleza propaganda zake ametafuta kikundi cha waendesha boda boda wachache pale stendi ya Korogwe na kukihonga ili kiwe kinamtangaza, kinamtetea na kusema yeyote atakayemchukia DC huyo watakufa nae eti kwa sababu anatetea maslahi ya wananchi wa Korogwe. Sikatai maslahi kutetewa lakini yatetewe kwa kufuata utaratibu na si kudhalilisha watumishi wa umma.

  Kitu kinachomtia kiburi DC huyo inasemekana ni bangi anayokula na urafiki wake na Ridhiwani Kikwete. Na tangu Mh. Rais alipomsifia kuwa ameanza kusimamia usafi wa Korogwe ndipo kama alimchochea vile na kiburi na Udikteta ndio vikazidi na akajidhania yuko juu ya sheria.

  DC huyo ni mtaalamu wa IT ambaye hana uzoefu wa uongozi, umri ndo miaka ishirini na kitu, na taratibu, kanuni na sheria za Serikali hazijui ila kilichomfanya ateuliwe ni ule ushoga wake na Ridhiwani na inasemekana huko Arusha alikotoka alichangia sana kuporomoka ubunge wa Godbless Lema wa CHADEMA wakati akiwa kada wa CCM huko Arusha na hivyo kuzadiwa zawadi ya U-DC na washkaji zake.

  Inasemekana Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe amekwisha kulalamika kwa RAS na RC wa Tanga juu ya utendaji mbovu wa DC huyo unaokiuka taratibu lakini inavyoelekea hakuna hatua zozote zilizochukuliwa labda ni kwa ajili ya ushoga wake na akina JK, anaogopwa!

  Sijui kwa uvunjaji taratibu, kanuni na sheria huo nae atashitakiwa au atapelekwa kwanza kwenye mafunzo ya uongozi apate msasa wa kanuni, taratibu na sheria ndo aendelee au ataachwa na washkaji zake.
   
 2. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  If what is alleged in this post ( of which I can call a "plaint"), this is quite a fit case for malicious prosecution. It has all the chances of success, I can assure you!!!
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Nilishasema hapo awali kuwa kutakuwa na fujo sana wilayani baada hao ma DC wapya kuapishwa!!maana walipewa maneno ya unafiki kuwa eti wakasimamie wakurugenzi wa wilaya maana ni wezi na wabadhirifu!sasa najiuliza hakutakuwa na mgongano hapo!DC ana mamlaka yake na mkurugenzi yake tofauti kabisa!sifa wanazotaka kupata zitawafanya waishie kuaibika na kupelekwa mahakamani....labda wabadili vifungu vya uteuzi wao na uwajibikaji na report channels!la sivyo fujo tupu
   
 4. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  kwakweli kwa utendaji wa namna ile hatuendi hivyo sioni sababu ya kuwaweka ndani watumishi wa serikali!
   
 5. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,731
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Ndo tatizo la kuwateua watu wa vijiwe vya ccm kua wakuu wa wilaya,. Akili ndogo kuongoza akili kubwa
   
 6. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,135
  Likes Received: 2,158
  Trophy Points: 280
  Mkuu Imekuuma Sana... Hata wewe ingekutokea Mwanao Anarejea mapema kutoka Shuleni anasema kerejeshwa na mwalimu kuwa hajatoa Mchango wa Jengo na ukitaka kumlipia anasema mchango ni zaidi ya elfu hamsini lazima umkalishe chini na uende mwenyewe... Huo ukarabati lazima uwe unaeleweka sasa mtu akuambie chungwa moja linauzwa kariakoo sokoni elfu tano lazima utamuona ni Mwizi... Nadhani walikuwa wanamtest Mrisho waone kama ni Bogus au lah ili waendelee kula bata... Keshawastukia tia ndani hao Mrisho ila tizama Kwanza Sheria....

  Umetumwana Malya umchafue Mrisho!!! pole zako mwache mwenzako afanye kazi yake haitakusaidia Hiyo ya Lema inaingiaje hapo? wataka CDM Waone ili wamchukie? Urafiki wa riz1 au jk ni sawa na Magufuri ya Mbowe....k
   
 7. K

  Konya JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 920
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  si mara ya kwanza kwa huyo gambo kufanya haya,na kifupi ni kwamba ameingia kwa mbwembwe mno ili tu aonekane kama ni mchapa kazi kwa wakubwa zake pasi na kujua au kufuata utaratibu wa utendaji kati ya ofisi yake na ofisi ya halmashauri/w,sasa sijajua kama ni ugeni wa ofisi/madaraka kwa ngazi hiyo au ndo kutumwa kurudisha heshima ya chama kwa staili hii
   
 8. Mr. Mwalu

  Mr. Mwalu JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2012
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 809
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 60
  pole sana eng swai, tayarisha wanasheria! siasa lazima ziwe na nidhamu!
   
 9. T

  Twasila JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2012
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,913
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  Eng. Nenda mahakamani mshitaki dc na serikali. Hakika utashinda. Nimepata taarifa kuwa ni tabia yake kuweka watumishi kizuizini.
  Hawa wateule wa jk vipi?
   
 10. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 866
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  kama ni kweli hayo yametokea, kuna haja kufungua kesi mahakamani, kwa kuangalia vifungu vya kisheria ni wapi huyo mhandisi anatakiwa kuripoti na kuchukuliwa sheria.Hapa kunaonyesha ni mwingiano wa madaraka na matakwa ya sheria.nachela kusema madiwani kama kuna ukweli wanawajibika kuitisha baraza la madiwani na kupiga kura ya kutokuwa na imani naye ili asiendelee kuingia kwenye vikao wakati hana mamlaka kma hayo.Ni lazima hapa sheria ingaliwe.Lakini CDM wakati wanapitisha sheria ya wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa , walitahadhalisha hayo.Lakini wingi wa wabunge wa ccm walipitisha sheria hiyo bila kujali.nashangaa kuona ubabe huo leo unaendelea.Ni kwamba ni vyema tukawa tunatunga sheria kwa masilahi ya umma na si maslahi ya chama.
   
 11. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  hayo ni maelezo ya upande mmoja,ni ngumu kuyasemea!
   
 12. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #12
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Habari za upande mmoja
   
 13. Gwangambo

  Gwangambo JF-Expert Member

  #13
  Jul 8, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 3,655
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Please leteni CV ya huyo DC!
   
 14. p

  petrol JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 322
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  hili lingepelekwa kwenye eneo la udaku, hapa si mahali pake
   
 15. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Alishindwa Ubunge wa Afrika ya Mashariki wakampa Ukuu wa Wilaya; Ni Kujipendekeza kwake huko
   
 16. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #16
  Jul 8, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  huyu Dogo ni mpuuzi sana..yaani nimemzikia jana anavoongea pale hakuna DC ni matapishi matupu
   
 17. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #17
  Jul 8, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,454
  Likes Received: 2,503
  Trophy Points: 280
  Wakuu, Huyo DC ni yule Kada kilaza wa CCM from Arusha kwa jina la Mrisho Gambo
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. alberaps

  alberaps JF-Expert Member

  #18
  Jul 8, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,450
  Likes Received: 804
  Trophy Points: 280
  Mrishooo! Actualy jina lake ni mrisho mashaka!
   
 19. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #19
  Jul 8, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Jina lake ni Mrisho Gambo na Mashaka ni jina la baba yake na Gambo ni la UKOO.

  Gambo, taratibu kijana. Haya mambo ya karne ya 21 ni magumu sana kuvamia kama huyajui vizuri.

  Nenda taratibu na usisite kuwauliza wazoefu wa nini kinatakiwa kufanywa kwa mambo fulani fulani. Ikibidi tafuta mwanasheria uwe unam-consalt na ukiweza basi anza kozi za uongozi hata za kujisomea mwenyewe na kwenda kufanya mitihani.

  Dunia inabadilika na Tanzania inabadilika. Isijekuwa siku moja unabadilishiwa kibao na kuwekwa ndani kwa kutumia madaraka vibaya kama yule mama wa Ukraine aliyekuwa Prime Minister.
   
 20. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #20
  Jul 8, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  Sehemu kubwa ya m-dc sina uhakika kama walipata dozi ya kutosha pale dodoma ili waweze kujua wajibu wao, na nafasi ya ya halmashauri, na haswa uhusiano uliopo. serikali lazima ikubali kutumia pesa ya kutosha kwa kuwapeleka huko hombolo, na huko mzumbe wakapate dozi stahili.
   
Loading...