DC wa K'ndoni Ally Hapi, afanya ziara ya kushtukiza ujenzi wa barabara ya Ali Hassan Mwinyi

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,575


Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mhe. Ally Hapi akikagua matengenezo ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi



Mkuu wa wilaya Kinondoni Ally Salum Hapi wa kwanza kulia akipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa ujenzi wa barabara ya Ali Hassani Mwinyi Halipo tembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo



Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mhe. Ally Hapi akiwa na wafanyakazi wa MS ESTIM CONSTRUCTION CO.LTD



Mkuu wa wilaya Mhe.Ally Hapi akiongea na msimamizi wa ujenzi.



Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi kushoto akiwa na meneja wa Tanroad katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi
 
Mkuu emb tuelezee tafsiri ya neno "kushtukiza" Maana hili neno sasa ni kama linatukanwa na maccm
 
Hivi DC wa Kinondoni ni mhandisi au ndio kutafuta kicks za kijinga.
 
Hivi ni kwanini hawa viongozi hawapendi kuvaa vifaa vya usalama mahali pa kazi kama safety boot, reflector, helmet na eye glass? Nimeipenda hiyo picha akiwa na wafanyakazi wa ESTIM, Naona baada ya "ziara ya kushtukiza" wakaamua wakonge foto.
 
16aac279d49317ca456d22096f3609a8.jpg


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Salum Hapi leo ametembelea ujenzi unaoendelea wa upanuzi wa barabara ya Mwenge-Morocco kuona maendeleo yake. Barabara hiyo ambayo ilikua na kero kubwa ya foleni iliamriwa kupanuliwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli katika hatua yake ya kubana matumizi na kupeleka fedha katika shughuli za maendeleo.
Katika ziara yake hiyo Mh. Hapi alitembea umbali wa mita 500 kwa miguu kukagua pia usafi wa mazingira ya kando ya barabara ambapo alipofika katila kituo cha mafuta cha Total, aliagiza uongozi wa kituo kufanya usafi wa mazingira yaliyo mbele ya kituo chao.
Aidha Mh. Mkuu wa Wilaya pia alizungumza na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es salaam, Mkandarasi na wataalam wengine wa ujenzi na kujua maendeleo yao.
Meneja wa TANROADS na Mkandarasi walimueleza Mkuu wa wilaya kuwa tayari kazi imekamilika kwa asilimia 90 na kwa mbali wanatarajia kukabidhi mwezi June mwaka huu.
 
... waandishi wa habari kila ziara za kushtukiza wapo?
Kuna waliokuwa wanasema mwafrika hajafikia hatua ya kujitawa mwenyewe tukawatukana lakini kila nikiangalia hizi movie za kutengeneza za viongozi wetu ndio nimeamini! Mtu anayefanya kazi kwa bidii si rahisi hata kujua kama yupo ila utaona mambo yananyooka tu. Du sina cha kusema na hizi movie. Magufuli aliharibu sana kumsifia msanii kama Makonda eti ndio mfano wa kuingwa. Matokeo yake wengine wote wanaiga uongozi wa kisanii..
 
Back
Top Bottom