DC wa Kinondoni Ali Hapi ama unashiriki kwenye mkakati huu dhidi ya Magufuli au unawajua wahusika'

Status
Not open for further replies.

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,903
2,000
Wadau, amani iwe kwenu.

Kama mnavyojua ni kwamba Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utafanyika Julai 23 huku ukitanguliwa na vikao vya kiutendaji. Mkutano huu ni mahsusi kwa ajili ya kukabidhiana kijiti cha Uenyekiti baina ya Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Jakaya Kikwete na Rais Magufuli ambaye ndiye atakuwa Mwenyekiti wa chama chetu. Binafsi napenda kumpongeza Jakaya Kikwete kwa kukiongoza chama chetu kwa ufanisi mkubwa hadi kufanikiwa kushinda kwa kishindo nafasi za Urais, Ubunge, Udiwani na Serikali za Mitaa kwa kipindi chote akiwa Mwenyekiti. Naheshimu pia kauli yake kuwa hatajiongezea hata sekunde na kwamba atakabidhi chama kwa Rais Magufuli kama ilivyopangwa Julai 23.

Hata hivyo, tunapoelekea kwenye mkutano Mkuu, yapo mambo mengi yanaendelea chini kwa chini ambayo kwa hakika hayajengi taswira nzuri kwa chama chetu. Ipo mikakati ya siri na ya dhahiri ya kutaka kumhujumu Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM. Kibaya zaidi, mikakati hiyo inaratibiwa na kutekelezwa na watu wazito chamani pamoja na baadhi ya Wateule wa Rais Magufuli.

Siku ya Jumatano Julai 13, saa 8:23 Mchana, siku kumi tu kabla ya Mkutano Mkuu, nilianza kuwafichua baadhi ya wanaomhujumu Rais pale nilipoanzisha mada yenye kichwa cha habari "Kinara wa kukwamisha Rais Magufuli asiwe amwenyekiti wa CCM ni Rajab Luhwavi, NKM CCM Bara'. Baada ya uzi ule ambao kwa kweli ulipata wachangiaji na watazamaji wengi, yamepita masaa 53 kabla ya mtu anayejiita Egnecious kujitokeza na kumjibia Luhwavi.

Majibu hayo hakika yameibua mjadala mzito hasa juu ya mmiliki halisi wa ID hiyo. Mjadala huu naufananisha na mjadala wa mkulima maskini ambao uliibuka miaka kadhaa iliyopita wakati wa vuguvugu ndani ya CHADEMA ambapo ilikuja kubainika kuwa inamilikiwa na Samson Mwigamba. Kwa nini watu wanaendelea kuumbuka?

Imekuwa ni kawaida kwa makada wa vyama vyote kuwa na majina Bandia Jamiiforums. Ni majina hayo ndiyo tunayotumia kuweka taarifa zetu huku tukiamini tuko salama kutokana na sera ya Jamiiforums ya kuwalinda watoa habari ambayo kwa kweli imekuwa ni msaada mkubwa sana kwetu.

Hata hivyo, pamoja na kumiliki majina Bandia JF, tunafanya makosa makubwa ya kuweka majina yetu halisi kwenye mitandao mingine na hasa Facebook. Pia tunafanya makosa makubwa ya kuanzisha mada Jamiiforums na wakati huo huo tunakimbilia facebook kupost na kushare. Ndio udhaifu uliofanywa na mmiliki wa ID ya Egnecious . Kitendocha mada zinazowekwa Jamiiforums kufanana na zile zinazowekwa kwenye akaunti yake ya facebook tena kwa wakati ule ule hakika inatia shaka. Nitatoa mifano kadhaa kuthibitisha hili. Mada za hapa chini zimeandaliwa na Ali Hapi na kuwekwa Jamiiforums na Egnecious lakini Facebook ikawekwa na Ali Hapi. Kosa kubwa hili.
Udhaifu mwingine ni pale akaunti hii inapotumika kuweka mada nyingi za kumuelezea mtu mmoja tu. tangu Ali Hapi ateuliwe kuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, akaunti hii imeacha kuandika masuala mengine ya kisiasa na badala yake inafanya kazi ya kuanzisha mada za kueleza nini anafanya Mkuu huyo wa wilaya hapo Kinondoni. Hili ni kosa jingine na sijui atajinasuaje. Pitia nyuzi zilizoanzishwa na Egnecious utaona jinsi anavyotumia akaunti hiyo kujijenga.

DC Hapi atembelea hospitali, eneo la Uwanja wa fisi Tandale
DC Kinondoni amaliza tatizo la Madawati
EATV wamuomba radhi Mkuu wa Wilaya Kinondoni
DC Kinondoni ashiriki Ibada ya Ijuma msikiti wa Mtambani na kuongea na waislam
DC Hapi apokea sh million 19 za mchango wa madawati
Mkuu wa Wilaya Kinondoni afanya doria na Polisi saa 8 usiku
DC Hapi amtembelea rais wa awamu ya pili nyumbani kwake
DC Hapi aanza ziara kutembelea hospitali zote zilizopo wilaya ya Kinondoni
DC Hapi kunguruma Clouds Tv 360 Live kesho asubuhi
DC KINONDONI AGAWA VIFAA VYA WAGONJWA HOSPITALI YA OCEAN ROAD
DC Hapi atinga mahakamani kuhusu ukataji rufaa dhidi ya kampuni ya Q_CONSULT kuhusu Coco beach
DC Hapi apokea msaada wa madawati toka kwa NSSF Kinondoni

Kwa kweli mada ni nyingi na kwa jinsi gani utaona uhusiano mkubwa uliopo baina ya Egnecious na Ali Hapi.

Kwa vile tuhuma hizi ni nzito na ni za waziwazi, hakika ni wakati sasa wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi kujitokeza na kukana tuhuma hizi. Dhamana aliyopewa ni kubwa na anapaswa sasa kubadili mwelekeo wa aina ya siasa anazofanya. Sikutarajia kuona mtu aliyepigiwa debe na Kikwete apewe kazi na Rais akishiriki mkakati wa kumhujumu.
 

ugalila

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
652
1,000
Wewe ni jemedari aisee. Upo kitengo kijitonyama nini?? Kwa sasa naanza kuona kazi yako nzuri kwa mbali. Keep it up maovu ni yakuyafichua
 

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,903
2,000
hakuna ubishi hiyo account inamilikiwa na yeye mwenyewe.... acha wafu mzikane wenyewe sisi yetu macho na masikio
Kibaya zaidi anaitumia kumtetea mtu ambaye anamhujumu Rais. Bahati mbaya sana hamjui Lizaboni na hajui mantiki ya kuweka uzi ule. Yeye anajitokeza kichwa kichwa
 

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,183
2,000
Hii ni kwa maslahi mapana. Hakuna aliyetajwa moja kwa moja ila kilichooneshwa ni mahusiano. Huu mkakati ni mkubwa na mods wanapaswa kuwa wavumilivu
Ndugu Lizaboni unapaswa uvumilie, kutofautiana kwa mitazamo katika siasa ni kitu cha kawaida sana.Sasa na wewe unaanza kumchafua mwezio bila sababu humu! Kama huna uhakika na ID zake kaa kimya. Mbona wewe hutumii ID yako kama verified user? Wakiamua kukuanika na wewe itakuaje? Kama ni kweli yeye Alli nae anayo haki ya kuzungumza kama kawaida.
 

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
34,027
2,000
Sasa kumekuchaa...haya sasa kumekuchaa...jogoo limeshawika dodomaaa...!!

Kada wa CCM......!!

Magufuli apewe kura za ndioo!!
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
47,068
2,000
Sarakasi zimeanza vigogo wa jiji wanashambuliana hadharani sasa.Baada ya uteuzi wa kinondoni na kibamba nilitegemea haya kutokea na huu ni mwanzo tu kwa kisingizio cha Dodoma.Kwa utamaduni wa CCM Rais ni mwenyekiti wa chama tayari na hilo halina mjadala wala kutishiana NYAU.
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom