Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 875
- 960
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi, leo tarehe 3 Mei, 2016 ameendelea kutembelea hospitali Mbali mbali zilizoko Wilayani Kinondoni, ikiwa ni Siku ya Pili ya Ziara yake ya zaidi ya wiki moja.
Katika Ziara yake hiyo Mh. Mkuu wa Wilaya ameambatana na viongozi mbali mbali akiwemo Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni,
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinononi Muuguzi Mkuu wa Wilaya.
Mh Hapi ameanza Ziara yake majira ya Saa Tano asubuhi ambapo amezuru vituo vya afya vya
UNUNIO, KUNDUCHI, MBWENI - MPIJI,
Dispensari ya MBWENI,
Kituo cha afya cha MABWEPANDE,
Dispensari ya BUNJU na BOKO.
Katika ziara hiyo Mh. Mkuu wa Wilaya amekutana na kuzungumza na watumishi wa hospitali hizo, kutembelea vyumba vya kutolea huduma, kukagua vifaa tiba na mazingira yanayozunguka hospitali hizo na kujionea changamoto mbalimbali zinazokabili utoaji wa huduma za afya ambapo ametoa maelekezo mbalimbali ya kufanyiwa kazi kwa uongozi wa vituo hivyo na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Dr. Azizi Msuya.
Mh Hapi amehitimisha ziara yake Saa 12
jioni na kurejea Ofisini kuendelea na Majukumu mengine.