DC wa Kigamboni Hashim Mgandilwa, avifunga Viwanda vya Wachina

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,650
2,000
*DC MGANDILWA AFUNGA VIWANDA VYA WACHINA KIGAMBONI*

*_Ni kufuatia ukwepaji wa kodi za serikali..._*

Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe Hashim Mgandilwa, leo tarehe 20/7/2017 amefanya ziara ya kushtukiza katika kiwanda cha plastic cha Ruider Plastic Limited kinachomilikiwa na raia mwenye asili ya China.

DC Mgandilwa aliyeambatana na Mkurugenzi wa manispaa ya Kigamboni Ndg Steven Katemba, walikagua na kugundua mambo mbalimbali yakiwemo ya kiwanda hicho kuendesha shughuli zake pasipo kufuata taratibu za nchi kikamilifu na baadhi ya mianya ya ukwepaji wa kodi.

Baada ya kutembelea eneo la kiwanda ili kujionea shughuli za uzalishaji, Msafara huo ulioongozwa na DC Mgandilwa ulibaini kuwa katika eneo hilo kuna viwanda tofauti Saba vinavyozalisha bidhaa tofauti tofauti.

Viwanda vilivyobainika ni pamoja na kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji ya plastic, kiwanda cha kutengeneza mikeka, kiwanda cha kutengeneza bodi za dari (Ceiling board), kiwanda cha kutengeneza mifuko ya plastic, kiwanda cha kutengeneza maboksi ya plastic kwa ajili ya kutunza vitu vya baridi, kiwanda cha kuyeyusha chupa za plastic, na kiwanda cha kutengeneza mito ya kulalia.

Viwanda vyote hivyo Saba vinafanya shughuli za uzalishaji katika eneo moja na huku kiwanda kinacholipa kodi za serikali kikiwa ni kimoja tu nacho kikisuasua kulipa kama inavyostahili.

Baada ya kutembelea viwanda vyote hivyo, DC Mgandilwa amewataka wamiliki wa viwanda hivyo kusitisha uzalishaji wake mara moja leo hii.

DC Mgandilwa amesema kusimama kwa shughuli za uzalishaji unatoa mwanya kwa timu kutoka mamlaka ya mapato (TRA) na Manispaa ya Kigamboni ambao amewaagiza kuweka kambi katika viwanda hivyo kuanzia kesho ili kupitia nyaraka zote na kubaini kiasi cha mapato ambayo serikali imekuwa ikiyapoteza tangu waanze uzalishaji.

DC Mgandilwa ameagiza kuwa baada ya tathimini hiyo kukamilika pesa yote ambayo serikali imekuwa ikipoteza tangu kuanzishwa kwa viwanda hivyo ilipwe mara moja iwezekanavyo na ndipo uzalishaji uendelee kwa kufuata taratibu zote za serikali.

Inakadiriwa kuwa kiwanda kimoja kilitakiwa kulipa Shilingi Milioni 101kwa mwezi hivyo kuifanya serikali kupoteza mapato ya zaidi ya Shilingi Milioni 700 kwa mwezi kwa viwanda vyote.
 
Kps chad

JF-Expert Member
Jan 10, 2017
539
1,000
Hapo ni viwanda vitatu tuu.Kwa mujibu wa orodha ya bidhaa zinazotengenezwa hapo.siyo saba kama alivyobainisha..... Chochote kilichotajwa hapo cha plastic, kinawekwa kwenye jumba moja la vifaa vya plastic.... Pili, kuhusu mapato kadanganya kabisa.si kweli kwamba anauza kiasi hicho.... Hata asiye na akili anajua kuwa katuzuga!!!!! Kwann msiwe mnaweka hesabu zenu vzr kabla ya kuja kwenye vyombo vya habari? Msikurupuke kumfurahisha bwana mkubwa
 
Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
3,945
2,000
Bora aseeh awa jamaa wametesa sana wananchi wanawalipa hela kiduchu sana wafanyakazi uku wakiwashirutisha na kuwanyanyasa,..5000 per day haikua sahihi, wakimaliza waende na oilcom
5000 per day haikuwa sahihi?
Kwahiyo kazi ikisimama ndio hiyo per day itaongezeka?
Hivi kuna aliyelazimishwa kufanya hiyo kazi ?
 
Lumwagoz

JF-Expert Member
Dec 29, 2013
978
1,000
Kufunga Si sahihi Sana. Wangeacha uzalishaji uendelee wakati huo mahesabu ya ukwepaji kodi yakiandaliwa. Ukifunga kiwanda ghafla ivyo unaumiza maskini waliokuwa wanapewa hiyo elfu 5 kwa siku.
 
Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
3,976
2,000
*DC MGANDILWA AFUNGA VIWANDA VYA WACHINA KIGAMBONI*

*_Ni kufuatia ukwepaji wa kodi za serikali..._*

Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe Hashim Mgandilwa, leo tarehe 20/7/2017 amefanya ziara ya kushtukiza katika kiwanda cha plastic cha Ruider Plastic Limited kinachomilikiwa na raia mwenye asili ya China.

DC Mgandilwa aliyeambatana na Mkurugenzi wa manispaa ya Kigamboni Ndg Steven Katemba, walikagua na kugundua mambo mbalimbali yakiwemo ya kiwanda hicho kuendesha shughuli zake pasipo kufuata taratibu za nchi kikamilifu na baadhi ya mianya ya ukwepaji wa kodi.

Baada ya kutembelea eneo la kiwanda ili kujionea shughuli za uzalishaji, Msafara huo ulioongozwa na DC Mgandilwa ulibaini kuwa katika eneo hilo kuna viwanda tofauti Saba vinavyozalisha bidhaa tofauti tofauti.

Viwanda vilivyobainika ni pamoja na kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji ya plastic, kiwanda cha kutengeneza mikeka, kiwanda cha kutengeneza bodi za dari (Ceiling board), kiwanda cha kutengeneza mifuko ya plastic, kiwanda cha kutengeneza maboksi ya plastic kwa ajili ya kutunza vitu vya baridi, kiwanda cha kuyeyusha chupa za plastic, na kiwanda cha kutengeneza mito ya kulalia.

Viwanda vyote hivyo Saba vinafanya shughuli za uzalishaji katika eneo moja na huku kiwanda kinacholipa kodi za serikali kikiwa ni kimoja tu nacho kikisuasua kulipa kama inavyostahili.

Baada ya kutembelea viwanda vyote hivyo, DC Mgandilwa amewataka wamiliki wa viwanda hivyo kusitisha uzalishaji wake mara moja leo hii.

DC Mgandilwa amesema kusimama kwa shughuli za uzalishaji unatoa mwanya kwa timu kutoka mamlaka ya mapato (TRA) na Manispaa ya Kigamboni ambao amewaagiza kuweka kambi katika viwanda hivyo kuanzia kesho ili kupitia nyaraka zote na kubaini kiasi cha mapato ambayo serikali imekuwa ikiyapoteza tangu waanze uzalishaji.

DC Mgandilwa ameagiza kuwa baada ya tathimini hiyo kukamilika pesa yote ambayo serikali imekuwa ikipoteza tangu kuanzishwa kwa viwanda hivyo ilipwe mara moja iwezekanavyo na ndipo uzalishaji uendelee kwa kufuata taratibu zote za serikali.

Inakadiriwa kuwa kiwanda kimoja kilitakiwa kulipa Shilingi Milioni 101kwa mwezi hivyo kuifanya serikali kupoteza mapato ya zaidi ya Shilingi Milioni 700 kwa mwezi kwa viwanda vyote.
Suala siyo kufunga kiwanda kinachotakiwa ni mkuu wa wilaya awaelimishe hawa wawekezaji kwani makosa sio yao mfumo ndio uliwaruhusu kufanya kazi hivyo. Mheshimiwa Rais Magufuli anaomba wawekezaji halafu mkuu wa wilaya anafunga. Masuala ya viwanda yaachiwe Wizara husika.
 
wa hapahapa

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
6,359
2,000
hadi DC anaenda kufunga hicho kiwanda maafisa biashara, mafisa wa TRA wa wilaya walikuwa hawajaliona hilo la ukwepaji kodi.....
 
BIGstallion

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
6,391
2,000
5000 per day haikuwa sahihi?
Kwahiyo kazi ikisimama ndio hiyo per day itaongezeka?
Hivi kuna aliyelazimishwa kufanya hiyo kazi ?
Ivo unajua kiwanda kilipo au unapayuka tu usikike na wewe umeongea,..ilikua kama nauli iyo,..5000 MTU anafany kazi siku nzima bora ata 10000
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom