DC wa Kahama: Nitaifunga Hotel baada ya siku 7 isipolipa kodi inayodaiwa

Hivi punde

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Messages
1,778
Likes
4,273
Points
280
Hivi punde

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2017
1,778 4,273 280
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhil Nkurlu ametishia kuifunga Hoteli ya Kahama Gold ya mjini Kahama iwapo mmiliki wake hatalipa kodi ya mauzo ya Sh30 milioni ifikapo Novemba 9.

Uongozi wa hoteli hiyo pia umuagizwa kuwalipa fidia wateja, akiwemo Mwandishi wa habari wa Kituo cha Luninga cha ITV Mkoa wa Shinyanga, Frank Mshana aliyeibiwa kamera na kompyuta mpakato wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Elias Kwandikwa.

Nkurlu ametoa maagizo hayo leo Ijumaa baada ya kutembelea hoteli hiyo kutokana na uongozi kukaidi agizo la Mamlaka ya Mapato(TRA) la kulipa kiasi hicho kabla au ifikapo Julai 5.

“TRA walitoa siku 90 zilizomalizika Julai 5 kodi hii iwe imelipwa. Naona mlipuuza; sasa nawapa siku saba kuanzia leo mlipe, la sivyo nitaifunga huku hatua zingine za kisheria ikiwemo kuipiga mnada zikifuata,” ameagiza Nkurlu

Kabla ya kuuzwa na kubadilishwa jina kuwa Kahama Gold, hoteli hiyo ilikuwa ikiitwa Mongo Hotel.
Meneja wa TRA Mkoa wa Kodi wa Kahama, Jacob Mtemang’ombe amethibitisha hoteli hiyo kudaiwa Sh30 milioni inayotokana na kodi ya asilimia 10 ya mauzo yaliyofanyika zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

“Tayari tumekamilisha taratibu kadhaa za kiofisi ikiwemo kuwaandikia wahusika kuwakumbusha kulipa deni hilo; hatua zingine zitafuata kwa mujibu wa sheria,” amesema Mtemang’ombe

Akizungumzia suala hilo, meneja wa hoteli hiyo, Obedi Hussein amesema wanapitia nyaraka, kumbukumbu na sheria kubaini iwapo mmiliki mpya au wa zamani ndiye anastahili kulipa kodi ya mauzo.

“Ikibainika sisi wamiliki wapya ndiyo tunapaswa kulipa kodi hiyo, tutalipa mara moja,” ameahidi Hussein

Kuhusu wizi wa mali za wateja, meneja huyo amesema tayari uongozi umechukua hatua kadhaa kudhibiti hali hiyo anayodaiwa waliikuta waliponunua hoteli hiyo.
 
mr gentleman

mr gentleman

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Messages
2,677
Likes
2,887
Points
280
Age
34
mr gentleman

mr gentleman

JF-Expert Member
Joined Aug 1, 2012
2,677 2,887 280
Nchi inanyooka kwa kweli.
 
kidole007

kidole007

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2012
Messages
3,082
Likes
901
Points
280
kidole007

kidole007

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2012
3,082 901 280
Habari ya julai leo ya nini
 
makinikia 101

makinikia 101

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Messages
493
Likes
864
Points
180
makinikia 101

makinikia 101

JF-Expert Member
Joined Sep 2, 2017
493 864 180
Hizo ndo habari tunazotaka kusikia mheshimiwa DC. Uteuzi mwngne utapiga uRC. Saiv tafuta wananchi waliopigia kura upinzani na uwakere kwasana.
Thank me later
 
Consigliere

Consigliere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
9,026
Likes
10,702
Points
280
Consigliere

Consigliere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
9,026 10,702 280
Hiyo ni kazi ya DC? Baada ya serikali hii kuondoka madarakani kuna watu wengi sana watatajirika kupitia fidia kwa ajili ya haya matamko na mihemuko inayoonyeshwa na kutolewa na watu wasio na mamlaka.
Anayejiita ana uchungu na nchi ndiye anaipeleka nchi kwenye mahasara makubwa kuwahi kutokea katika historia ya bara hili
 
B

Babati

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2014
Messages
31,790
Likes
25,151
Points
280
Age
33
B

Babati

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2014
31,790 25,151 280
Hizo ndo habari tunazotaka kusikia mheshimiwa DC. Uteuzi mwngne utapiga uRC. Saiv tafuta wananchi waliopigia kura upinzani na uwakere kwasana.
Thank me later
Akamate wapinzani ndiyo sifa no moja kwa utawala wetu.
 
Root

Root

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Messages
28,043
Likes
14,869
Points
280
Root

Root

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2012
28,043 14,869 280
ukiona kodi zinatafutwa kwa nguvu hivi jua hali ni mbaya sana
 
Muyobhyo

Muyobhyo

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2014
Messages
7,931
Likes
5,770
Points
280
Muyobhyo

Muyobhyo

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2014
7,931 5,770 280
Hizo ndo habari tunazotaka kusikia mheshimiwa DC. Uteuzi mwngne utapiga uRC. Saiv tafuta wananchi waliopigia kura upinzani na uwakere kwasana.
Thank me later
awakere kivipi, awatandike risasi au niaje mkuu, umeanza vizuri ila mwisho umekoroga
 
makinikia 101

makinikia 101

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Messages
493
Likes
864
Points
180
makinikia 101

makinikia 101

JF-Expert Member
Joined Sep 2, 2017
493 864 180
awakere kivipi, awatandike risasi au niaje mkuu, umeanza vizuri ila mwisho umekoroga
Yani sehemu yenye diwani wa ukawa au mbunge wa upinzani ahakikishe tunaanzisha miradi mipya ya barabara na nyumba ziende chini mara moja
 
kiumbe kipya

kiumbe kipya

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2016
Messages
2,586
Likes
1,126
Points
280
Age
38
kiumbe kipya

kiumbe kipya

JF-Expert Member
Joined Sep 30, 2016
2,586 1,126 280
Hiyo ni kazi ya DC? Baada ya serikali hii kuondoka madarakani kuna watu wengi sana watatajirika kupitia fidia kwa ajili ya haya matamko na mihemuko inayoonyeshwa na kutolewa na watu wasio na mamlaka.
Anayejiita ana uchungu na nchi ndiye anaipeleka nchi kwenye mahasara makubwa kuwahi kutokea katika historia ya bara hili
Kazi ya DC ni nini kwa mfano? Kujaa kimya nalo ni jibu,u DC wa awamu hii sio wa kipindi cha viongozi waliopita hapa kazi tu
 
Washawasha

Washawasha

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Messages
9,651
Likes
1,161
Points
280
Washawasha

Washawasha

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2006
9,651 1,161 280
Walipe kodi kwa faida ya Taifa
Nalog off
 
Consigliere

Consigliere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
9,026
Likes
10,702
Points
280
Consigliere

Consigliere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
9,026 10,702 280
Kazi ya DC ni nini kwa mfano? Kujaa kimya nalo ni jibu,u DC wa awamu hii sio wa kipindi cha viongozi waliopita hapa kazi tu
MAJUKUMU YA MKUU WA WILAYA

(i) Kumweka mtu kizuizini kwa muda wa saa 48 mfululizo iwapo atashukiwa kuwa ni mhalifu au anayehatarisha hali ya utulivu na Amani (Sheria ya tawala za mikoa Na 19/1997)

(ii) Kufungisha ndoa za serikali (Law of Marriage Act No 5/1971)

(iii) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuwa mwenyekiti wa Kamati yaMkoa inayochambua maombi ya watu wanaotaka kuuza madawa ya sumu (Pharmaceuticals and Poisons Act No 9/1978)

(iv) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuongoza Kamati ya kusikiliza rufani za leseni za biashara mkoani (Business Licensing Authority Act No 25/1972, ib. 1)

(v) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa ya leseni za vileo (Intoxicating Liquours Act No 28/1968)

(vi) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuteua wakaguzi wa magereza (Prisons Act No 34/1967, ib. 100)

(vii) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuwashughulikia watu wanaodhaniwa kuwa ni wachawi (Witchcraft Ordinance Cap 18)

(viii) Kuwa mhimili msaidizi wa Halmashauri za Wilaya (Sheria Na 7/1982).

(ix) Kuwa mwenyekiti wa Kamati mbalimbali zitakazoundwa Wilayani.

(x) Kuhudhuria vikao vya Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kamamjumbe

(xi) Kushughulikia malalamiko ya wananchi na kuyapatia ufumbuzi

(xii) Kumsaidia Mkuu wa Mkoa katika kuzisimamia Halmashauri za Wilaya na kuhakikisha kuwa zinatoa huduma nzuri kwa wananchi na kwa ufanisi

(xiii) Kuziwekea Halmashauri za Wilaya mazingira mazuri na kuhakikisha kuwa zinatekeleza majukumu yake kulingana na sera za serikali.

(xiv) Kutekeleza majukumu yote atakayopewa kisheria au kukasimiwa na Mkuu waMkoa.
 
IPILIMO

IPILIMO

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
1,858
Likes
592
Points
280
IPILIMO

IPILIMO

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
1,858 592 280
Sasa, ukifunga hotel sababu ya kodi iliyopita ni kosa utakosa kodi ijayo pia watu watapoteza kazi..kaeni na mmiliki kwa hatua yenye akili zaidi
 
kiumbe kipya

kiumbe kipya

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2016
Messages
2,586
Likes
1,126
Points
280
Age
38
kiumbe kipya

kiumbe kipya

JF-Expert Member
Joined Sep 30, 2016
2,586 1,126 280
MAJUKUMU YA MKUU WA WILAYA

(i) Kumweka mtu kizuizini kwa muda wa saa 48 mfululizo iwapo atashukiwa kuwa ni mhalifu au anayehatarisha hali ya utulivu na Amani (Sheria ya tawala za mikoa Na 19/1997)

(ii) Kufungisha ndoa za serikali (Law of Marriage Act No 5/1971)

(iii) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuwa mwenyekiti wa Kamati yaMkoa inayochambua maombi ya watu wanaotaka kuuza madawa ya sumu (Pharmaceuticals and Poisons Act No 9/1978)

(iv) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuongoza Kamati ya kusikiliza rufani za leseni za biashara mkoani (Business Licensing Authority Act No 25/1972, ib. 1)

(v) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa ya leseni za vileo (Intoxicating Liquours Act No 28/1968)

(vi) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuteua wakaguzi wa magereza (Prisons Act No 34/1967, ib. 100)

(vii) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuwashughulikia watu wanaodhaniwa kuwa ni wachawi (Witchcraft Ordinance Cap 18)

(viii) Kuwa mhimili msaidizi wa Halmashauri za Wilaya (Sheria Na 7/1982).

(ix) Kuwa mwenyekiti wa Kamati mbalimbali zitakazoundwa Wilayani.

(x) Kuhudhuria vikao vya Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kamamjumbe

(xi) Kushughulikia malalamiko ya wananchi na kuyapatia ufumbuzi

(xii) Kumsaidia Mkuu wa Mkoa katika kuzisimamia Halmashauri za Wilaya na kuhakikisha kuwa zinatoa huduma nzuri kwa wananchi na kwa ufanisi

(xiii) Kuziwekea Halmashauri za Wilaya mazingira mazuri na kuhakikisha kuwa zinatekeleza majukumu yake kulingana na sera za serikali.

(xiv) Kutekeleza majukumu yote atakayopewa kisheria au kukasimiwa na Mkuu waMkoa.
Izo sheria ni za miaka ya 60-70,apo nimekumbuka kulikuwa na sheria ya matunzo ya mtoto ilikuwa inasema kwa mwezi baba atoe sh 100 kama matunzo halali ya mtoto je 100 inatosha kwa maisha ya sasa huo natoa kama (mfano tu) ndo maana nasema viongozi wanaoteuliwa sasa na awamu hii ya hapa kazi tu lazima wajiongeze,hakuna sehemu DC atashtakiwa kwa sababu kambana mfnanyabiashara aliyekuwa anakwepa kodi halali ya serikal na kabla hawajaanza kazi wanakuwaga na semina piana kwenye hizo semina lazima poa wasisitiziwe hayo.na huko tuendako itabidi kiundwe chombo maalum cha kufuatilia kodi,kiwe tofauti na wakusanya mapato TRA.,taratibu tutaelewana tu kwa sbb mda bado tunao.
 
Mzalendo2015

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2012
Messages
2,810
Likes
3,433
Points
280
Mzalendo2015

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2012
2,810 3,433 280
Kazi ya DC ni nini kwa mfano? Kujaa kimya nalo ni jibu,u DC wa awamu hii sio wa kipindi cha viongozi waliopita hapa kazi tu
Acha ujinga pse....!!
Kama DC anakusanya kodi TRA wanafanya kazi gani? Rais mstaafu Kikwete hakuwa mjinga kuwapa Semina elekezi viongozi walokuwa chini yake!!
Kama DC anafikiriia kufunga hoteli atakuwa ni kibuyu wazi asiyejua ABC za uchumi hata kidogo.........!!!
Huwezi kufunga hotel yenye thamani ya mabilioni kwa deni lla 30mil Tsh huo ni uwendawazimu....
 
Ukiwa kwenye ile idadi ya 12,000 bado utakuwa una mawazo hayo, DC hawezi shtakiwa popote kwa kujiongeza na kutafuta mapato ya serikali ndo kwanza Mh anawapandisha cheo kuwa ma RC we kaa apo ukiniambia unyumbu wako,endeleeni na tafrija ya kulipokea DUME

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Forum statistics

Threads 1,214,997
Members 462,952
Posts 28,531,402