DC wa Iringa, Richard Kasesela ameomba radhi kwa picha zinazomuonyesha akiwa ameshikilia viungo bandia vya uume

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
ec21d23a5f0403f3dbc49d0522a1a815.jpg

IRINGA: Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela, amewaomba radhi Watanzania kufuatia kusambaa kwa picha zinazomuonyesha akiwa ameshikilia viungo bandia vya jinsia ya kiume na kuzua taharuki katika jamii, ndani ya nchi na nchi za jirani.

Akitoa ufafanuzi kwa Vyombo ya habari mapema leo Aprili 23, amesema alikuwa katika ufunguzi wa utafiti katika Chuo kikuu cha Mkwawa uliofanyika Aprili 9 akiwa miongoni mwa washiriki.

"Kabla ya ufunguzi, banda la uelimishaji rika lilikuwa ni miongoni mwa mabanda kadhaa yayotembelewa na washiriki, ambalo lilikuwa linatoa Elimu Rika kwa wananchi juu ya maambukizi ya VVU na kujikinga ukizingatia mkoa wetu ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa maambukizi ya VVU hapa nchini.

"Licha ya picha kupigwa wakati nikipokea Elimu kutoka kwa mwelimisha rika, ninakanusha maelezo yaliyoandaliwa na Dauson Kumbusho ambae ni Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na pia msaidizi wa Mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa," amesema.

DC Kasesela ameongeza: "Andiko lake lilielezea kufungua kiwanda cha kutengeneza viungo bandia vya jinsia ya kiume, nilimpigia simu na akaniomba radhi yakaisha, hivyo basi ninakuja kwenu Watanzania kuomba msamaha na kueleza kuwa maneno yaliyoandikwa hayakuwa na ukweli bali ni uzushi, naomba tuyapuuze."
IMG_20190423_182131.jpg
 
Hii picha kila anaeiona bila maelezo yoyote ni lazima atawaza anayoyaona hapo
Kwa hiyo hata ajitetee kwa kuapa pia hakuna kitu
Meme yake sasa
Daa inatakiwa ukiwa katika jamii uwe na hekma sana na kuwa na tahadhari kubwa kila wakati
Mwingine yule wa kumkashifu Mungu yaani watu wakubwa wamekuwa kichekesho kwa watoto siku hizi
 
Back
Top Bottom