DC wa Hai (Novatus Makunga) chanzo cha migogoro hai

PIPOO

Senior Member
Dec 19, 2012
141
13
Katika kile kinachoonekana ni udhaifu wa watendaji wa wateule wa Mh. Rais Jakaya Kikwete Mh Novatus Makunga dc wa Hai amelalamikiwa na wananchi wa kwa kushindwa kutatua migogoro ya vijiji na kata mbalimbali na kuwa chanzo na mlezi wa migogoro ya uongozi ktk maeneo tofauti tofauti ambayo nitayafafanua hapa chini.

MGOGORO KIJIJI CHA ISUKI –KATA YA MASAMA KATI: Mnamo tar 24-12-2012 mh DC akiambatana na DED (mkurugenzi) hai walifika kijj cha isuki kuja kusikiliza kero za wananchi dhidi ya m/kiti wao wa kijiji ya kutofanya mikutano ya kisheria tangu achaguliwe 2009.Kwenye mkutano huo wananchi walimkataa m/kiti huyo ila DC akamlinda kwa kutumia polisi.

-Aliahidi kutuma timu ya ukaguzi badala yake wale wananchi waliokuwa mstari wa mbele kudai TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZ YA KIJIJI WALIFUATWA NA POLISI NA KUTENGENEZEWA KESI YA KUFANYA VURUGU na kesi ipo mahakamani kwa maelekezo ya DC-NOVATUSI MAKUNGA.

-Amekuwa akiingilia utendaji wa halmashauri na kujifanya ni sehemu ya baraza la madiwani. Mfano mnamo tar 21/5/2013 madiwani walihoji azimio la utatuzi mgogoro wa mas/kat na kujulishwa kuwa DC ameunda tume ya kushughulikia suala hilo jambo ambalo liliwakasirisha madiwani na kuhoji DC ni nan kwenye baraza la madiwani? Madiwani walikataa majibu hayo na kumwagiza mkurugenz kushughulikia na kumuonya DC asiingilie maamuzi ya baraza la madiwani.

-Amekuwa akitoa maelekezo kwa mkurugenzi kutoshughulikia malalamiko yanayoletwa na wananchi juu ya utendaji mbovu wa watendaji wa vijiji na kata.

-Amekuwa akitumia magari ya halmashauri kwa shughuli zake za kikazi na binafsi na baadaye kudai posho huku akujuwa hana fungu la DC kwenye halmashauri wakati yeye ni mtumishi wa serikali kuu.

NI CHANZO NA MLEZI WA MGOGORO WA SHAMBA LA NKWANSIRA. Amewatapeli wananchi (vyama vya ushirika) waliokuwa na mgogoro na uongozi wa bodi ya shamba ambayo imeshindwa kuwasomea wananchi mapato na matumizi ya shamba chini ya usimamizi wao. Aliahidi kufikisha suala lao kwa waziri wa chakula na ushirika ili kulipatia ufumbuzi badala yake amesimamia ubinafsishaji wa shamba hilo kwa mwekezaji mwingine kupitia bodi ile iliyokataliwa na bila vyama vya ushirika/wananchi kujulishwa.

KUINGILIA KESI ZILIZOKO MAHAKAMANI
Kesi ya ndg LEVIS LEWIS Vs KADCO uwanja wa ndege KIA ambapo kauli yake ya tar 21/5/2013 ktk mtandao wa fb alimwagiza ndg Levis kuondoka kwenye nyumba za kadco huku akijua Levis ni mpangaji halali jambo ambalo tar 30/5/2013 mahakama ya kitengo cha ardhi moshi ilifuata uamuzi wa Mh. Makunga.

Amekuwa akiwapa kiburi wenyeviti wa na watendaji wa wa vijiji na kata wanaaovurunda katika utumishi wao kwa kuingiza siasa katika utendaji. Mfano tar 03/2/2013 alikaa kikao na wenyeviti wanne wa vijiji vya kata ya masama kati na kuwashauri kuandika barua kwa waziri mkuu kumlalamikia diwani wa kata hiyo (CHADEMA) ushauri ulitekelezwa tar 5/2/2013.
 
Mwenyewe yuko jamvini na uhakika ameyasoma subiri muda kidogo utapata majibu ya unachokitafuta
 
PIPOO

Naomba nitangulie kwa kukuomba uwe mkweli si vyema na siyo vizuri kuzusha mambo yasiyokuwepo.Mimi nipo katika mtandao na nimekuwa wazi kujibu hoja mbalimbali ni vyema ungeanza kuniuliza baadhi ya masuala ambayo labda unayafahamu juu juu sana.Kuhusu hoja zako ulizoa ebu nianze kukujibu moja baada ya nyingine.

ISUKI:
Tangu nifike nimefanya mikutano zaidi ya mitatu na huo mkutano unaozungumzia nilimwomba DED ambaye kimsingi ndiye mwenye mamlaka ya kusimamia uendeshaji wa kijiji twende huko Isuki.Kwa taarifa yako kwa DED ilikuwa siku ya kwanza kufika hapo, Tulisikiliza kero na yeye alijitahidi kwenda kwenye kanuni kwani kuna baadhi walikuwa wanataka mwenyekiti aondoke lakini kwa kuumia ukurasa mmoja tu wa sheria badala ya kutumia kitabu kizima ambacho kinafafanua taratibu za kumwondoa mwenyekiti wa kijiji, Tatizo kubwa ukikosea na kumwondoa mwenyekiti bila kufuata utaratibu,akikata rufaa anarudi madarakani na aibu itakuja kwetu sote.

Lakini la pili DED aliahidi kutuma ukaguzi maalumu hiyo kauli alitamka yeye,mimi jukumu langu lilikuwa kumleta na kumtaka ashughulikie huo mgogoro.
Mimi sina maslahi yoyote na mwenyekiti wa kijiji cha Isuki bali sitapenda kuona kijiji kile kinavurugika bila sababu na baadhi ya vijana walitoa tuhuma za kutofanyika mikutano na ubadhilifu hoja ambazo mwenyekiti Yule alijitahidi kuzijibu kila alipopata nafasi.

Mkutano ule uliendelea lakini mwishowe tulikubaliana na wananchi wenyewe walitaja tarehe ya kikao kingine ambacho taarifa ya mapato na matumizi itasomwa.Katika hiyo tarehe nilipewa taarifa wananchi hawakukubali taarifa hiyo na kuagiza iandaliwe tena
Suala la Isuki lipo kisiasa sana na toka kikao cha mwisho nilimpa kazi ya kulimaliza DED kwa kuwa wengine mnatuchulia kama makada wa chama tawala,hivyo kupata kujenga imani ninaamini DED ana nafasi kubwa zaidi.

Ingawa mimi nilipanga kuwafikisha mpaka mnapotaka pa kutoa maamuzi,hayo nimeshafanya katika baadhi ya vijiji. LAKINI naendelea kurudia tena na hili nimeshaandika sana,Issue ya Isuki,uongozi wa kata na kijiji una nafasi kubwa sana wa kumaliza kuliko hata ngazi ya wilaya.

KUTENGENEZA KESI
: Katika maisha yangu kamwe sitakuja kufanya kitu hicho,Labda inawezekana ufahamu au unafahamu lakini unafanya kusudi.Isuki kuna mgogoro wa ofisi ambayo inadaiwa ya CCM huku kundi linguine likidai ni ya Kijjiji.Kiichotokea watuhumiwa walikwenda kufunga kwa nguvu ile ofisi hivyo viongozi wa CCM walienda kufungua kesi polisi na polisi walichofanya ni kuwakamata watuhumiwa na kuwafikisha mahakamani. Katika mikutano ya Isuki nilishauri kama wanadai ofisi ni ya kijiji mbna njia rahisi ni kupitia vyombo vya sheria ambapo itakuwa rahisi kutoa uamuzi wa kisheria kuliko kutumia nguvu ambazo mara nyingine inachukuliwa kama uvunjifu wa amani.

KUINGILIA UTENDAJI WA HALMASHAURI,Ndugu yangu nafahamu sheria na taratibu za halmashauri na baraza la madiwani katika eneo hilo usitegemee kunipata hata siku moja nikifanya kosa,Tume unayodai kuiunda mimi sijaunda na nitafanya jitihada za kukutag barua ya uundaji wa tume ambao ulifanywa na Mkurugenzi yaani DED kwa ajili ya kushughulikia mgogoro wa Masama Kati na kuomba mtu mmoja kutoka ofisini kwangu,Mimi niliona jambo jema kwani hatuwezi kuendelea kuwa na mgogoro uliodumu karibu miaka miwili.

KUTOSHUGHULIKIA UTENDAJI MBOVU WA WATENDAJI WA VIJIJI,mimi nitakuwa mtu wa ajabu sana endapo nitalea utendaji mbovu wa watendaji wa vijiji,tangu nije hapa kazi kubwa nanayofanya ni utendaji mbovu wa watendaji wa vijiji hilo unaweza kupata ushahidi kutoka kwa mwenyekiti wa chadema wilaya uhusiana na mtendaji wa kijiji chake na hatua ambazo niliweza kuchukuwa.

Suala la kudai posho,hilo siyo la kweli kwani zijawahi hata siku moja katika halmashauri ya wilaya kama una ushahidi leta na kama ulivyozungumza hapo juu katika halmashauri hakuna fungu la DC.
Shamba la Nkwansira,Shamba hilo lilikuwa na mgogoro na mwekezaji na baadaye ukamalizika na wenye shamba walitafuta mwekezaji mpya hata kabla ya mimi kuja.

Lakini kikubwa siwezi kuwa chanzo cha mgogoro kama ufahamu vizuri masuala ya ushirika ni ya wana ushirika wenyewe na taratibu,kanuni na sheria zipo,mimi nazifahamu vizuri sana hivyo maamuzi yanatokana na kuamua wenyewe wenye ushirika,namshukuru mungu sijawahi kutoa agizo lolote huko wala kuhudhuria mikutano yao.
Nashukuru umenifahamisha kwamba kuna mgogoro nashukuru sana hivyo ni suala la kufuatilia

KESI YA LEWIS :Lewis ni rafiki yangu lakini sihifahamu kama ana kesi na KADCO bali Lewis aliwahi kuja ofisini kwangu na alieleza suala lake la nyumba kuwa KADCO wanamwondoa kwa nguvu na siku hiyo alifuatana na mchungaji mmoja wa KIA.Mimi nilimshauri kuwa zile nyumba ni za mamlaka ya viwanja vya ndege zipo kwa ajili ya wafanyakazi wao na hivyo endapo hayupo tena kazini ni vigumu kuruhusiwa kuendelea kuishi,tulibishana lakini Yule Baba mchungaji alimwelewesha.

WENYEVITI KUANDIKA BARUA KWA WAZIRI MKUU .Siyo kweli kuhusiana na wenyeviti wa vijiji vya kata ya masama kati kwamba nimekaa nao na kuwaambia waandike barua kwa waziri mkuu.Labda kwa nia yako ya kuandika uongo ama kwa kutokujua ama kwa kufanya makusudi,wenyeviti wana mgogoro na diwani wa kata ya masama kati na ni mgogoro ambao nimeukuta.

Mwenyekiti wa halmashauri mzee Clement Kwayu kwa nafasi yake kusuluhisha na hata mkurugenzi yaani DED na katika kikao cha mwisho cha baraza la madiwani niliongea kuhusu mgogoro huo na kuelezea matarajio yangu ya kwamba utafika kikomo na binafsi nimekuwa namshauri mheshimiwa diwani kumaliza hilo tatizo kama mwenyekiti wa WDC na hata viongozi wa madhehebu ya dini wa kata hiyo nimekuwa nikiwaomba kama viongozi wa kiroho.

Labda hujui kwa sisi tuliopo katika nafasi hizi,kiutendaji nisingeweza kuwashauri waandike barua kwa waziri mkuu kwa kufanya hivyo inamaana uongozi wa wilaya umeshindwa kazi.
Lakini kwa msisitizo na kwa taarifa yako tangu nifike Hai ndani ya mwaka mmoja nimefanyakazi kwa mafaniko makubwa,nimeboresha masuala mengi,nimetatua migogoro mingi sana na nashukuru kazi hii naifahamu vizuri na nashukuru vitu vingi sana navijua na kwa upande wa vichache ambavyo sivifahamu sisiti kukuuliza kwani kuuliza si ujinga.

Miongoni mwa ya kujivunia ni kumaliza mgogoro wa waslamu na wakristo kuhusiana na nani achinje,kumaliza mgogoro wa wenyeviti wa vitongoji na vijiji na halmashauri ambapo huko nyuma ilikuwa ni chui na mbuzi,kumaliza migogoro ya wafugaji na wakulima na kumaliza mgogoro wa Modio Islamic,Roo na wawekezaji na mingine mingi Suala la utawala bora pia katika kuhakikisha fedha za umma zinatumika vizuri sana na baadhi ya wabadhilifu wana kesi TAKUKURU na polisi na kizuri nimewajengea imani kubwa waheshimiwa madiwani bila kujali itikadi za vyama vyao.

Nachokuthibitisha mgogoro wa Isuki utakwisha na katika kata ya Masama kati katika muda mfupi ujao lakini pia ndani ya chama cha msingi cha Nkwansira kama kuna tatizo nalo litafika mwisho.


KWA KUMALIZIA NASHUKURU NAPATA USHIRIKIANO MZURI SANA KUTOKA KWA MADIWANI,MHESHIMIWA MBUNGE NA WATENDAJI WA HALMASHAURI NA KAZI KWA UJUMLA ZINAKWENDA VIZURI,CHANGAMOTO CHACHE ZIPO NA TUNAENDELEA KUZISHUGHULIKI
 
Sikubaliani na uwepo wa ma DC ila Makunga hana tabia za itikadi yake,sio fisadi wala hana tamaa ya mali.hapa unamuonea Novatus
 
DC, RC ni ulaji baada ya kulamba viatu vya wakubwa. Nova Makunga jiandae hatutaki vyeo vya kipuuzi kwenye Tanganyika mpya
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom