Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,893
- 940
DC VICTORIA MWANZIVA - MIAKA MIWILI YA RAIS MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN NDANI YA WILAYA YA LUDEWA
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Victoria Mwanziva amesema; kwa hakika Miaka Miwili imekuwa ya Neema na Baraka tele kwa Wana-Ludewa, kwani Rais Samia amekuwa akiitazama Wilaya kwa jicho la upekee sana. Wananchi wa Ludewa wameshuhudia Miradi mikubwa na ya fedha nyingi ikija ndani ya Wilaya.
1. Ludewa imepata Shilingi Bilioni 2.6 kwaajili ya ufunguzi wa barabara za Mwambao.
2. Ludewa imepata Shilingi 2.8 Bilioni kwaajili ya ujenzi wa Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Milioni 500 za ujenzi wa Ikulu, na Milioni 150 za ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi (DED )
3. Ludewa imepata Shilingi 5.4 Bilioni kwaajili ya ujenzi wa Chuo cha VETA Shaurimoyo.
4. Ludewa imepata Shilingi 179 Bilioni kwaajili ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha zege Lusitu - Mawengi.
5. Ludewa imepata Shilingi 5.4 Bilioni kwaajili ya ujenzi wa barabra eneo la Mlima Kimelembe ambao ulikuwa chanzo cha ajali nyingi.
6. Ludewa imepata Milioni 900 kwaajili ya ukarabati wa Hospitali ya Wilaya, Milioni 250 kwaajili ya ujenzi wa jengo la ICU Hospitali ya Wilaya, Milioni 500 kukamilisha kituo cha Afya Mundindi, na ujenzi wa zahanati 16 ambapo nne zimeshakamilika na zinatoa huduma (Mholo, Nsisi, Mdilidili na Lifua), huku 12 zikiendelea na ujenzi (Mkiu, Kimelembe, Ndowa, Chimbo, Liunji, Lihagule na Mbongo, Sagalu, Ludewa kijijini, Kimata, Nsele na Mbugani).
7. Ludewa imepata fedha za miradi ya Maji, Kata ya Mawengi wamepewa Bilioni 2, Mavala Bilioni 1, Mavanga Bilioni 1.5, Luvuyo Bilioni 1.5, Madope Milioni 508, Lifua na Manda Milioni 600 na kata ya Ludewa Bilioni 7.
8. Ludewa imepata minara ya simu mipya 7 ambayo inatoa huduma na mwaka huu tunarajaia kuanza ujenzi wa minara mingine sita.
9. Ludewa imepata Ujenzi wa daraja mto Ruhuhu, ambalo limeokoa wananchi wengi wa Kata ya Ruhuhu kuliwa na Mamba
10. Ludewa imepata Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Lubonde ambayo kiasi cha Sh. 470 Milioni kutoka Serikali kuu na Milioni 55.5 kutoka mapato ya ndani yametumika na imeanza kutoa huduma, ujenzi wa maabara mpya 12, ujenzi wa vyumba 41 vya madarasa S/M na Vyumba 81 S/Sekondari
11. Ludewa imepata zaidi ya Bilioni 10.3 kwaajili ya ujenzi wa barabra vijijini kupitia TARURA.
#LudewaYetu