DC Venance Barama amfukuza kazi mtumishi kama mbwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DC Venance Barama amfukuza kazi mtumishi kama mbwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mugishagwe, Sep 9, 2009.

 1. M

  Mugishagwe JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 295
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Katika hali ya kushangaza mkuu wa Mgambo wa Ilala wakiwa katika mkutano pale mnazi mmoja muda mfupi uliopita amemfokea na kumfuza nje Mkuu wa Mgambo wa Ilala kwa madai kwamba mkuu huyo alikataa kuitika wito wa mkuano kwa maneno akitaka maandiko ya kuonyesha kuna mkutano na DC na Mkurugenzi wa Jiji. DC alikuwa nalia lia uchafu wa Jiji na baada ya hapo alitoa nje kwa maneno na utemi Askari mwanajeshi Mstaafu ambaye anajulikana kwa jina la Chuma, kwa madai ya kuomba barua ya kuhudhuria mkutano.

  Ameagiza Mkurugenzi kumfuza kazi mara moja na asionekane kokote ofisi za Jiji. Hii ni ile style ya Lowasa naona jamaa anayo pia. Wajuvi, huyu DC akil yake ina akili? Hivi ndiyo mtumishi wa serikali anavyo fukuzwa kazi?

  Msaada wenu kuelewa hili kama limekaa kisawa sawa.
   
 2. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2009
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hivi hujui jamaa nae ni njagu pia???

  Sasa na huyo mgambo alikuwa anataka nini? Barua ati? Kazi yao kuonea machinga na akina mamantilie eti?
   
 3. Kipunguni

  Kipunguni Senior Member

  #3
  Sep 9, 2009
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu, hakuna cha kushangaza hapo .... huyo ndiyo Venance Barama ... ni mmoja kati ya watu makini sana; huwa hataki longolongo!
   
 4. M

  Mugishagwe JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 295
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Umakini ndiyo huu? Kumfukuza pale mkutanoni na kusema Mkurugenzi naamuru afukuzwe kazi huyu na toka hapa nenda huko nje ?
   
 5. Kipunguni

  Kipunguni Senior Member

  #5
  Sep 9, 2009
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naweza ku-speculate kwamba hilo kosa siyo la kwanza, na inawezekana alishamuonya huko nyuma ...... hivyo leo akaona amfukuze kazi! .... Barama hana mambo ya kuoneana aibu au haya ... ukiharibu unaondoka!
   
 6. M

  Mugishagwe JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 295
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Habari kutoka ndani ya Jiji zinasema huyu mkuu wa Mgambo hajawahi kuwa na kosa na ni mwanajeshi mstaafu . Kosa lake ambalo jamaa yenu kaona ni kosa ni Mkuu wa mgambo kuomba barua ya kuitwa mkutanoni mnazi mmoja .Yeye amehoji kuitwa kwa taarifa ya maneno bila ya maandishi .Je bado Barama anataka kusema kwa jambo hili anaweza kusema ondoka kuanzia sasa kazi huna na toka humu ndani ?
   
 7. S

  Simoni Member

  #7
  Sep 9, 2009
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 67
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa mazingira ya Ilala na kiburi ambacho nina hakika anakumbana nacho huyo DC hata kutoka kwa madiwani wa Ilala na hasa Meya Abuu Jumaa sishangai. Hata ningekuwa mimi ningefanya hivyo hivyo. Pale Ilala kama ingekuwa amri yangu ile Halmashauri ningeifutilia mbali na badala yake ningeunda Tume. Otherwise kudos to Afande Balama. Sawasawa Mkuu endelea hivyo hivyo hawana maana hao. Kazi kutafuta rushwa tu. Kama mnabisha waulizeni hata wakandarasi wanaojenga madarasa au zahanati au barabara. Cheki hupati mpaka umtangulizie chochote mstahiki Meya. Yeye ndiye mtia saini wa mwisho. Ukileta noma cheki hasaini. Hiyo ndiyo habari yenyewe. Sijui TAKUKURU wako wapi. Bila shaka wanafuatilia kashfa za EPA
   
 8. K

  Kadudu Member

  #8
  Sep 9, 2009
  Joined: Mar 22, 2008
  Messages: 71
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  suala si aibu bali taratibu lazima zifuatwe,au kwasababu yeye ni mgambo.huo sio uadilifu tunaoutaka kama anamakosa siku alitakiwe amtimue kwa taratibu zinazotakiwa
   
 9. M

  Mugishagwe JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 295
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  This was the point I wanted to raise here . Sikuleta kwa ajili ya kumjua mtu bali the rule of law na haki za mkuu wa mgambo ni zipi ?
   
 10. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,317
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Haishangazi huyo Barama kutoa amri hiyo. Itashangaza kama huyo mkurugenzi aliyeamriwa kumfukuza mtumishi huyo atatii hiyo amri!
   
 11. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #11
  Sep 10, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  aliongea kisiasa zaidi, sasa mkurugenzi akimfukuza jamaa aende mahakamani tu, labor laws ziko wazi, akoma nao tu kama wanadhani kila kiltu ni siasa za ccm, wanasahau nchi hii in sheria.
   
 12. U

  Umushoshoro Senior Member

  #12
  Sep 10, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 121
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Mgambo ni mwanajeshi,na kwa kanuni Mkuu wa wilaya ndio msimamizi wa jeshi la mgambo wote wilayani.

  Ni rahisi kufukuzwa kazi kwa kutotii amri ya afande.

  Je kama kulikua na vita,angetaka barua?

  Kuna kazi ambazo mtu anahitaji barua kuitwa kikaoni,hata mgambo?
   
Loading...