DC Sabaya ataka wabunifu Chuo cha Ufundi Arusha wasikwamishwe

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya amezitaka mamlaka zinazothibisha ugunduzi unaofanywa na wabunifu mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa chuo cha ufundi Arusha kuhakikisha hawakwamishi kazi hizo badala yake wazithibitishe ili ziweze kwenda kutatua changamoto zilizopo katika jamii.

Sabaya aliyasema hayo wakati akizindua umoja wa wanafunzi waliosoma katika chuo cha ufundi Arusha( ATC)wenye lengo la kuendeleza ugunduzi walioufanya pamoja na kusaidia wanafunzi waliopo kujifunza juu ya teknolojia za kisasa na baadae kusaidia jamii.

Alisema kuwa kumekuwa na urasimu unaokwamisha kuendeleza ubunifu mbalimbali unaofanywa kutokana kila mamlaka kuwa na taratibu na sheria zake jambo linalofanya vifaa vilivyogunduliwa kuwa kwaajili ya mitihani na sio kwaajili ya kusaidia na kuondoa changamoto zilizopo katika jamii.

"Waafrika wanafanya maajabu ya kugundua vitu vinavyosaidia jamii lakini mamlaka husika zinawakwamisha kwani ni vita iliyopo kati ya mamlaka inayoamua vyuo vikuu na vyuo vya nadharia na vitendo ambayo haisemwi vitu ambavyo vipo kwenye wizara na taasisi moja,"alisema Mkuu wa wilaya huyo.

Sabaya alisema ni vyema Nacte na TCU wakakaa pamoja na kuunda bodi moja itakayosaidia vijana wabunifu kufanikisha ugunduzi wao na sio kila mmoja kuwa na vigezo vyake kwani jambo hilo linawarudisha nyuma na kuwakatisha tamaa na kufanya jamii kuendelea kuamini teknolojia za njee.

Kwa upande Mkurugenzi wa elimu ya ufundi kutoka wizara ya elimu, Dr.Noel Mbonde alisema ni vyema wanafunzi wanapohitimu chuo wakaendeleze kwa vitendo kile alichokipata kutoka chuoni hapo ili kuonyesha umuhimu wa uwepo wao lakini ukiondoka kama ulivyofika atakuwa amepoteza muda na kutokuwa na msaada wowote katika jamii.

IMG_20210115_133512_922.jpg
IMG_20210115_123129_680.jpg
 
Hamna kitu hapo.

Afrika haijawa tayari kutumia wagunduzi, wataalamu wake na muda bado haujafika.

NOTE:
Kuna binti mmoja wa chuo cha ufundi Dar Es Salaam DIT ambaye amebuni mfumo wa kutoa taarifa kwa daktari au nesi ambaye yupo (labda) ofisini kuwa wodi, kitanda flani mgonjwa kazidiwa na mfumo huo unatunza data endapo daktari au nesi atachelewa kwenda au hakwenda kabisa kutoa huduma na mgonjwa kadhurika au kufariki dunia.

Sasa tafakari mfumo huo ulivyo mzuri kwa kiasi hicho ni serikali gani ya kiafrika itakayokubali kuutumia ambao (mimi nasema ni mfumo wa kuumbua udhaifu) utachuja pumba na ngano za watendaji?
 
Nani ataifanya africa iwe na utayari wa kutumia wataalamu wake??
JamiiForums1379143281.jpg
 
Nani ataifanya africa iwe na utayari wa kutumia wataalamu wake??
Ndiyo maana mwanzo kabisa nikasema "Afrika haijawa tayari kutumia wagunduzi, wataalamu wake na muda bado haujafika."

Maelezo ya pale chini kwenye comment yangu yanatosha kupata jibu la swali lako.
 
Back
Top Bottom