jd41
JF-Expert Member
- Aug 23, 2015
- 3,756
- 4,842
Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ameagiza wamiliki wawili wa mabasi kufika kituo cha polisi Boma n'gombe leo kabla ya saa 12 jioni, kwa tuhuma za kuandaa genge la watu wanaohujumu miundombinu ya reli.
Watuhumiwa hao ni Clemence Mbowe anayemiliki mabasi ya Machame Safari, na Rodrick Uronu anayemiliki mabasi ya Lim Safari.
Mbowe alipoulizwa na Mwananchi kuhusu tuhuma hizo alisema si za kweli na kwamba DC anataka tu kuwachafua, amesema kama wana tuhuma angewaita ofisini maana yeye ni kiongozi hivyo haoni sababu kwa nini aongee kwenye mkutano wa hadhara, atatafuta haki yake mahakamani.
Sent using Jamii Forums mobile app