Dc rungwe ondoa fikra mgando kuhusu mgogoro wa maji mjini tukuyu,chukua hatua

Mwamakula

JF-Expert Member
Nov 7, 2010
1,890
382
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, Jackison Msome ameingia katika mgogoro na wananchi wa kata saba za mjini Tukuyu wanaopinga ongezeko la maji kwa kiwango cha asilimia 125 kulikofanywa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tukuyu.

DC huyo anadai kuwa wananchi wanaolalamikia tatizo hilo eti ni wahuni tu,kana kwamba wanachokilalamikia hakina maana. Hivi wananchi anao waita MSOME kwamba ni wahuni inawezekana kweli wahuni wakafungua kesi mahakamani kupinga ongezeko hilo la maji?.

Msome kumbuka JK bado hajafanya uteuzi wa ma-DC usipokuwa makini huu mgogoro utakushusha CV zako, nakushauri chukua hatua kushughulikia tatizo hili, tumia busara katika kusghughulikia mgogoro na siyo ubabe kama unavyofanya. Uongozi wa kibabe ulishapitwa na wakati hii ni karne nyingine.
 
Yaani huyo DC ndivyo alivyowatamkia wananchi huko kuwa ni wahuni??
Subiri....!!!!hiyo kauli lazima imghalimu.
 
wateule wa kikwete ni wajeuri sana na hawana utu, mwingine alitukana wananchi kule Arusha!
 
Back
Top Bottom