DC Ole Sabaya: Jabali amelala Hayati Dkt. Magufuli

ANAANDIKA DC SABAYA LENGAI
_
Baada ya Kushuhudia Mwili wa Dr John P.Magufuli ukiwa Akiwa Amelala Sasa Nimeamini Jabali Lenye Moyo wa Simba Na Akili ya Duma Amelala Usingizi wa Mauti.

Usiku ule wa Tarehe 17 March ni usiku Mgumu kuwahi kutokea katika Maisha Yangu, Nilimfikiria Baba, Mwalimu,mtu mwenye Huruma,ambaye kabla ya "kukuhukumu" atataka akusikilize na wewe, Na siku zote akisema USIOGOPE,Mtu asiyejua UNAFIKI wa kupikwa ila aliyezingatia zaidi matokeo ya kazi Aliyokupa, na aliyeamini sana katika nafasi ya pili,Anayesikiliza sana tena kwa Upendo.

Kuondoka kwake kwa wakati huu kuliniingiza Ganzi Nisiyowahi kuiona Maishani, Ninajua Mama Janeth amempoteza Mume, Taifa Limempoteza Baba na Rais, Africa Imempoteza Mwana mapinduzi Jasiri,Lakini Mbingu Imempokea shujaa Wa Imani, Aliyevipiga vita bila Kujali maumivu ya Moyo aliyoyapitia, akailinda imani kwa Kulitambulisha Jina la MUNGU aponyaye kwa mataifa, Na sasa amemaliza mwendo na Amepumzika Miguuni kwa bwana Wa vita. MATENDO uliyoyatenda kwa Gharama ya maisha yako, yamekutangulia.

Nenda Baba Nenda, matendo yako, kazi zako,na kujitoa kwako kumeandikwa kwa wino wa dhahabu kwenye moyo wangu na katika mioyo ya watanzania wa kweli umeandika Dibaji mpya. Hadithi za kazi ulizowatendea wana wa Taifa hili zitasimuliwa na vizazi, kwangu umenipa sababu ya kuamka tena, kutenda kwa Ujasiri bila woga wala Hofu,Nikiona Fahari sana Kwamba nimejifunza na Kuwa Mwanafunzi wako na uwe na Uhakika kwamba sasa Nitatenda kwa ujasiri zaidi bila kutokuonea wala kupendelea na niikijua ipo siku MUNGU mwenyewe, katika ukamilifu wake, atatuita kutoa hesabu ya matendo yetu na Sio Maneno yetu.

Tukutane baadae Nyumbani kwa baba, kusiko na Kuomboleza, kilio wala maumivu,Tutakapohesabiwa haki na Bwana's Mwenyewe.

Imenyamaza sauti dhabiti ya wanyonge, imenyamaza kimya kiranja mkuu na mkufunzi wapigania usawa kwa vitendo, Amelala Mjamaa Asiyetishika,Ardhi imemeza shujaa na kaka wa Taifa,Bwana Ataitia Nguvu Mioyo iliyosinyaa, wala Hataacha Taifa Lililolitetea Jina Lake liaibike kamwe.

Umetufunza ushupavu na misimamo imara,Nyayo na Kumbukumbu zako vitatupa hasira za kufanya kwa ajili ya Taifa .
Ndugu yangu ukweli umeondokewa na kupungukiwa ulikanyaga Sheria upendavyo hakuna wa kukukemea ulidhalilisha watu ukaonekana shujaa,ulidhulumu watu na kufanya ujambazi wa mchana Ila waliotakiwa kukuwajibisha wakakulinda na kusema ni mtakatifu yote ujue hatujasaha km ubongo wako ulivyomsahaulifu Ila ss siku zako zinahesabibika suntashangaa siku nikija kukuona gereza la karanga hapo

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Ndugu yangu ukweli umeondokewa na kupungukiwa ulikanyaga Sheria upendavyo hakuna wa kukukemea ulidhalilisha watu ukaonekana shujaa,ulidhulumu watu na kufanya ujambazi wa mchana Ila waliotakiwa kukuwajibisha wakakulinda na kusema ni mtakatifu yote ujue hatujasaha km ubongo wako ulivyomsahaulifu Ila ss siku zako zinahesabibika suntashangaa siku nikija kukuona gereza la karanga hapo

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
SABAYA anayo kazi aisee
 
Wakuu mbona huyu sabaya ni moja kati ya viongozi niliona walikua wakiitendea haki nafasi zao....! Ila naona humu wengi mnamponda sana, inawezekana ana makando kando mengi nisiyoyafahamu
 
Sabaya ni moja ya viongozi ninaowatabiria makubwa kwa nchi hii.
Yes yes ata sisi tuliowengi tunamtabiria makubwa sana yatakayo enda sambamba na maofu yake..

Lazima alipe mpaka doti ya mwisho Mungu alali!
 
Back
Top Bottom