DC Nyamagana, Meya wa jiji la Mwanza waingia kwenye "Vita"

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
DC Nyamagana, Meya wa jiji la Mwanza waingia kwenye "Vita"

DC asema meya Bwire anatuhumiwa na wananchi wa kata yake kwa kushindwa kufanya mikutano

MKUU wa Wilaya ya Nyamagana, Dk. Philis Nyimbi amesema amechukizwa na kitendo cha kudharauliwa na Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire na kushindwa kufika kwenye mkutano wake uliofanyika mtaa wa Igelegele Kata ya Mahina kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Meya Bwire ambaye ni Diwani wa Kata ya Mahina (CCM) ndiye alikuwa mwenyeji wa mkutano huo ambapo alishindwa kutokea wala kutoa udhulu au kutuma mwakilishi wake kitendo ambacho kilisababisha kikao kukosa mtu wa kufungua ambapo DC Nyimbi alilazimika kujifungulia mkutano na kufunga.

Akizungumza katika mkutano huo, Dk. Nyimbi alisema kitendo cha Meya Bwire kushindwa kufika katika mkutano huo ambao wote walipanga na kupeana ratiba ni dhararu kubwa kwake na ikizingatia wananachi waliomchangua wanamlalamikia kwa kushindwa kufanya mikutano ya kutatua kero zao.

“Hii ni dharau ya hali ya juu dhidi yangu, haiwezekani mimi kama mkuu wa wilaya nafika ndani ya kata ya diwani husika kasha yeye hayupo wakati tulipanga wote ratiba na anajua leo nipo eneo lake, kama alikuwa na shida binafsi ni heri angenijulisha mimi au kutuma mwakilishi wake, pia najua hapa kuna diwani viti maalum naye hayupo, hii ni dharau.

“Kwa kuwa viongozi wa CCM wapo hapa na mtendaji wa kata hii naomba mfikishie salamu zangu kwamba amenidharua sana, isiwe kificho fikisheni salamu zangu kwamba nimechukizwa na ameonyesha dharau ya hali ya juu, hapa wananchi wanamlalamikia hafanyi mikutano ya kutatua kero zao isitoshe wapo wanaomlalamikia moja kwa moja, inawezekana ndiyo maana amekwepa.

“Hapa Mahina ndiyo aneo pekee ambalo wananchi zaidi ya 700 wanalalamika juu ya ardhi yao kuchukuliwa kati ya mwaka 2000/2010 na wa watu wenye fedha zao, sasa kama viongozi wa awamu ya tano tunataka wapate haki zao lakini tunakwamishwa na watu na namna hii, hali hii naomba isijirudie, tumepewa dhamana ni lazime tuwajibike kuwahudumia wananchi.

“Haingii akilini leo mimi kama mkuu wa wilaya nipo hapa, mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiburwa Kibamba yupo hapa, wakuu wote wa idara za jiji wapo,kamati ya ulinzi na usalama ipo na wengine lakini Meya wa Jiji anadharau na kuendelea na shughuli zake tena bila kutoa taarifa, sikupendezwa hata kidogo,”alisema.

Hata hivyo wakati Dk. Nyimbi akilalamika Meya Bwire kukosekana eneo hilo, alikuwa katika Uwanja wa Mpira wa Nyamagana akishuhudia mechi kati ya KMC na Alliance ambaye ndiye Mkurugenzi na mmiliki timu hiyo yenye maskani yake Kata ya Mahina.

Alipotafutwa kwa njia ya simu ,Meya Bwire ili kueleza sababu ya kutofika eneo la mkutano lakini simu yake iliita bila kupokelewa.
Baadhi ya wananchi waliotoa kero zao walilalamikia kukosa umeme baadhi ya maeneo, maji, ubovu wa barabara, kudhulumiwa viwanja na watu wenye fedha, kuchelewa kupewa fidia ya maeneo yao yaliyochukuliwa na Serikali.

Akijibu malalamiko ya ardhi na fidia, Mkurugenzi wa jiji hilo, Kibamba alisema wananchi wa Mahina wana haki ya kulalamika kwa sababu hawakutendewa haki miaka ya 2000 kutokana na uongozi uliokuwapo kuwanyang’anya ardhi yao bila fidia.

Alisema mpaka sasa kuna wananchi 3000 ndani ya Jiji la Mwanza wanadai kupewa viwanja mbadala ambapo Serikali inaendelea kutafuta eneo lingine na kulipima na kuwagawia.

Aliongeza kuwa wapo ambao wanaendelea kulipwa fidia ingawa uthamini uliofanyika kipindi hicho haukuwa wa haki ambapo alitoa mfano kuna mtu anatakiwa kulipwa Sh 60,000 hadi milioni moja wakati maeneo yao yalichukuliwa na kupimwa huku yakiuzwa kwa bei kubwa kwa watu wenye fedha.
 
Watajuana wenyewe...wakiweza wapigane kabisa sisi hayatuhusu....wakigombana ndo wanakimbilia huruma zetu.wakiwa kwenye high table huko sisi hatukumbukwi
 
Hivi huyu Dr. Phillis Nyimbi ni nidyo yule alizaa na Nabii Mwingira? Kesi ikanguruma mahakamani ikaamuriwa Mwingira akafanye DNA? Ha ha ha sijui ile kesi iliishia wapi? Kua na kuzeeka uyaone.
 
Hivi huyu Dr. Phillis Nyimbi ni nidyo yule alizaa na Nabii Mwingira? Kesi ikanguruma mahakamani ikaamuriwa Mwingira akafanye DNA? Ha ha ha sijui ile kesi iliishia wapi? Kua na kuzeeka uyaone.
Mkuu samahani hivi wewe ni ME au KE!!?
 
Mkuu samahani hivi wewe ni ME au KE!!?
Ha ha ha vipi Mkuu mbona umetaka kufahamu jinsia yangu? Mimi ni mwanaJF kama wewe Mkuu na hapa tunaongelea kwenye keyboard tu na mbaya Zaidi pamoja na ukongwe wangu JF huu ni mwaka wa 12 sijawahi hata kuhudhuria zile get together za miaka ile. Aise JF kulikuwa na burudani Enzi hizo si kama sasa imegeuka kabisa MKUU. Kwani wewe ni HE and SHE? Tuanzie hapo MKUU.
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom