DC Namtumbo, Moses Machali ajihami kwa bastola baada ya kunusurika kukatwa mapanga akihamasisha wauza madafu kuchukua vitambulisho

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Wakati Mkuu wa Wilaya Nanyumbu, Moses Machali, akidai kunusurika kukatwa panga akihamasisha wajasiriamali kuchukua vitambulisho, Polisi mkoani Mtwara imesema aliwatishia bastola wauza madafu baada ya kutofautiana kauli.

Hata hivyo, Mwananchi halikufanikiwa kupata maelezo ya upande wa pili wa kijana huyo anayetuhumiwa.

Katika mitandao ya kijamii leo Jumatatu Aprili 29, 2019 kuna taarifa inayosambaa ikieleza namna Machali alivyonusurika katika tukio hilo baada ya kufika kijiji cha Mikangaula wilayani humo.

Machali alithibitisha taarifa hiyo inayoeleza baada ya kufika kijijini hapo, alisimama kununua madafu huku akikagua wenye vitambulisho na kuhamasisha wasio navyo kulipia lakini mmoja wa wauza madafu alianza kukashifu Serikali akisema inawaibia wananchi.
“Ni kweli ilitokea, nilienda kutoa taarifa jana Kituo cha Polisi cha Mangaka wilayani hapa, kwa hiyo siwezi kuzungumzia kwa kina liko chini ya uchunguzi,” amesema Machali.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Blasius Chatanda, amesema taarifa alizopata kutoka eneo la tukio hilo ni kwamba baada ya kutofautiana kauli na kijana huyo, Machali alitoa bastola kumtishia.

“Niko safari Morogoro. Hata hivyo, taarifa za awali nilizozipata ni kwamba yeye (DC) alimtolea bastola muuza madafu baada ya kupishana lugha, sasa mazingira ya kutoa hiyo bastola sijui lakini mpigie msaidizi wangu ofisini atakupa taarifa za kina, ”amesema Chatanda.

Akisimulia sakata hilo, Machali amesema katika hali ya kustaajabisha muuza madafu huyo mkazi wa Msufini alianza kutoa maneno ya kashifa Serikali.
 
Moses Machali moja ya ushahidi wa teuzi za rushwa wanazolazimisha wapinzani kutoka CDM,Machali alikuwa CDM,Katambi alikuwa CDM,Mwita alikuwa CDM,Msando alikuwa CCM,Dr. Slaa na bado wengine kibao wakaula,Julius Mtatiro wa CUF bado anasugua makalio
 
Hawa vijana waliotoka Chadema shombo sana...... Sasa DC mzima unamtolea bastola muuza madafu?!!

Heri DC Kasesela aliyetaka kuzichapa kavu kavu na Mchungaji Msigwa pale Nduli kuliko hawa wahamiaji.
Huyo Machali alishawahi kuchapwa bakora na vijana wa area C pale Dodoma akiwa mbunge...... Kichapo alichochezea ilibidi alazwe hospitali ya mkoa!
 
Patamu sana, na Kumuweka ndani huyo muuza madafu bila sababu ya msingi hawezi. Itakula kwake huyu DC
 
Mkuu lawama za nn..? Si ameenda mwenyewe.. si yuko ccm sasa.? Ya nn kumita chadema hahahaha.
Ndio kusema mkuu alikosea kumteua
Hawa vijana waliotoka Chadema shombo sana...... Sasa DC mzima unamtolea bastola muuza madafu?!!

Heri DC Kasesela aliyetaka kuzichapa kavu kavu na Mchungaji Msigwa pale Nduli kuliko hawa wahamiaji.
Huyo Machali alishawahi kuchapwa bakora na vijana wa area C pale Dodoma akiwa mbunge...... Kichapo alichochezea ilibidi alazwe hospitali ya mkoa!
 
Hawa vijana waliotoka Chadema shombo sana...... Sasa DC mzima unamtolea bastola muuza madafu?!!
Heri DC Kasesela aliyetaka kuzichapa kavu kavu na Mchungaji Msigwa pale Nduli kuliko hawa wahamiaji.
Huyo Machali alishawahi kuchapwa bakora na vijana wa area C pale Dodoma akiwa mbunge...... Kichapo alichochezea ilibidi alazwe hospitali ya mkoa!
Nani kawaambia Moses machali katoka chadema? Au ndio ushabiki uchwara uo? Pia swala la vijambulisho wafanyabiashara wadogo wanaogoma kuvichukua nadhani wanatatizo kwenye akili zao. Hivi ni nchi gani mtapewa fursa ya kufanyabiashara mwaka mzima kwa ada ya elf 20 alafu mkatae kuchangamkia fursa hiyo? Dah watanzania sijui tumerogwa? Ingekua mimi Rais ningevichukua vitambulisho vyangu na mgambo na almashauri za miji waendelee kufanya yao pumbavu sana.
 
Akili yako imezidi fuvu la kichwa
Muuza madafu ni mfanyabiashara!
Anaingiza sh ngapi kwa mwaka?
 
Acha afunzwe kazi
Anadhani yupo Kigoma kule wanakopiga wazee wao.
Huko ni shughuli atiiii
 
Kauli ya RPC ambaye hayupo mkoani kwake kuthibitisha wazi kwamba DC ana makosa inatoa maswali mengi kuliko majibu, yawezekana huyu DC hakubaliki na viongozi wenzake au system imemchoka au uwezo wake wa kutetea chama upo chini au malipo aliyopewa yanaelekea mwisho anapaswa kurejesha madaraka kwa wenyewe.

Waliotoka upinzani wengi wanaonekana wamekwenda kuchukua nafasi za watu hivyo ukiaribu Kama alivyoaribu DC lazima wakushindilie nyundo ikiwezekana wakupeleke kwa court

RC Kilimanjaro anaonja joto ya jiwe kwa wakuu wa wilaya aliopewa katika mkoa wake, hawamheshimu kwa sababu wanaamini ile nafasi si yake Ni ya mwana CCM.

Hii ni fundisho kwa wale wote waliokabidhiwa madaraka kujifunza kuwatambua maadui na marafiki zako
 
Back
Top Bottom