DC Mwenda awahakikishia Wanairamba kutafuta suluhu ya migogoro ya mipaka

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,781
898
MHE MWENDA AWAHAKIKISHIA WANA-IRAMBA KUTAFUTA SULUHU YA MIGOGORO YA MIPAKA.


Mkuu wa wilaya ya Iramba Mkoani Singida Mhe Suleiman Yusuph Mwenda amewahakikishia wananchi wa kata ya Ntwike kuwa Serikali wilayani humo inaendelea kutafuta Suluhu ya mgogoro wa mpaka kati ya wilaya za kishapu, Igunga na Meatu. Mhe Mwenda ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kusikiliza kero za wananchi wa kata ya Ntwike na kuwataka wananchi wote wa wilaya ya Iramba kuendelea kuwa watulivu wakati suala hilo likitafutiwa muafaka juu ya Mgogoro huo ambao umechukua muda mrefu bila ya kupatiwa ufumbuzi.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Ntwike Mhe Albert Makwala amemuomba Mkuu wa wilaya ya Iramba Mhe Suleiman Yusuph Mwenda kuendelea kulifuatilia kwa ukaribu mgogoro wa mpaka kati ya vijiji vya wilaya za kishapu, Meatu na Igunga kwani mgogoro huu umekuwa wa muda mrefu na baadhi ya watangulizi walilitafutia ufumbuzi ingawa halikufika mwisho alisema Mhe Makwala.

Akitoa kero kwa Mkuu wa wilaya ya Iramba Mhe Mwenda Mwenyekiti wa wafugaji ambaye ni mkazi wa kata hiyo kwenye kijiji cha Nsunsu Mzee Ntegi Dogani amemweleza Mhe Mwenda wafugaji wa kata ya Ntwike wanapata kero kwani kikao cha ujirani mwema walichokaa mwaka jana walikubaliana eneo hilo la malisho lililopo kwenye vitongoji vya Wagamoyo na Sangasa ambalo lipo wilaya ya iramba wafugaji waendelee kulitumia wa maeneo yote yenye mgogoro mpaka wataalamu kutoka Wizara ya Tamisemi watakapokuja kutatua kero hiyo ingawa baadhi ya wafugaji kutoka Kishapu wamekuwa wakiuza malisho kwenye eneo hilo na kusababisha wafugaji wa Iramba kukosa eneo la malisho na hali inayopelekea uvunjifu wa amani.

Aidha Mhe Mwenda amewaomba wakazi wa wilaya ya Iramba hususani wananchi wanaokaa vitongoji vya Sangasa na Nsusu kuendelea kuwa wavumilivu kwani Serikali ya wilaya ya Iramba imeanza kuchukua hatua tarehe na tarehe 7.8 kamati ya Ulinzi na Usalama walikutana na viongozi wa wilaya ya Kishapu kwa ajili ya kufanya mazungumzo na wamekubaliana kwa pamoja waitishe kikao kitakachojumuisha viongozi wa mkoa, vijiji na kata husika pamoja na wataalamu kutoka Wizara ya TAMISEMI ili kero hiyo iweze kutatuliwa. Alisema Mhe Mwenda.

Mkuu wa wilaya amehitimisha ziara yake ya kutatua na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi kwa kuwaahidi kero zote alizofikishiwa na wananchi kila sehemu ataendelea kuzifanyia kazi na anawashukuru Sana wananchi kwa ushirikiano wanaoipatia Serikali ya awamu ya 6 chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan.

#IrambaKaziInaendelea

IMG-20210824-WA0066.jpg


IMG-20210824-WA0067.jpg


IMG-20210824-WA0065.jpg


IMG-20210824-WA0064.jpg


IMG-20210824-WA0063.jpg
 
Safi sana nimejitahidi sana kufuatilia ziara na matukio ya mh. Dc Iramba kupitia page zenu zaidi ya instagram kwakweli Mh dc anafanya kitu cha tofauiti na kikubwa sana, hizi ziara zina tija sana kwa wananchi, kuliko kukaa tu oficn,
sinabudi kusema Kongole kongozi.
 
Huyu DC anafanya kazi kwelikweli. Toka nasikia kateuliwa hajawahi kukaa chini. Ni mwendo wa safari za kusikiliza na kutatua kero tu kila siku. DC kama huyu ukimpandisha akawa RC ujue huo Mkoa unapaa sana. Watu kama hawa wenye commitment kubwa ya utumishi wa watu kama Mhe Mwenda ni WA kupandishwa juu kileleni ili nchi inufaike nae sana.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom