DC Mwenda awafunda vijana jinsi miaka 60 ya uhuru uchumi wa Tanzania ulivyobadilika

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
DC MWENDA AWAFUNDA VIJANA JINSI MIAKA 60 YA UHURU UCHUMI WA TANZANIA ULIVYOBADIRIKA

Maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru mkoani Singida vijana wamefanya Kongamano Vijana na wametakiwa kuenzi miaka 60 ya uhuru wa Tanzania bara na miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanziba kwa kuangalia mabadiliko katika nyanja za uchumi utamaduni na namna ya upatikanaji wa viongozi unavyofanyika hapa nchini.

Akiongea katika Kongamano la Vijana lililofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Mkuu wa ya Iramba Mhe. Suleimani Mwenda amesema hali ya uchumi wa Taifa umebadilika kwa kiasi kikubwa kabla na baada ya uhuru hivyo Vijana wanatakiwa kujifunza kutokana na mabadiliko hayo.

DC Mwenda akabainisha kwamba katika kipindi cha baada ya uhuru kulikuwa na Chuo Kikuu kimoja cha Dar es Salaam ambacho kilichukua wanafunzi wachache hivyo kusababisha walio wengi kukosa fursa ya kupata elimu ya juu, ikilinganishwa na kipindi hiki ambapo vyuo ni vingi sana zaidi ya 50 nchini.

Amesema ukizungumzia Uhuru wa Tanzania unazungumzia uhuru wa nchi nyingi za Kiafrika kwakuwa Tanzania ilishiriki katika kutafuta ukombozi wa Mataifa mengi ya Kiafrika yakiwemo Msumbiji, Afrika ya Kusini jambo ambalo vijana wanatakiwa kufahamu hali ya ukarimu ambao umekuwa ni sehemu ya utamaduni wetu.

Aidha siasa za Tanzania hasa namna ambavyo viongozi wamekuwa wakibadilishwa kwa njia ya chaguzi ambapo Mataifa mengi yamekuwa yakishikwa na butwaa hasa kwa kuangalia nchi za jirani na Tanzania ambazo zimekuwa zikiingia kwenye migongano mara kwa mara.

Awali DC Mwenda alitoa shukrani za dhati kwa wandaaji wa Kongamano hilo ambalo liliwafungua Vijana na kuwafanya kuwa wazalendo na kuwaonesha fursa mbalimbali zinazowazunguka.

DC Mwenda akabainisha umuhimu wa kufanyika kongamano hilo wilayani Manyoni kwa kuwa ilikuwa ni sehemu ya kuwafundisha Vijana umuhimu wa nashujaa waliotokea Manyoni katika mapambano ya kudai uhuru.

Kwa upande wake Afisa Vijana Mkoa wa Singida Fredrick Ndahani akaishukuru Serikali kwa kufufua na kuendeleza shirika la ndege nchini na ambapo awali lilikuwa na ndege moja lakini baada ya miak 60 ya uhuru shirika lina ndege 11.

Ndahani alisema shirika hilo linatoa fursa kwa vijana kufanya biashara ndani na nje ya nchi kwa kwa kuwa miundombinu ya barabara na anga vimeendelezwa kwa kiasi kizuri sana.

FB_IMG_1638849560691.jpg

FB_IMG_1638849555796.jpg

FB_IMG_1638849551468.jpg

FB_IMG_1638849548021.jpg

FB_IMG_1638849543508.jpg
 
Hoja ya kisiasa inayoongelea masuala ya kiuchumi,in reality maisha ya mtanzania wa kawaida yamekua magumu mno kuliko hiyo miaka inayosemwa, huku Lingusenguse nothing much changed katika miaka hiyo, wale maadui 3 bado wapo na wanasumbua mno hasa adui UJINGA, universities ni mfano wa hovyo uliotumika hapa, tunahitaji QUALITY na sio quantity, nchi vyuo zaidi ya 50 na hakuna hata kimoja kinachojishindanisha na dunia, miaka ya 70s hadi 80s UDSM kilikua ndani ya top 20 ya vyuo bora hapa Africa,but now kimepotea kabisa na hata majarida yake sijui yanachapwa wapi au tafiti zake. Tunahitaji tufanye mabadiliko makubwa ndani ya nchi yetu kinyume chake tutabakiwa na hadithi hizi tinazoletewa sasa.
 
Back
Top Bottom