DC Mwenda atumia siku ya wanawake kueleza makubwa yaliyofanywa na Rais Samia

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Mhe. Suleiman Yusuph Mwenda amesema kwa muda mfupi wa Uongozi wa Rais Samia Suluhu, Wilaya yake imepokea Mabilioni ya fedha ambayo hayakuwahi kuletwa kwenye maendeleo kwenye Wilaya hiyo.

Mhe. Mwenda ameyasema hayo Jana Jumanne Machi 08, 2022 wakati akihutubia maelfu ya Wananchi waliohudhuria katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kiwilaya katika Viwanja vya Shule ya Msingi Tumaini.

Akiongelea michango muhimu inayofanywa na
Wanawake nchini, Mhe. Mwenda alisema kuwa tunaye Mwanamama Shupavu ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye kwa kipindi cha miezi michache amefanya mambo makubwa ambayo hayajawahi kutokea katika historia ya nchi yetu.

Aidha, alifafanua kuwa katika kipindi cha awamu ya kwanza ya Urais hadi ya tano, Wilaya ya Iramba kulikuwa na vituo vya afya vitatu tu lakini katika kipindi cha Rais Samia tayari Iramba inajenga vituo vya afya vitano na maendeleo haya ni katika wilaya zote za nchi yetu.

Kwa upande wa barabara kwa mara yakwanza katika kipindi hichi cha Rais Samia, Iramba ilipata Tsh 6.5 Bilioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara huku fedha nyingi yakwanza kuja wilaya ya Iramba tangu kupata uhuru kwenda kwenye barabara ilikuwa ni Tsh 800 milioni pekee.

Pia, katika nishati ya umeme tayari Mkandarasi ameshapatikana ambaye atamalizia vijiji 14
vilivyokuwa havina umeme, hivyo ni dhahiri sasa Iramba itakuwa haina kijiji ambacho hakina umeme.

Hali kadhalika, kwa upande wa madarasa kwa ajili ya wanafunzi, Iramba ilifanikiwa kupata fedha na kujenga madarasa 67 huku madarasa zaidi ya elfu kumi na tano (15,000) yakijengwa kwa Tanzania nzima. Katika kuhakikisha mama anatuliwa ndoo kichwani na maji yanapatikana kwa urahisi takribani Tsh 4.8 Bilioni zinatekeleza miradi mbalimbali ya maji nakuifanya Iramba kufikia asilimia 52 ambapo wakati Rais Samia anaingia madarakani Iramba ilikuwa na asilimia 26 tu.

“Kwa kweli kwa ushahidi na takwimu hizi
ninashawishika kusema kuwa tukiwaamini
wanawake katika nafasi za uongozi tutapata matokeo makubwa chanya.” Alisema Mhe. Mwenda.

IMG-20220309-WA0026.jpg


IMG-20220309-WA0027.jpg


IMG-20220309-WA0024.jpg


IMG-20220309-WA0025.jpg


IMG-20220309-WA0023.jpg
 
Back
Top Bottom