Dc Muro azungumzia chanjo za corona, adai watanzania sio watu wa majaribio. Awataka viongozi wa dini kutoyumba kiiimani

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Mkuu wa wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Jerry Muro ametamka ya kwamba msimamo wa Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kuhusu kutoruhusu uingizaji wa chanjo za corona hapa nchini ni wa kishujaa kwa kuwa watanzania hawawezi kutumika kama majaribio.

Pia amewashauri baadhi ya viongozi wa dini nchini kutoyumba kiimani kwa kuwa baadhi yao wamegawanyika na kukosa msimamo kutokana na ugonjwa wa corona.

Muro alitoa kauli hiyo leo katika kanisa la kiinjili na Kilutheri nchini (KKKT) usharika wa Enaboishu wakati wa ibada ya shukrani ya familia ya Elphace Mollel iliyopo mtaa wa Oloigero.

Akizungumza kanisani hapo Muro alisema kwamba Rais Magufuli hajapinga ujio wa chanjo ya corona lakini alichopinga ni chanjo hizo kutumika kwa watanzania kama majaribio.

Muro,alisema kwamba Rais Magufuli atawavusha watanzania salama katika janga la Corona na anathamini watu wake na hivyo msimamo wake wa kuzipinga chanjo hizo za majaribio unapaswa kuungwa mkono.

“Msimamo wa Rais Magufuli kutotaka chanjo za corona kutumika kama majaribio kwa watanzania ni wa kishujaa sio kwamba amekataa chanjo zisiletwe nchini lazima tuelewane huyu Rais wetu anawathamini watu wake sana “alisema Muro

Hatahivyo,aliwashauri baadhi ya viongozi wa dini kuwa na msimamo katika imani kwa kuwa wao wamepewa jukumu la kuwachunga kondoo na sio kuwatia hofu.

Awali Mchungaji aliyeongoza ibada hiyo,Samwel Laiser alisema kwamba pamoja na serikali kupitia wizara ya afya kutoa mwongozo katika kupambana na ugonjwa wa Corona lakini watanzania wanapaswa kumtegemea Mungu kwanza.

Alisema kwamba watanzania wanapaswa kuondokana na hofu katika kipindi hiki kwa kuwa ugonjwa wa corona ni janga litakalopita na kuwasihi wasimame imara muda huu kumtegemea Mungu katika maombi,sala na shukrani.

“Neno na Mungu ndilo linalotia nguvu endeleeni kumtumikia Mungu sote tuondoe hofu na mashaka pamoja na wizara ya afya kutoa maelekezo lakini maombi yawe nambari moja “alisema Laiser

Akitoa shukrani katika ibada hiyo,Mollel alisema kwamba anamshukuru Mungu kumponya mama yake mzazi aliyelazwa mahututi katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) akipumulia mashine na ameamua kutoa shukrani kumshukuru Mungu.

Mollel,alisema watanzania wanapaswa kumshukuru Mungu katika janga la corona na kumuombea Rais Magufuli kwa kuwaondolea hofu kwa kuwa awali hofu ilikuwa inawaua kuliko corona.

Mwisho.....
IMG_20210306_160451_5.jpg
IMG_20210306_170023_0.jpg
IMG_20210306_171652_8.jpg
IMG_20210306_171711_8.jpg
 

Attachments

  • IMG_20210306_171711_8.jpg
    IMG_20210306_171711_8.jpg
    81 KB · Views: 1
Back
Top Bottom