Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 749
- 1,797
VIONGOZI wa dini wametakiwa kuondoa dhana ya kuishi kwa kutegemea sadaka za waumini na michango ya wahisani badala yake wafanyekazi kwa bidii ikiwemo kutumia taaluma zao kuinua uchumi wa Taifa.
Kauli hiyo ameitoa mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro ,ambaye alilazimika kutiririkwa na machozi mara kwa mara wakati watumishi hao wa mungu wapatao 300 wakishusha maombi ya nguvu kwa rais John Magufuli, yaliyofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha ualimu Patandi kilichopo wilayani humo na kushirikisha maaskofu,Mapadri na wachungaji.
Askofu wa kanisa la Blessing Altar, Isaya Sezya amesema kuwa rais Magufuli ni mzalendo na ameonyesha dhamira ya kweli ya kulikomboa taifa kwa kupambana na mafisadi waliokuwa wananufaika na rasilimali za nchi kwa maslahi yao binafsi.
Muro aliwataka viongozi wa madhehubu hayo kufanya kazi kwa bidii ikiwemo kutumia taaluma zao kujenga uchumi badala ya kukaa na kutegemea sadaka kama sehemu ya kipato chao.
Kuhusu malalamiko yaliyowasilishwa ofisini kwake na baadhi ya wananchi juu ya makanisa yanayomea kama uyoga kwenye makazi ya watu Muro alisema ni vyema makanisa hayo yakawa na vifaa maalum vya kuzuia sauti kutoka nje ili kuepuka kusumbua watu nyakati za usiku wakati wa maombi.
Alisema kwa kipindi chake atakachokuwa mkuu wa wilaya hiyo hakuna kanisa litakalofungwa na serikali na kwamba atashirikiana na viongozi wa makanisa hayo kufanya harambee kwa ajili ya kujenga makanisa yenye vifaa maalum vya kuzuia sauti.