DC Muro asambaratisha baraza la madiwani wa Meru na Polisi

Huu ujinga wenu Wa kuivuruga amani kisha mjidai kuirejesha kwa mbwembwe na kamera nyingi IPO Sikh utabuma!
Jerry kaikuta arumeru ikiwa poa kabisa na inajiletea maendeleo yake ila baada ya ujio wake kila kitu kimekenda hovyo akidhani ataweza kuwageuza wanaarumeru kuirejea ccm!
Ajiandae tu kuiba kura na siyo vinginevyo!
Huyo hatafanikiwa na hizo hila zake , Meru wapi imara hawezi kuwabadilisha huku ni , " piiiiipooooooz pawa!¡!!!!
 
Huyo hatafanikiwa na hizo hila zake , Meru wapi imara hawezi kuwabadilisha huku ni , " piiiiipooooooz pawa!¡!!!!
Anamzuga aliyemteua ili kulinda kibarua chake lakini kiuhalisia alishafeli tangu awali! Hao wazee au wachili wanamchora tu!
 
Huyu DC ni mchapakazi sana na uthibitisho ni huu
.

Hivyo linapokuja suala la utulivu na amani, Muro hana mchezo kabisa, enzi akiwa mwandishi, alikuwa anatembea na pisto na pingu na enzi hizo alikuwa hana mamlaka ya nguvu za dola, sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, hivyo Arumeru sasa ni heshima adabu.

P
Mayala
 
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro
Ambaye pia ni Mwenyekiti Wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo, ameamuru polisi kuwatimua Madiwani wote waliokuwa kwenye kikao cha baraza la Madiwani wa halmashauri ya Meru .

Muro alitumia Mamlaka yake hayo kwa kile alichodai ni kunusuru amani iliyotishia kutoweka katika kikao hicho kufuatia malumbano yaliyokuwa Yakiendele baina ya Madiwani hao kujibizana pasipokuwa na hoja yamsingi na kupelekea kuhatarisha usalama wao.

"Moja ya majukumu yangu ni kuhakikisha nazuia hali yoyote ya viashiria vya uvunjifu wa Amani"Alisema Muro

Baraza hilo la Madiwani lilivunjika na kushindwa kuendeleauwasilishwa Taarifa za maendeleo za kata 10 kutokana na kuwepo kwa sintofahamu kati yabaadhi ya wajumbe kutaka kuondolewa Kwa diwani wa Viti maalumu Chadema kwamadai ya kuvuliwa uanachama na chama chake.

Katika Baraza hilo la robo ya 4 ya mwaka 2018/2019 lililokuwa na Agenda yakupokea Taatifa zamaendeleo zakata ,diwani wa kata ya Kikwe Paul shangwe alisimama na kuomba mjumbe huyo Digna Nasari viti maalumu kata ya maruvango kutolewa nje kwani chama chake cha demokrasia na maendeleo chadema kilishamvua uanachama wake na kuja kwake pale hakuwawa na barua yakumtambulisha kama ni diwani kwani tayari alishavuliwa uanachama wake,

Aidha diwani huyo Amesema kanuni ya 21kifungu (h)cha sheria za halmshauri hiyo hakiwezi kujadili taarifa zakata wakati kuna hoja iliyojitokeza ya diwani huyo kuvuliwa udiwani wake hali iliyopelekea kuwepo kwa malumbano kwa baadhi ya wajumbe wa chadema kumtaka Mwenyekiti wa baraza hilo kutumia kiti chake kumtomruhusu kubakia kwenye kikao hali na kudai kutokuwa na imani na Mwenyekiti kwakutokutoa maamuzi.

Mwenyekit wa halmashauri ya wilaya ya meru Willy Njau baada yakuona uwepo wa malumbano kwa zaidi ya nusu saa nakupelekea kutoelewana alisema kwa mujibu wa kanuni ya 18 inamruhusu kutoa maamuzi ya mwisho kwenye kikao hicho licha ya kuwataka Madiwani hao kuwa nasubira kwani suala hilo angelitolea ufafanuzi siku ya kesho ambapo angetoa hotuba yake yaufunguzi,kwani majibizano hayo yanaonyesha utovu wa nidhamu na nikosa kwa Madiwani kukidharau kiti chake.

Akijibu shutuma zakuvuliwa udiwani viti maalumu Digna Nassari kata ya maruvango Amesema nikweli Awali palikuwa na mgogoro na hali kutoelewana kati yake na viongozi wachama chake na maamuzi yaliyotolewa na chama chake hakuridhika nayo nakueleza kuwa ataendelea kuwa diwani.

Ends.....

View attachment 1193227
Hivi kwa nn chadema wanapenda fujo sana, Dc aliamua kufanya hivyo kwa kuwa aliona kunakoelekea sio kuzuri na naamini Dc angewaacha waendelee kurumbana najua wale wapenda kuleta uchochezi wangeleta huku kwa lugha nyingine.
 
Back
Top Bottom