DC Muleba: Nitaagiza mafisa elimu wakafundishe kuziba pengo la walimu

Magane

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
202
57
Wana jf leo katika taarifa ya habari ITV, DC wa Muleba ameamuru maafisa wa elimu waingie darasani wakafundishe ili kuokoa vijana wanaojiandaa kwa mitihani ya kumaliza elimu ya msingi.

Is this practically possible au ni hamaki tu. Ama kweli fahari wagombanapo ni nyasi zinazoumia. Let these two faharis, serikali na cwt wakae pamoja haraka sana wamalize tofauti zao ili walimu warudi darasani wakafundishe watoto wetu.

Athari ya mgomo wa walimu kwa watoto wetu ni ya muda mrefu na pengine athari hizi ni zaidi ya migomo mingine ya wafanyakazi. Elimu ni ufunguo wa maisha na ni haki ya msingi kwa watoto wetu.

Kwa hiyo tunaiomba serikali yetu urudi katika meza na CWT waweke pembeni politics. Ni imani yetu wakijadiliana in good faith kutoka kila upande utapatika muafaka.

Naamini malalamiko ya walimu ni ya msingi na yamekuwepo kwa muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.
 
Nimesikiliza kwenye ITV mkuu wa wilaya akiagiza maafisa elimu wa wilaya waende wakafundishe kwenye mashule kutokana na kuendelea kwa mgomo wa walimu.

Maagizo haya yananifanya niamini ukuu wa wilaya hauna maana katika hii nchi kwani hata watu wenye upeo hafifu kama wa huyo mkuu wa wilaya anaweza kuupata basi ni cheo kisicho na tija kwa taifa.

Nimejiuliza wilaya moja wapo maafisa elimu wangapi? watafundisha masomo gani na shule ngapi? Je, hiyo itasaidia kuondoa tatizo?

Nimejiridhisha wakuu wa wilaya hawahitajiki na nimeona aibu kwa mtu mzima kuongea ujinga kama ule mkuu mzima wa wilaya anaongea mawazo mepesi na dahifu kiasi hicho nimeona aibu ssana.

Sijaweza kulifahamu hata jina lake ni aibu kwelikweli.
 
huyo mkuu wa wilaya ni kichaa kabisa. sijaona busara yake hapo anatoa mawazo mepesi utadhani ni balozi wa nyumba kumi wa CCM. kweli ukuu wa wilaya ni kituko.
 
Nanukuu........."nitawachomoa maofisini waje kufundisha..............." watoto wamempigia ngoma naye kakubali kuicheza
 
Huyo mkuu wa wilaya ya mleba kimuonekano hana tofauti na m/kiti wa kitongoji,
halafu hana hata lugha ya kisomi anasema eti tutawachomoa maafisa elimu huko maofisini ili waje wawafundishe,kweli?!!?
Aise hawa magamba kama wanaoshughulikia hili tatizo la walimu ndio wana akili ka za huyo mkuu wa wilaya basi kazi ipo,
 
Tutafanyaje ndo viongozi wetu hao tunaotegemea watuletee maendeleo. Long way to go.
 
Maagizo haya yananifanya niamini ukuu wa wilaya hauna maana katika hii nchi kwani hata watu wenye upeo hafifu kama wa huyo mkuu wa wilaya anaweza kuupata basi ni cheo kisicho na tija kwa taifa.

Nimejiuliza wilaya moja wapo maafisa elimu wangapi? watafundisha masomo gani na shule ngapi? Je, hiyo itasaidia kuondoa tatizo?

Nimejiridhisha wakuu wa wilaya hawahitajiki na nimeona aibu kwa mtu mzima kuongea ujinga kama ule mkuu mzima wa wilaya anaongea mawazo mepesi na dahifu kiasi hicho nimeona aibu ssana.

Sijaweza kulifahamu hata jina lake ni aibu kwelikweli.
Pole ndugu. Ndo Tanzania hiyo ktk miaka 50 ya uhuru.

Sijui ana maafisa elimu wangapi hapo wilayani mwake wa kukudhi pengo la walimu waliogoma. Na sijui yy ni nani kuwaagiza hao maafisa elimu kufundisha. Mwajiri wao hajasema neno yy political leader anajchanganya.
 
Huyu jamaa ni hopeless kabisa nilimsikia sikumuelewa kabisa..hao ndo wakuu wa wilaya wa jk
 
Utafiti unaonesha kwamba shule ambazo makada wa ccm ni wengi miongoni mwa wana CWT hawakuunga mkono mgomo. Magamba hawakujua kuwa ni hatari kuhusisha mgomo huu na siasa?freedom is coming 2mmor!
 
muhurumieni jamani mana alikua anausongo san kwani toka apewe hicho cheo hajawah kuuza sura kideoni
 
Kweli tangu aingie pale hajawahi kutokea kwenye luninga,atauzaje wadau wake wamjue kuwa nae ametoka povu??pumba kwenda mbele!! Angesema na yeye atajitolea afundishe darasa la saba uwanja wa mpira...ili wajibu paper ......hivi mtihani wa darasa la saba lini??
 
ameiga kwa liwalo na liwe aliesema atawatoa maafisa wa wizara ya afya na madokta wastaafu wakatibie mhimbili.!
 
Athari za serikali Dhaifu inayoshindwa kukaa na kada mbalimbali za watumishi wake ili kuondoa/kupunguza kero zao ni zipi?
 
Back
Top Bottom