DC Mtatiro: Marufuku kufanya Sherehe za darasa la saba, fedha za Sherehe wazitumie kuwasomesha wasiwe mzigo kwa Taifa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,847
141,769
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mh Julius Mtatiro amepiga marufuku sherehe za kuhitimu elimu ya msingi yaani Darasa La Saba wilayani kwake.

Mtatiro amesema kuhitimu darasa la saba ni sawa na Sifuri hivyo kufanya sherehe ni kuwadumaza wanafunzi na kuwafanya wawe na mawazo ya kimasikini yatakayoharibu future zao.

DC Mtatiri amemuagiza OCD kuwakamata wote watakaokaidi amri yake.

Source ITV habari

My take

Dr Msukuma, Kibajaji na Jah People ni LA SABA lakini wako bungeni.

Maendeleo hayana vyama!

=======

Maelezo ya Mheshimiwa Julius Mtatiro

========

Julius Mtatiro said:
Tunachopambana nacho hapa Tunduru ni kitu tofauti kabisa. Kinachonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari sicho tunachokifanya hapa. Mahafali za darasa la saba zinaendelea Tunduru nzima na hizo ni za kudumu. Tofauti na maeneo mengi ya nchi yetu, Tunduru kuna sherehe 2 za kuwaaga darasa la saba. Ya kwanza ni mahafali yanayoandaliwa na shule yakiwashirikisha wahitimu, wazazi wao na wanafunzi. Haya ni mahafali sahihi na hufanyika kabla ya mitihani ya darasa la saba na wageni rasmi huwa ni viongozi wa kiserikali, kijamii na sekta binafsi kwa kadri ya chaguo la shule husika. Kwa Tunduru shule kadhaa za msingi ziliniita kwenye mahafali haya mwaka 2019 na nilihudhuria.

Mahafali ya pili ni yale ambayo hayako rasmi, haya yanafanywa na wazazi siku ambayo kijana wa darasa la saba anakamilisha mitihani yake. Wazazi hushona sare, huandaa vyakula na hualika majirani na ndugu, hufunga safari hadi shuleni wakaizingira shule wakimsubiri binti au kijana atoke kwenye chumba cha mtihani. Hapo nje humlaki na kuanza maandamano ya kijiji kuwarejesha wahitimu kijijini kuendelea na sherehe za kifamilia. Familia za Tunduru zinatumia fedha nyingi sana katika sherehe hizi, na mantiki yao ni furaha kuwa mtoto aliyehitimu ataolewa au kuwa nguvu kazi, furaha zaidi huwa ni juu ya dhana kuwa mtoto amemaliza shule na wazazi wametua mzigo!

Kichekesho zaidi huwa ni ikishafika mwezi Januari mwaka unaofuatia, zaidi ya nusu ya watoto wa Tunduru waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza huwa hawaripoti shuleni, sababu zinazotolewa ni; wazazi kukosa uwezo wa kuwanunulia sare za shule na madaftari; wazazi kuamini kuwa elimu ya darasa inatosha; wazazi kuamini kuwa watoto waliomaliza darasa la saba wanapaswa kuoa na kuolewa na kuanza maisha n.k. .
.
Kwa mfano mwaka jana 2019, wahitimu wa darasa la saba Tunduru ni 4,959, ambapo 100% wamechaguliwa kuanza kidato cha kwanza lakini watakaoripoti shuleni ni 50%, nusu ya waliochaguliwa hawataripoti hadi tuanze oparesheni za kukamata wazazi wao n.k. Lakini kwenye yale mahafali ya pili ya kushona sare na kununua vyakula na zawadi 100% ya wahitimu hufanyiwa, ikifika kwenye kununua sare za sekondari 50% ya wazazi husema hawana uwezo.

Tunachopambana nacho Tunduru ni kuzuia na kuelimisha wazazi waachane na tabia zenye madhara kwa watoto wao, tabia ambazo huwabwetesha watoto kudhani elimu ya darasa la saba ndiyo elimu kubwa, tabia ya kuwafanya wazazi waamini kuwa jukumu la kuwalea watoto kielimu linaishia darasa la saba.

Kama sherehe hizi na mbwembwe za wazazi na wanafunzi wao siku ya kumaliza mtihani wa mwisho zingelikuwa zinafanywa kwa nia nzuri, nia ya furaha kwa wazazi kwamba watoto wao wanajiandaa na kidato cha kwanza, hata mimi DC ningelienda kushiriki kwenye sherehe hizo na shati ningelivua nijumuike na wananchi, lakini UNFORTUNATELY ni sherehe zinazofanya kuaminishana kuwa sasa KAZI YA MZAZI NA MTOTO KIELIMU IMEKWISHA na imefika mwisho!

Tunduru ni eneo ambalo inatupasa tutumie nguvu kubwa sana kuwafanya wazazi wajue na waone umuhimu wa elimu. Tumekuwa tukiwashauri na kuwaelimisha wazazi wetu kuwa elimu ya ANGALAU katika nchi yetu KIDATO CHA NNE kinachoambatana labda na CHETI CHA VETA cha ujuzi fulani. Tunatamani kila mtoto wa Tunduru walau afike kidato cha nne na asomee ujuzi fulani na huyo ndiye tuseme hajasoma sana, tunataka watoto wa Tunduru wawe wahandisi kwa wingi, madaktari kwa wingi, wanasheria kwa wingi, walimu kwa wingi n.k.

Jambo moja ambao watu wengi hawalijui, Tunduru ni wilaya yenye watoto wenye IQ ya hali ya juu mno (watoto wa huku wana akili mno, kushinda hata wilaya yangu ya asili). Shida yetu Tunduru ni mwamko wa wazazi walio wengi, ambao wanaamini elimu ni mzigo na ni kitu cha kutua mtoto akimaliza mitihani yake ya mwisho.

Kwa hiyo kwa mwaka huu 2020, kila shule ya msingi itafanya mahafali moja tu ambayo ni rasmi na itawahusisha wazazi, walimu, wahitimu, wanafunzi, ndugu, jamaa na marafiki. Ile mahafali ya pili ambayo hufanywa na wazazi peke yao kwa kuwafuata watoto wao shuleni wakiwa kwenye vyumba vya mtihani wa mwisho, na kutumia gharama nyingi kufurahia KUTUA mzigo, tumeipiga marufuku na haitafanyika tena.

Fedha ambazo wazazi walikuwa wanatapanya kufurahia watoto kumaliza darasa la saba tumewataka waziwekeze kwenye maandalizi ya vijana hao kuanza kidato cha kwanza kila mwezi January.
@juliusmtatiro
 
Watu wamefanya elimu ya tz ya kichwa Cha mwendawazimu kila anayejisikia anaagiza anachotaka!

Ndalichako - hakuna kuvaa joho isipokuwa mpaka digrii eti inashusha hadhi ya joho na hamasa ya kusoma

Waitara- kazuia uamisho wa walimu nae eti anaimarisha elimu

Mtatiro - hakuna graduation

Maofsa elimu - hakuna likizo Sasa hivi mwaka mzima wanafunzi wanasoma hakuna kupumzika! hasa madarasa ya mitihani! Mpaka watoto wanakuwa frustrated!

Ma-RC +REO + DEO Wanaweka kambi wanafunzi wa Sanaa wafundishwe masomo matatu tu! (Kiswahili, civics na Historia.) Masomo mengine hawafundishwi eti wafaulu 'D' Tatu wapate vyeti.

Wakuu wa shule - wanasahihisha lesson plan na kuweka alama katika jitihafa zao za kuimarisha elimu.
 
CCM ni mzigo wa taifa letu. tumeumia. mtatiro niliyemjua kawa ziro brain taslimu.

Naogogpa sana hata ukihamia CCM unakuwa ziro kama huyu hafai hata kwa mboga
 
Angeanza kufuta za chekechea kwanza. Kila mtu hupenda kufurahia hatua alofuzu kwenye maisha. Anataka kutuambia miaka saba ya mtoto kwenda shule haikuwa na maana?

Kuagana na watoto wenzao na walimu waliokaa nao miaka saba si kitu kibaya. Labda angeweka muongozo wa namna shughuli itavyofanyika lakini kufuta ninukosefu wa hekima za kiuongozi. Hii na hakika mkuu wa mkoa ataipindua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii nchi kila Wilaya ina sheria zake na kila kata ina taratibu zake.
Ule utawala wa majimbo ndio umekuja kivingine? Wajuzi mtusaidie, usikute tukiemkataa amebadili kanzu, na kuingia 'msikitini'
 
Hivi huu wivu wa kijinga wa watu wazima kwa watoto tumeutoa wapi...!

Sherehe ya masaa manne tu Serikali ya tunduru inaathirika vipi...!

Nilishangaa mmoja alipopiga marufuku majoho kwa baadhi ya sherehe badala ya kutofautisha rangi na design ya hayo majoho kwani hata chekechea akivaa hapunguzi kitu ikiwa wazazi wake wameridhia bila shurti ashiriki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom