DC Mtatiro avitaka vyama vya Ushirika, akiba na mikopo kuzingatia Sheria na kuacha mazoea

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Ndg. Julius Mtatiro, amevitaka vyama vya ushirika na vyama vya akiba na mikopo kuzingatia taratibu na sheria katika utendaji kazi wao na kuacha kufanya kazi kwa kwa mazoea.

Ndugu Mtatiro ametoa rai hiyo leo alipokuwa akifunga mafunzo ya siku ya tatu ya vyama vya ushirika na vyama vya akiba na mikopo yaliyoandaliwa na Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Shirika la Ukaguzi na usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (Tawi la Ruvuma) na Maafisa Ushirika wa Wilaya ya Tunduru.

DC Mtatiro ameonya michezo michafu na vitendo visivyokubalika na kuwataka wana ushirika wote kuwa na msimamo wa kujali wakulima na ukuaji wa ushirika na vyama vya ushirika.

Mtatiro amewakumbusha viongozi wa Ushirika kuwa serikali ya wilaya iko macho na itahakikisha wale waote wanaojaribu kuyumbisha ushirika katika chaguzi zinazoenda kuanza hivi karibuni wanachukuliwa hatua bila kuonewa haya.

Mtatiro amewataka viongozi wa ushirika kuuchukulia kama sekta muhimu mno na yenye tija akitolea mfano kuwa wilaya ya Tunduru kwenye msimu ulipita 2018/19 wakulima ameweza kupata jumla ya shilingi bilioni 61kwenye korosho na msimu wa 2019/20 wakulima wamepata shilimgi bilioni 67 huku wakitarajia kupata shilingi bilioni 5 katika ufuta baadaye mwaka huu. Mtatiro amesisitiza fedha zote hizo zinapita katika vyama vya ushirika na vyama vya msingi na amewataka wadau wa vyama hivyo kuhakikisha wanawachagua viongozi wenye uwezo wa kulinda na kutetea maslahi na fedha za wakulima.

Ni kutoka hapa ukumbi wa Cluster Tunduru, Alhamisi 20 Februari 2020.
 
Back
Top Bottom