DC Msando na DC mwenzake wahamishiwa Muhimbili kwa matibabu zaidi lakini wako stable

Mkuu wa wilaya ya Morogoro Albert Msando na mwenzake wa Ulanga waliopata ajali leo wamehamishiwa hospitali ya taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.

Msemaji wa Hospitali ya Rufaa Morogoro amesema viongozi hao hali zao zinaendelea vizuri na wako stable.

Dereva na Wauguzi wawili waliokuwemo kwenye gari ya DC wanaendelea vizuri.

Source: TBC

Mungu ni mwema wakati wote!
Roho wa Bwana akawe juu ya Afya zao. Na watakapopona awaongoze kutenda yaliyo mema dhidi ya wanaowaongoza.
 
MaDC wawili na Manesi wawili.

Dereva alikuwa anaona mapicha picha tu!
Yaani Manesi badala ya kukaa kwenye gari la Wagonjwa (ambulance) wakakaa kwenye gari la DC? Na Manesi siku hizi hawavai sare wakiwa kazini au kwenye misafara ya wakubwa hawaruhusiwi kuvaa sare?
 
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Albert Msando na mwenzake wa Ulanga waliopata ajali leo wamehamishiwa hospitali ya taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.

Msemaji wa Hospitali ya Rufaa Morogoro amesema viongozi hao hali zao zinaendelea vizuri na wako stable.

Dereva na Wauguzi wawili waliokuwemo kwenye gari ya DC wanaendelea vizuri.

Source: TBC

Mungu ni mwema wakati wote!
Hata mwendazake tuliambiwa Yuko vizuri mwishowe.....
 
Kosa kubwa la kuwapandisha viongozi zaidi ya mmoja kwenye gari moja. Ikitokea kama haya ndio utaelewa kwa nini viongozi hata kama wanaenda kumoja wanapanda magari yao tofauti tofauti
Na ndege pia wakisafiri wapande ndege tofaut tofaut
 
Nawatakia soon recovery wote majeruhi katika ajali ile. Pia na ile Frester ya Dar Bk iliyoacha njia Isaka na kupoteza kijana wa miaka 35. Mnyazi Mungu awaponye haraka ajali ni mbaya sana hizi zisikie tu.

Ila sasa ajali ya DC na gari yao STL na ile gari ya DFP ukiangalia kwa haraka haraka hawa madereva wa serikali na hawa wa mashirika hawa yaani njiani highway huko hawanaga refa wanajiachiaga sanaaaa. Aisee barabara hainaga mbabe.

Jamaa wanafukiaga hawanaga 50km/hr wala nini ni mserereko tu hakuna tochi yaani wanatambaa tu utafikiri wanawahi mbinguni au wanaendesha space crafts za akina Jef Bezos vile.

Ule mzinga tena wa mav8 yote niwakibabe heads on kila mtu alikua anawahi mwingine anawahi kuungana na msafara wa PM mwingine sijui wapi.

Tunawapa Onyo wajifunze ila hawatasikia.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
Na wanachokiwahi mara nyingi hata hatukioni. ovyooo. Ingekua utendaji wa KAZI unafanyika kwa haraka km wanavyowahigi hivi Tanzania tungekua mbali Sana.
 
Kosa kubwa la kuwapandisha viongozi zaidi ya mmoja kwenye gari moja. Ikitokea kama haya ndio utaelewa kwa nini viongozi hata kama wanaenda kumoja wanapanda magari yao tofauti tofauti
Siyo kosa, hiyo Ni ajali viongozi Ni bunadamu Kama wengine. Kuna Basi zinabeba watu zaidi ya hamsini na zinapata ajali sasa huwezi sema Kila mtu apande gari yake.
 
Nawatakia soon recovery wote majeruhi katika ajali ile. Pia na ile Frester ya Dar Bk iliyoacha njia Isaka na kupoteza kijana wa miaka 35. Mnyazi Mungu awaponye haraka ajali ni mbaya sana hizi zisikie tu.

Ila sasa ajali ya DC na gari yao STL na ile gari ya DFP ukiangalia kwa haraka haraka hawa madereva wa serikali na hawa wa mashirika hawa yaani njiani highway huko hawanaga refa wanajiachiaga sanaaaa. Aisee barabara hainaga mbabe.

Jamaa wanafukiaga hawanaga 50km/hr wala nini ni mserereko tu hakuna tochi yaani wanatambaa tu utafikiri wanawahi mbinguni au wanaendesha space crafts za akina Jef Bezos vile.

Ule mzinga tena wa mav8 yote niwakibabe heads on kila mtu alikua anawahi mwingine anawahi kuungana na msafara wa PM mwingine sijui wapi.

Tunawapa Onyo wajifunze ila hawatasikia.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
Usimwandike Mungu vibaya, haitwi Mnyazi Mungu anaitwa Mwenyezi Mungu.
 
Back
Top Bottom