Sasa hivi yupo busy kidogo na walimu....Mzushi huyo....katutumia kisiasa
Umeongea vizuri...Kwa uelewa wangu, kwa kitendo cha DC Makonda kuwaambia mjikusanye kimakundi na kwa fani zenu ni kizuri sana na kwa namna moja nyie wenyewe mlipaswa mshikamane na muangalie mnaweza toka VIP kimaisha, mfano kwa wale mafundi fungueni gereji bubu mpige kazi na kwa wale walimu fungueni vijiwe vya tuisheni na pia wale wa masoko tembezeni bidhaa kama sabuni au miswaki ya viboksi. Makonda kawasaidia kukutana na nyie mjiongeze sasa badala ya kulalamika mitandaoni
Makamba naye alisemwa sana...Huyu makonda anasemwa sana ngoja nikae hapa niweze kumjua vizuri
Subirini tumalize hili la walimu harafu tutarudi kwenye jambo lenu,kwamaana hili la walimu zito kuliko lenu,si mnajua walimu walivyokuwa msaada sana kwa chama?Huyu jamaa anaonekana ni mjanja mjanja anajua kutafuta umaarufu kwa wakati muafaka.....sasa hvi yuko bize na ishu ya walimu kusafiri bure na kweli kapata kick sana !!!!
Ishu ipo hivi.....Mwaka jana sikumbuki tarehe mwezi wa sita DC wa wilaya ya Kinondoni alitukusanya vijana tusiokuwa na ajira(kula kulala) wa wilaya ya Kinondoni na wilaya zingine pia pale Leaders club Kinondoni mchana wa jua kali na kutupiga sound tamu na kutuambia tujigawe kulingana na elimu/taaluma/fani tulizosoma kwa mfano darasa la 7 kivyao, secondary kivyao, waliosoma ufundi kivyao,pia wenye elimu ya vyuo watengeneze vikundi kulingana na fani zao ...
Baadaye tukaandika miradi tunayoweza kufanya baada ya kuweka vikao vyetu kama mara 7 na ushee tena kwa kuungaunga. tukiwa na matumaini makubwa....
Cha kushangaza baada ya kumkabidhi ofisini kwake jamaa yupo kimya na kusababisha members kushikana mashati kwenye group zetu za WhatsApp kila mtu akimtafuta mchawi....
Bwana Makonda tuambie ule mpango umeishia wapi au ilikuwa kick tu ya kisiasa....Usije kesho ukatukusanya tena na kufikiri sisi ni malofa na wasahaulifu na kuleta mpango eti tuwe tunakula bure gengeni kwa mama ntilie...
Nawasilisha
Paulo????Wenye majina hayo hulka zao ni za kenge wanajifanya Wema kumbe wauaji!