DC Makala, hakikisha kuwa wamachinga wote hawarejei kwenye maeneo tena

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,293
12,593
Waliotii agizo la serikali la kuondoka bila shuruti kwenye maeneo yasioruhusiwa kwa biashara wanavunjika moyo kuona wenzao waliovunjiwa panoja bado wanaendelea na biashara zao kwenye maeneo yaleyale waliyoyahama. Hii itasababisha yafuatayo:

1. Wanunuzi wasiende kwenye maeneo mapya kutafuta na kununua bidhaa.
2. Waliohama maeneo kukosa wateja na kipato.
3. Waliohama kupata sonona.
4. Waliohama kuwaza kurudi pia kwenye maeneo Yao.
5. Serikali kudharaulika kwa kukurupuka.
6. Kuonyesha kuwa Kuna mvutano ndani ya Chama na serikali na ndani ya Chama na ndani ya serikali.
7. Wamachinga kugombana kwa kulazimisha kurudi kwenye maeneo Yao yaleyale waliyokuwa kabla ya kuvujiwa au kuondoka. Bila shaka maeneo Yao watakuta yanatumiwa na wale amabao wamegoma kuondoka na hakuna wanachofanywa.

Hii ni hatari kubwa sana kwa kiongozi yeyoye anaetoa maagizo yasiyosimamiwa. Rais Magufuli alitufundisha kusimamia maamuzi yako hata kama ulikosea kuamua.
 
Hapo juu kabisa kuna mmoja anahitaji usafi na haiba ya miji yetu na ndo anatoa ushirikiano kwa wenyeviti wa ulinzi na usalama wapate nguvu ya kulivalia njuga lakini hapo hapo juu mkono wa kushoto na kulia kuna watu kadhaa wanatamani zoezi lisifanikiwe maana wanafaidika kiuchumi na kisiasa kupitia wamachinga.
 
Machinga ni suala gumu sana, wanatakiwa watumie nguvu tu kama wanavyopambana na wapinzani hapo ndio watafaulu vinginevyo hamna kitu kimara wamerudi kama wote darajani, Mlimani City usiseme
 
Makala kanyooka kama Rula ila anaangushwa baadhi ya watu ndani ya Jeshi la Polisi, wamekuwa waoga kama Kunguru kuwasaidia Viongozi kwenye hili jambo.

Machinga wanapoelimishwa watoke wanatishia Usalama na kufanya uharibifu wa mali maeneo mengine ila hawawachukulii hatua kabisa.
 
Sababu kuu ya kuwaondoa hawa wanaofanya biashara sehemu zisizokuwa rasmi sio tu kuwa wanaikosesha Serikali mapato bali pia wanachafua Mazingira. Ndio maana kwa mfano huko Mbezi Beach sehemu inaitwa Mbuyuni na Rungwe barabara iendayo EFM utakuta watu wamejazana kwenye residential plots wanafanya biashara lakini hawana vyoo; hivyo kujisaidia hovyo hovyo kitu ambacho ni hatari kwa afya ya jamii.

Amos Makalla na wasaidizi wake wasiangalie majina ya wenye viwanja hivyo kuwa ni watu wakubwa bali wafuate sheria za mipango miji ama sivyo hapo baadae hizi sehemu zitaleta taabu zaidi kuliko sasa.
 
Kwani wafanyabiashara WALIOTII NA KUONDOKA ni wajinga?

Binadamu tumeumbwa na "kiasi"...na kiasi ni pamoja na utii wa maamuzi TUFANYAYO

Ilipofikia hakuna KURUDI NYUMA

SIEMPRE JMT
NCHI KWANZA
 
Hao watu wanasogeza huduma karibu zaidi kwa wananchi hasa wanyonge, unavunja vipi hadi magenge ya kuuza nyanya, vitunguu, matunda. Mnataka kila mtu akanunue nyanya na vitunguu mlimani city? Wanyonge watamudu kweli? manispaa wajipange namna watakavyowasimamia hao watu kwenye maeneo wanapofanyia shughuli zao, siyo kutumia ubabe tu kuwaondoa.
 
Makala kanyooka kama Rula ila anaangushwa baadhi ya watu ndani ya Jeshi la Polisi,wamekuwa waoga kama Kunguru kuwasaidia Viongozi kwenye hili jambo,Machinga wanapoelimishwa watoke wanatishia Usalama na kufanya uharibifu wa mali maeneo mengine ila hawawachukulii hatua kabisa.
Naskia askari wamekula kichapo maeneo ya zakiemu mbagala mnamo juzi
 
Hapo juu kabisa kuna mmoja anahitaji usafi na haiba ya miji yetu na ndo anatoa ushirikiano kwa wenyeviti wa ulinzi na usalama wapate nguvu ya kulivalia njuga lakini hapo hapo juu mkono wa kushoto na kulia kuna watu kadhaa wanatamani zoezi lisifanikiwe maana wanafaidika kiuchumi na kisiasa kupitia wamachinga.
Kazi ya serikali ni kuhakikisha kuwa viongozi na watendaji wote wanakuwa na uelewa na msimamo wa pamoja hata kama wengine Wana mawazo tofauti mioyoni mwao. Rais anawaunganisha Makamu vwake na Waziri mkuu na Baraza la mawaziri kwenye utekelezaji, Waziri mkuu anawakalia kooni mawaziribwake, Waziri awaunganishe wakuu wa mikoa, wakuu wa mikoa wawaunganishe ma DC na maDC wawawajinishe wakurugen wao na wakurugenzi waende kwa watendaji.

Inakuwaje machinga wanarudi wakati kiongozi wa mtaa, mtendaji kati, diwani, Mkurugenzi, DC, mkuu wa mkoa, mawaziri wa tamisemi, mazingira na biashara wapo? Kuna hujuma ya kuhujumiana. Ni nani afanye nini kuwaondoa hawa wanaohujumu zoezi hili la usafi ?

Mama tumia kofiabzako zote za ukuu wa nchi na ukuu wa Chama kuisafisha nchi iwe safi. Uholela ni tabia ya wanaume wengi lakini nabwanawake wachache sana. Kama mama safisha mitaa iwe safi kama ilivyo desturi ya akina mama zetu.

RC Makala fukuza kazi kila anaelihujumu hili zoezi
 
Makaka nahisi alitishwa na kauli ya yule katibu mwenezi..kwa kuwa amepata support ya mama hope ataendeleza wembe wake..otherwise ni aibu...mliman city pameanza kufura wamachinga..msenge usiseme..sinza kichefuchefu
 
viongozi wa chama huko matawini ndio vinara wa kupora maeneo ya wazi, ndio maana walikuwa wanamchukia Bashiru na mwenyekiti wake kwa kudhibiti mali za chama. kama maRC hawatakuwa macho jitihada zao za kumuunga mkono Rais kwenye zoezi hili la usafi zitagonga mwamba. Hapa wanamjaribu Mama na wala sio Makala.

Kama atatokea mtu awahoji wamachinga wote lazima utafahamu ni nani amewapa kibali cha kufanya biashara kwenye eneo lisiloruhusiwa na kwa mashariti gani.
 
Ila hujamtendea haki Amos Makala kwa kumtambua kama DC badala ya RC! Yaani umemuweka Papaa Makala, mutu ya watu katika kapu moja na akina Niki wa Pili?
 
viongozi wa chama huko matawini ndio vinara wa kupora maeneo ya wazi, ndio maana walikuwa wanamchukia Bashiru na mwenyekiti wake kwa kudhibiti mali za chama. kama maRC hawatakuwa macho jitihada zao za kumuunga mkono Rais kwenye zoezi hili la usafi zitagonga mwamba. Hapa wanamjaribu Mama na wala sio Makala.

Kama atatokea mtu awahoji wamachinga wote lazima utafahamu ni nani amewapa kibali cha kufanya biashara kwenye eneo lisiloruhusiwa na kwa mashariti gani.
Mkuu hongea sana kwa kutumia upeo mkubwa wa kuangalia jambo hili...
 
Back
Top Bottom