DC Magu atangaza kiama kwa watendaji wa kata, vijiji na wenyeviti

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
DC Magu atangaza kiama kwa watendaji wa kata, vijiji na wenyeviti

Mkuu wa Wilaya ya Magu mkoani Mwanza SALUM KALI amewataka watendaji wa kata, vijiji vitongoji na wenyeviti wote wilayani humo kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia na mimba za utotoni hususani wanafunzi wa shule za msingi kitendo ambacho kinakatisha ndoto za watoto hao.

Amesema kuwa endapo viongozi hao watashindwa kukomesha na kushughulikia vitendo hivyo katika maeneo yao ataanza kuwatengenezea mazingira ya kaondolewa na wananchi.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa mkutano wa wadau wa kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto lililoandaliwa na shirika lisiko la kiserikali la kutetea haki za wanawake na wasichana la Kivulini mkoani Mwanza.

Kali amesema kuwa katika wilayani hiyo kumeshamili vitendo vya ukatili pamoja na mimba kwa watoto wadogo hususani wanafunzi.

Amesema licha ya kuwepo kwa watendaji wa kata na wenyeviti wa vijiji, vitongoji lakini bado wimbi la wanafunzi kupewa mimba linaendelea katika maeneo yao na kakatisha masomo wanafunzi hao bado.

"Mwenyekiti wa kijiji, kitongoji na madiwani na kamati zao za uongozi katika maeneo yao wakaishi na shida za wananchi, wapate taarifa shuleni ni watoto wangapi wapo shule na kama hawapo wafahamu sababu za kutokuwepo kwao.

"Wafahamu kama hawapo wafuatilie kule walikotoka wajue nikitu gani kimesababisha hawapo shuleni, wabaini ni ujauzito, maisha magumu, mtoto katoroshwa ama kapelekwa kufanya kazi za ndani maeneo mengine.

"Tunaweza kukomesha hili kama viongozi wenzangu wataishi na shida za watu watakwenda kwa wananchi na hii tunataka kuona wilaya yetu inakuwa ni miongoni mwa wilaya bora nchini kufaurisha wanafunzi kwenye mitihani ya kimkoa na kitaifa," amesema Kali.

Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za wanawake na wasichana la Kivulini, Yassin Ally, amesema katika wilaya ya magu ndani ya robo ya mwaka huu, asilimia 25 ya kesi zilizo ripotiwa jeshi la Polisi ni mimba za utotoni.

Amesema kuwa pamoja na tatizo hilo, lakini bado kuna baadhi ya walimu "mafataki" waliokabidhiwa dhamana ya kuwalea watoto kujihusisha kimapenzi na wanafunzi.

"Kuna mwalimu wa shule moja ya msingi (jina linahifadhiwa) katika kijiji cha Irungu amebainika kujihusisha kimapenzi na kuwapa ujauzito wanafunzi wake na mchezo hup ameufanya miaka sita bila kuchukuliwa hatua.

"Mwalimu huyu amekuwa akitumia madaraka yake vibaya kwa mjibu wa watoto, wanaeleza inapokaribia mitihani anawadanganya atakalisha pamoja atawapa majibu," amesema Yassin.

Mkuu wa Polisi wilaya ya Magu, Amani Migoha amesema katika kipindi cha mwaka 2019 dawati la jinsia wilayani humo lilipokea makosa mbalimbali 304 yakiwemo ya ubakaji, mimba za utotoni.

Amesema katika kipindi cha robo tatu ya mwaka januari hadi Aprili mwaka guy yameripotiwa makosa 74.

Amani amesema makosa ya ukatili wa kijinsia na ubakaji yanaripotiwa katika kitengo cha dawati la jinsia kuweka mkazo kwa wenyeviti wa vijiji na vitongoji kuripoti makosa hayo kwenye vituo vya Polisi.

MWISHO
 
Back
Top Bottom