DC Longido alimwa Notisi ya siku saba kupelekwa mahakamani

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mkuu wa wilaya ya Longido Frenk Mwaisumbe ameagiza kukamatwa kwa mwekezaji wa Kampuni ya uwindaji ya Green mail,Awardhi Abdallah Ally popote alipo na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kutokana na kukaidi kulipa deni la sh,milioni 339 za vijiji 23 wilayani humo.

Awali mwekezaji huyo kupitia wanasheria wake wiki iliyopita alimwandikia notisi ya siku saba mkuu huyo wa wilaya, akimtaka akanushe kauli yake aliyoitoa kwenye vyombo vya habari na kumsafisha,inayodai kuwa kampuni yake inadaiwa na vijiji 23 na kwamba baada ya muda huo kupita angempandisha mahakamani.

Akiongea na vyombo vya habari jijini hapa mapema leo,Mwaisumbe amedai kuwa mwekezaji huyo ameshindwa kulipa deni hilo baada ya kuingia makubaliano na vijiji hivyo 23, tangu mwaka 2013.

Alisema fedha hizo ni zao la makubaliano ya kusaidia maendeleo katika vijiji hivyo vilivyoko jirani na eneo lake la uwekezaji ikiwemo utunzaji wa mazingira ,ulinzi wa maliasili na ujenzi wa miundo mbinu, ambapo alikubali kulipa kiasi cha sh,milioni 4.5 na kiasi cha shilingi milioni 1 kwa mwaka kwa ajili ya maendeleo ya elimu kwa kila kijiji.

" Tangu ameingia makubaliano na vijiji hivyo mwaka 2013 amelipa mwaka mmoja tu 2014 kwa vijiji vyote na mwaka 2015 alidai anakesi mahakamani hivyo kushindwa kulipa lakini kuanzia mwaka 2016 hakuweza kulipa chochote hadi sasa"Alisema mkuu huyo

Amemtaka Mkurugenzi huyo kujisalimisha popote alipo katika kituo chochote cha Polisi Tanzania bara au Visiwani ili aweze kulipa deni hilo na asipofanya hivyo nimeagiza akamatwe popote alipo.

"Akikamatwa hawezi kutoka bila kulipa fedha za wanakijiji hivyo ajitayarishe sisi hatuna mzaha tupo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi " Alisema

Jitihada za kumpatia mwekezaji huyo hazikuweza kuzaa matunda kutokana na kutopatikana kupitia Simu yake ya Mikononi.

Ends......

IMG_20190226_114814.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo ulimi vipi? , au swaga

View attachment 1032672

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom