DC kuambiwa hana adabu...JE, NI TUSI? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DC kuambiwa hana adabu...JE, NI TUSI?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mukuru, Sep 15, 2009.

 1. Mukuru

  Mukuru Member

  #1
  Sep 15, 2009
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakazi wa Kipawa wamwambia DC Ilala hana adabu


  WAKAZI wa Kipawa jijini Dar es Salaam wamemsikitisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Evance Balama baada ya kumwambia kinagaubaga kuwa hana adabu.

  Wananchi hao, walitoa kauli hiyo juzi ofisini kwa mkuu huyo baada ya wananchi hao, kuandamana hadi ofisi ya bosi huyo ili kupata ufumbuzi wa suala lao la malipo ya fidia ya kubomolewa nyumba.

  Mkuu huyo aliwaeleza wananchi hao, kuwa hajawahi kuambiwa hivyo tangu aanze kazi miaka 19 iliyopita na kwamba anashangaa wazee wa Kipawa wanamtaka awaamkie kwanza kabla ya kuwasikiliza.

  "Hutaki kuamkia?, "Huna adabu," alisikika mzee huyo akimwambia DC.

  Unasema sina adabu mimi?" alihoji DC huyo. "Ndiyo huna adabu," alisisitiza.

  "Mimi sina adabu? nina miaka 19 ya kazi hii tangu nianze sijawahi kutukanwa na mwananchi.

  Ninyi mlinivamia nikawaambia twendeni kule ili wazee wasikae chini, leo hii mnanitukana sina adabu? kama hali ndiyo hii mimi nimeshindwa,"alisema Balama.

  Kauli hiyo, iliyooenekana kumsononesha mkuu huyo wa wilaya na kusababisha agome kuwasikiliza wakazi hao na kuwaeleza kuwa kama wana tatizo lolote waende ngazi ya juu zaidi.

  "Nimemweleza Mkuu wa Mkoa William Lukuvi juu ya hili na nia yangu ya kujitoa naye ameridhia hivyo, mimi sitakuwa tayari kuwasikiliza madai yenu na kama mnataka niko tayari kuwaandikia barua,"alisema Balama.

  Pamoja na kueleza dhamira yake yakutosikiliza madai ya wakazi hao, alifafanua kuwa anataendelea na kazi ya kusaini fomu kwa ajili ya kulipa fidia wakazi hao kama sheria inavyomtaka kazi ambayo aliianza jana.

  Juzi wakazi hao waliandamana kwa sitaili ya aina yake baada ya kuwatanguliza wajumbe watano wa kamati kwenda kufuatilia nakala ya majibu ya ushauri kutoka kwa mwanasheria wa serikali, lakini baada ya kushindwa kupata nakala hiyo ndipo walipowataarifu wananachi wanzao waliokuwa kwenye majengo ya shule ya msingi Kipawa wakiwasubiria.

  Baada ya wananchi hao, kufika kwenye geti lililopo ofisi ya mkuu wa mkoa mlinzi aliyekuwapo ofisini hapo alilazimika kuwazuia, lakini wananchi hao walisukuma geti na kumzidi nguvu mlinzi huyo na kuingia ndani.

  Wakiwa ndani ya geti walisema walipanga kutotoka hapo hadi hapo watakapopata nakala hiyo, lakini baadaye walilazimika kuondoka baada ya Mkuu wa wilaya kurejea katika eneo hilo na kuwaeleza wazi kuwa yeye ameshindwa na kuwataka wachukue barua kwa jili ya kwenda ngazi za juu.

  Mwenyekiti wa wakazi wa Kipawa Magnus Mulisa alimweleza mkuu huyo wa wilaya kuwa udanganyifu uliofanywa na a Afisa Ardhi Mwandamizi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam, umewakwaza wakazi hao.

  Alisema Afisa huyo, aliahidi kuwapatia nakala hiyo juzi, lakini alipofika ofisini kwake alimfukuza akidai anakwenda kufanya nini na kwamba hawezi kufundishwa kazi na Mulisa.

  Alimtaka mkuu huyo kumuondoa afisa huyo katika kazi na kwamba ampangie kazi nyingine kwa madai kuwa hafai na anaidanganya serikali.
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  "Huna adabu" ni tusi ndiyo. Ni kumwambia mtu kwa lugha isiyo na heshima kwamba si mstaarabu, hajalelewa vema, hana utu wala uungwana wowote. Kumbe kumwambia mtu mzima tena mkuu wa wilaya kwamba hana adabu kwa kweli ni kumtukana hata kama inawezekana alikuwa ameonesha dalili hizo katika uhalisia. Kulikuwa na namna nyingi za busara za kumwambia Mkuu kwamba hakujiheshimu. Mkubwa ni mkubwa tu. Kuna namna za kumweleza na akatambua kwamba amekosea, au hajawa mstaarabu. Si lazima kumbomoa kwa lugha nzito isiyo na "nepi"
   
 3. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Kila neno ni tusi na kila neno si tusi linategemea limetumika wapi na mazingira yepi.
   
 4. S

  Simoni Member

  #4
  Sep 15, 2009
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 67
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Huyo Magnus Malisa ambaye anajiita Mwenyekiti wa walalamikaji ni tatizo na anayo malengo ya kisisasa. Ni mwanachama hai wa CUF. Kajipachika kwenye issue hiyo ilhali siyo mkazi wa Kipawa wala siyo muathirika. Ni mpuuzi mkubwa huyo.
   
Loading...