DC Kinondoni azishitaki kampuni za simu!

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Imeandikwa tarehe 30 Novemba 2012 na Gloria Tesha | HabariLeo

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni katika Mkoa wa Dar es Salaam, Jordan Rugimbana ameiomba Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kubana kampuni za simu zinazowalazimisha wateja kukatwa fedha za huduma wasizozihitaji.

Aidha amezitaka kampuni hizo kuacha kutumia vibaya teknolojia ya mawasiliano katika ushindani wa kibiashara uliopo, kwa kupotosha umma kuhusu huduma mpya zinazotolewa bure wakati si kweli kumbe lengo ni kupata wateja wapya.

Rugimbana alisema hayo jana, Dar es Salaam katika hotuba yake ya ufunguzi wa semina ya wadau wa mawasiliano wa Manispaa ya Kinondoni iliyoendeshwa na TCRA.

Hotuba hiyo ilisomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala wa Wilaya, Bernard Marcelline. Mkuu huyo wa Wilaya alisema malalamiko kwa watumiaji wa mitandao ya simu ni mengi na yanakera kwa kuwa hata mtu anapohitaji huduma ya dharura, analazimishwa kusikiliza matangazo ya kampuni yasiyomhusu jambo ambalo ni kinyume cha haki ya mlaji.

"Kama tujuavyo kumekuwa na maendeleo makubwa katika sekta ya mawasiliano lakini changamoto pia ni nyingi, mojawapo ni hizi mbizu za kampuni za simu kutangaza huduma zao kwa wateja kwa njia ya kupotosha."

"Kwa mfano, mteja anatangaziwa atapata muda wa maongezi mara mbili akiongeza salio, au muda wa kutuma ujumbe iwapo atatuma fedha kwa simu, lakini wengi wanalalamika hawaoni kile walichoahidiwa kikijionesha kwenye gharama za kupiga simu," alisema Rugimbana.

Pia alisema kumekuwa na huduma mbovu katika vitengo vya huduma kwa wateja vya baadhi ya kampuni za simu nchini ikiwemo lugha mbaya, mpigaji kushindwa kuunganishwa na anayempigia huku simu majibu yakiwa hapatikani wakati yupo hewani.

"Hili la kulazimishwa kusikiliza matangazo ya simu nalo linakera, wateja hawahitaji matangazo hayo maana wengi mahitaji yao ya simu ni ya dharura na haraka, mitandao mingine mtu unakatwa fedha za nyimbo au ujumbe wa sauti wakati hajajiunga, TCRA isaidie mambo haya yanakera watumiaji," alisema Rugimbana.

Kuhusu minara ya simu karibu na makazi ya watu, Rugimbana aliiomba TCRA japo ilishatoa taarifa ya kutokuwepo kwa madhara yoyote, kufuatilia kama wanaofunga minara hiyo wanazingatia matakwa ya Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na ushirikishwaji wa viongozi wa Serikali za Mitaa.

Hata hivyo, aliipongeza TCRA kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kudhibiti mfumuko wa matumizi mabaya ya simu za mkononi baada ya kuzisajili lakini aliwataka kuongeza udhibiti kwa kuwa bado laini zinauzwa holela na kutumika bila kusajiliwa.

Awali, Naibu Mkurugenzi, Masuala ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano wa TCRA, Richard Kayombo alisema lengo la semina hiyo ni kuwafikia wananchi kupitia wawakilishi wao (Madiwani) na watendaji wa Serikali za Mitaa kujua haki za huduma hiyo na mabadiliko yaliopo.
 
Sawia! Haya makampuni ya simu hasa Vadacom ni kama matapeli vile. Kuna hii kitu kinaitwa Bima ya Faraja ambayo mtu akituma pesa mara kumi kwa mpesa ndani ya mwezi mmoja anaahidiwa kupewa laki mbili. Mwezi huu nimekuwa nikitumia huduma za mpesa mara 12 hadi hivi sasa. Wakati nimefikisha mara 8, nililetwa ujumbe ulionijulisha kuwa nijitahidi kutumia mpesa mara mbili zaidi ili niweza kunufaika na Bima ya faraja. Ujumbe huo uliniingiza mkenge (najuta ningehamia airtelmoney), kwani nilitumia huduma hiyo kwa kuwatumia pesa watu wengine wanne kwa siku tofauti tofauti. Baada ya kufikisha zaidi ya mara 10, niliwapigia simu ambayo ilikuwa inaita bila kupokelewa kwa muda mrefu hadi inakatika yenyewe! Kama hiyo aitoshi, kila nikitaka kupata huduma za Bima ya Faraja kwa kutumia *154*44# kile kifungu cha 5, mtandao unaniambia "request uncompleted". Kwa hiyo nimebaki solemba, sina hamu!
 
bila kusahau airtel wanavokata wateja wao sh 54 kutaka kuongea na huduma kwa wateja na.ukipiga mara ya kwanza wanakukatai ili upige tena afu pia ukiweka hela.inaisha hujui imeelekea wapi
 
Sawia! Haya makampuni ya simu hasa Vadacom ni kama matapeli vile. Kuna hii kitu kinaitwa Bima ya Faraja ambayo mtu akituma pesa mara kumi kwa mpesa ndani ya mwezi mmoja anaahidiwa kupewa laki mbili. Mwezi huu nimekuwa nikitumia huduma za mpesa mara 12 hadi hivi sasa. Wakati nimefikisha mara 8, nililetwa ujumbe ulionijulisha kuwa nijitahidi kutumia mpesa mara mbili zaidi ili niweza kunufaika na Bima ya faraja. Ujumbe huo uliniingiza mkenge (najuta ningehamia airtelmoney), kwani nilitumia huduma hiyo kwa kuwatumia pesa watu wengine wanne kwa siku tofauti tofauti. Baada ya kufikisha zaidi ya mara 10, niliwapigia simu ambayo ilikuwa inaita bila kupokelewa kwa muda mrefu hadi inakatika yenyewe! Kama hiyo aitoshi, kila nikitaka kupata huduma za Bima ya Faraja kwa kutumia *154*44# kile kifungu cha 5, mtandao unaniambia "request uncompleted". Kwa hiyo nimebaki solemba, sina hamu!

Mkuu, bima ya faraja ni bima ya maisha. Ni malipo ambayo familia yako au mrithi wako atapewa iwapo itatokea wewe ukaaga dunia katika kipindi hicho ambapo uko covered. Ndio maana kuna taratibu za kumwandikisha beneficiary wako baada ya ku-qualify. Hata mimi mwanzoni nilipata shida sana kuwaelewa hawa jamaa.
 
TCRA wako kwenye payroll ya hayo makampuni ya simu.
Hawana meno, tena wamebemendwa.
Hivi Tanzania kwani tuna mamlaka ya mawasiliano,mi naona,huyo professor naona anajilia hela buure hakuna anachokifanya,mimi siku hizi naamini kazi kama hizi zinahitaji vijana wa dotcom na sio old skool,ukitaka kuamini angalia mashirika au taasisi zinazoendeshwa na ma ceo dotcom na hao old skool utaona tofauti kubwa,angalia NHC ilivyokuwa hapo nyuma na hivi sasa
 
Kwenye cheka time ndo utalia.Nusu saa inavyokimbia utatadhani roketi.Dakika 1 na sekunde 3 wanakata dakika 2.Vodacom?!
 
Mkuu, bima ya
faraja ni bima ya maisha. Ni malipo ambayo familia yako au mrithi wako
atapewa iwapo itatokea wewe ukaaga dunia katika kipindi hicho ambapo uko
covered. Ndio maana kuna taratibu za kumwandikisha beneficiary wako
baada ya ku-qualify. Hata mimi mwanzoni nilipata shida sana kuwaelewa
hawa jamaa.

Na ukishaipata hiyo bima inadumu kwa muda gani?
 
Kwa mfano kama umetuma hela mara kumi au zaidi ndani ya mwezi huu wa November, basi unakuwa ume-qualify kwa bima ya bure kwa mwezi wa Disemba. Hivyo basi ikitokea bahati mbaya ukafariki ndani ya mwezi huo wa Disemba, basi warithi wako watapewa hiyo hela.
 
Back
Top Bottom