Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,582
- 6,627
Imeandikwa tarehe 30 Novemba 2012 na Gloria Tesha | HabariLeo
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni katika Mkoa wa Dar es Salaam, Jordan Rugimbana ameiomba Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kubana kampuni za simu zinazowalazimisha wateja kukatwa fedha za huduma wasizozihitaji.
Aidha amezitaka kampuni hizo kuacha kutumia vibaya teknolojia ya mawasiliano katika ushindani wa kibiashara uliopo, kwa kupotosha umma kuhusu huduma mpya zinazotolewa bure wakati si kweli kumbe lengo ni kupata wateja wapya.
Rugimbana alisema hayo jana, Dar es Salaam katika hotuba yake ya ufunguzi wa semina ya wadau wa mawasiliano wa Manispaa ya Kinondoni iliyoendeshwa na TCRA.
Hotuba hiyo ilisomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala wa Wilaya, Bernard Marcelline. Mkuu huyo wa Wilaya alisema malalamiko kwa watumiaji wa mitandao ya simu ni mengi na yanakera kwa kuwa hata mtu anapohitaji huduma ya dharura, analazimishwa kusikiliza matangazo ya kampuni yasiyomhusu jambo ambalo ni kinyume cha haki ya mlaji.
"Kama tujuavyo kumekuwa na maendeleo makubwa katika sekta ya mawasiliano lakini changamoto pia ni nyingi, mojawapo ni hizi mbizu za kampuni za simu kutangaza huduma zao kwa wateja kwa njia ya kupotosha."
"Kwa mfano, mteja anatangaziwa atapata muda wa maongezi mara mbili akiongeza salio, au muda wa kutuma ujumbe iwapo atatuma fedha kwa simu, lakini wengi wanalalamika hawaoni kile walichoahidiwa kikijionesha kwenye gharama za kupiga simu," alisema Rugimbana.
Pia alisema kumekuwa na huduma mbovu katika vitengo vya huduma kwa wateja vya baadhi ya kampuni za simu nchini ikiwemo lugha mbaya, mpigaji kushindwa kuunganishwa na anayempigia huku simu majibu yakiwa hapatikani wakati yupo hewani.
"Hili la kulazimishwa kusikiliza matangazo ya simu nalo linakera, wateja hawahitaji matangazo hayo maana wengi mahitaji yao ya simu ni ya dharura na haraka, mitandao mingine mtu unakatwa fedha za nyimbo au ujumbe wa sauti wakati hajajiunga, TCRA isaidie mambo haya yanakera watumiaji," alisema Rugimbana.
Kuhusu minara ya simu karibu na makazi ya watu, Rugimbana aliiomba TCRA japo ilishatoa taarifa ya kutokuwepo kwa madhara yoyote, kufuatilia kama wanaofunga minara hiyo wanazingatia matakwa ya Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na ushirikishwaji wa viongozi wa Serikali za Mitaa.
Hata hivyo, aliipongeza TCRA kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kudhibiti mfumuko wa matumizi mabaya ya simu za mkononi baada ya kuzisajili lakini aliwataka kuongeza udhibiti kwa kuwa bado laini zinauzwa holela na kutumika bila kusajiliwa.
Awali, Naibu Mkurugenzi, Masuala ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano wa TCRA, Richard Kayombo alisema lengo la semina hiyo ni kuwafikia wananchi kupitia wawakilishi wao (Madiwani) na watendaji wa Serikali za Mitaa kujua haki za huduma hiyo na mabadiliko yaliopo.