Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 875
- 960
DC KINONDONI ASHIRIKI IBADA YA IJUMAA MSIKITI WA MTAMBANI NA KUONGEA NA WAISLAM
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi leo ameshiriki ibada ya Ijumaa katika msikiti wa Mtambani, Kinondoni ambako alipata nafasi ya kuwasalimia waumini wa kiislam walioswali swala ya Ijumaa msikitini hapo.
Hapi alifika msikitini hapo majira ya saa 6 unusu mchana ambako baada ya swala Imamu alimkaribisha kuongea na waumini.
"Leo ni mara ya kwanza kwa msikiti wetu huu kutembelewa na kuswali swala ya Ijumaa pamoja na kiongozi wa serikali kama Mkuu wa Wilaya. Tumefarijika sana. Historia imeandikwa leo..." alisema Imamu.
Katika salam zake, Mh Hapi alielezea shukrani zake kwa Mwenyeezi Mungu na Mh. Rais Dr John Magufuli kwa kumteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni. Aidha, Hapi aliwasihi waumini kuwa na imani na serikali yao kwani awamu ya tano imejipanga kusimamia haki na uadilifu ili kuwaletea maendeleo watanzania. Mkuu wa Wilaya aliwatoa shaka kuwa serikali ya Rais Dr. John Magufuli iko pamoja na wale wote wanaopenda haki na uadilifu.
Katika hatua nyingine, Hapi aliwaomba kumpatia ushirikiano wa kutosha katika kuongoza wilaya ya Kinondoni, kupambana na ufisadi, ukwepaji kodi na uchafu.
"Tumeanza kusafisha mji wetu, kuondoa madanguro, biashara haramu ya kuuza mwili na kudhibiti baa zinazopiga kelele kinyume cha sheria. Tunaomba mtuunge mkono katika kazi hii muhimu..." alisema Mh. Hapi.
Katibu wa msikiti huo alimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa salamu zake na kumuahidi ushirikiano mkubwa kwake. Aidha, katibu alitoa ombi kwa Mh. Mkuu wa Wilaya kufikisha kilio chao kwa Mh. Rais John Magufuli kufuta hati ya kiwanja cha waislam kilichopo Chang'ombe jijini Dar es salaam kilichoporwa na mfanyabiashara mmoja jijini.
"Tumedhulumiwa kiwanja cha waislam pale Chang'ombe na mfanyabiashara mmoja mkubwa. Tuna imani na Dr. Magufuli kuwa ni mtu imara asiyeyumbishwa na wafanyabiashara. Tunaomba umfikishie kilio chetu kuwa afuhte hati ya kiwanja hicho na kukirejesha kwa waislam ili tujenge chuo watoto wetu wapate elimu."
Alisema katibu.
Mkuu wa Wilaya alimaliza salamu zake kwa kuwaomba waumini kuliombea taifa na kumuombea Mh. Rais Dr. John Magufuli na wasaidizi wake wote, kwani kazi anayoifanya ni kubwa na ina maslahi kwa watanzania wanyonge na taifa kwa ujumla.