DC Kihongosi wa Arusha amekosea, Huu ni ulevi wa madaraka na unyanyasaji wa raia walioipa dhamana Serikali

3456321.jpg
 
Dah .... Inatia hasira sana....tunalipa kodi...serikali inanunua madawati....kila moja Laki...halafu wanatokea wapuuzi wachache wanageuza viti mageti....bora wamechukua bakora....na kulipa viti vyote.....ningekuwepo wangechezea vitasa hadi jinsia zao zibadilike dadadadeki
 
Kuna wababe ukiwafanyia hivyo jipange kutembea na KY wakati wote
 
RC Chalamila na DC Kihongosi wote ni wahehe panick kubwa kuliko akili,maana RC Chalamila nae alichapa watoto viboko huko Chunya
 
Tunawaza v
DC KIHONGOSI wa Arusha amekosea Huku ni ulevi wa madaraka na unyanyasaji wa RAIA walioipa dhamana Serikali

Adhabu ya Viboko (corporal punishment)
ni moja ya Adhabu zilizowekwa na Sheria za Jinai za Tanzania hususani KANUNI YA ADHABU (The Penal Code) Sura ya 16, chini ya Kifungu cha 25 cha Sheria hiyo.

Adhabu ya viboko imewekewe utaratibu namna ya utekelezwaji wake kwa Mtuhumiwa; chini ya Sheria yake Mahsusi inayoitwa The Corporal Punishment Act, baada ya kukutwa na Hatia na Mahakama yenye mamlaka kwa mujibu wa Ibara ya 13 (6) (a & b) ikisomwa sambamba na Ibara ya 107A ya Katiba ya JMT,1977.

Adhabu zilioorodheshwa katika Sheria hiyo ni pamoja na Adhabu ya Kifo kwa Kunyongwa, Kifungo jela, Kulipa faini, n.k.

Kitendo alichofanya DC wa Arusha kuwachapa Viboko watuhumiwa wa wizi; ni Kuwahukumu na Kutekeleza Adhabu ya Viboko bila Kushtakiwa na Kusikiliza katika Mahakama yenye Mamlaka na bila kwanza kutiwa hatiani.

Je, DC akibaini au akimtuhumu Muuaji katika eneo lake la utawala; atamnyonga kwa mkono wake?

Amejichukulia Sheria mkononi. Ni kosa!

DC atapata ujasiri wa kukemea tabia ya Wananchi kujichukulia Sheria mkononi dhidi ya washukiwa na watuhumiwa?

DC amekuwa ni Mlalamikaji mwenyewe, kisha akawa Mshtaki mwenyewe, halafu akajivika Mamlaka ya Mahakama kuwahukumu Adhabu ya Viboko; mwishoni akawa ni Afisa wa Polisi yeye mwenyewe akatekeleza adhabu aliyowahukumu watu hao.

Amekiuka Misingi ya Utoaji Haki.

Amekiuka Misingi ya Mgawanyo wa Madaraka miongoni mwa Mihimili ya Dola. DC ameingilia kazi ya Mahakama, kutoa haki na kuhukumu baada ya kusikiliza kesi kwa ukamilifu wake (Due process of the law).

DC wa Arusha amekosea.

Ahsante

BARAKA TUMAINI KASKASI

Gwata Kisarawe
iboko vitatu walivyochapwa wale watu tusisahau tukimaliza tuanze kuwaza madawati 108 yatapatikana vipi
 
Kuna wababe ukiwafanyia hivyo jipange kutembea na KY wakati wote
Ni kweli kabisa.

Afrika kuna mashujaa wachache sana kutokana na hulka ya kupuuza. Enzi za mkoloni Waafrika ndio waliokua wanawabeba wakoloni Mabegani na wanawavusha kwenye mito mikubwa na mapori manene na milima mirefu.

Nyuma yao walisimama waafrika waliokua wanawadhibiti waafrika wenzao wasije wakawadondosha Mabwana waliokua wanawabeba mabegani kwenda kununua ndugu zao kama watumwa na kuwauza kama bidhaa zinazopatikana kwa bei nafuu sana.

Fikiri tu ilikuaje kwa manynyaso yote yaliyofanywa na wakoloni lakini hakuna aliyekua anakerwa na Watesi wao waliojiita mabwana wakubwa na hivyo kuamua kuchukua hatua ya kishujaa ya kuwatupilia mbali kwenye majabali na mtoni wakaliwa na mamba ili iwe ni mwiko kuwatumia waafrika kama magari ya kubeba mzigo na abiria huku wakiwauza kama mifugo!!

Nafikiri mashujaa kuna wakati wanajitokeza kutokana na mazingira ya ukiukwaji wa sheria na haki za mwanadamu.

Hata Tembo wakivamia kijiji mkuu wa wilaya hachukui Bunduki na kuwaua bila kufuata kanuni za askari wenyewe wa mali asili.

Ukiibuka tu na kuanza kuwashambulia tembo halafu wakaleta madhara makubwa kwako au kwa jamii nadhani kosa litabaki kwako mwenyewe.

Kwa upande wa wale wanafunzi ,Mfano angetokea mmoja wapo wa wale wanafuanzi akawa na hulka ya ushujaa na akawa ni miongoni mwa wale wa Ma scout wanaojfunza Kareti na mbinu za kujihami halafu akafanya jambo moja kwa uhakika,kwa wepesi na kwa haraka na kumpiga finger kwenye chembe ya moyo yule kijana mkubwa aliyekua anafanya vitendo vya kuchapa chapa watu kihuni na kusubiri matokeo yoyote ingekuaje kama sio kama ishu kama ile ya Mwamwindi.!!?

Hakuna anayeunga mkono uharibifu wa Mali ya umma.

Ni kweli kabisa Wale wanafunzi walipaswa kuadhibiwa ama kwa kufukuzwa shule au kuchapwa viboko na kulipa madawati mapya mawili kwa kila moja kama adhabu na adhabu nyingine Kali kwa kuzingatia misingi na kanuni za shule.

Lakini katika adhabu zote hizo hakuna inayotolewa na DC zaidi ya ile ya kutoa amri ya kuwaweka ndani masaa 48.

Sasa tunaiomba serikali ituambie DC ametumia Kanuni na sheria ipi kupiga watu tena watoto kwa kitu kizito kwenye makalio yao mana hana sheria inayomwambia akae ofisini au atembee na kifaa cha kupigia watu.

DC hana mamlaka ya kuchukua sheria mkononi kuingilia idara zilizopo kwenye Wilaya kwa kupoka madaraka ya watendaji walioko chini ya idara hizo. Wilaya ina Afisa Elimu ,kuna waratibu wa Elimu ,kuna mwalimu Mkuu ,kuna mwalimu wa nidhamu na mlezi wa wanafunzi ,Kuna Mwalimu wa zamu n.k. Wote hao walikuwepo na wanajua utaratibu gani ungefuata baada ya Kutokea kwa tukio hilo.
Hivi mkuu wa Wilaya anaweza kufanya kazi za watendaji wote kwenye wilaya kama anavyotaka yeye.?

Kama anauwezo wa kwenda shuleni na kuchukua madaraka ya kuadhibu wanafunzi tutakua na imani gani naye pale atakapomuita Mhasibu wa Halmashauri na kumwambia Lete pesa kwa kiasia Fulani kimabavu bila hata kufuata utaratibu wa kifedha?

Hivi huyo DC haoni kuwa tumeanza kuwa na mashaka na utendaji wake unaoingilia kazi za kitaalamu ziwe za fedha au Mali za umma?

Tumekwama kwa muda mrefu na kujikuta tunawabebesha wanyonge mzigo mzito sana kutokana na kuwa na viongozi wasiofuata sheria. Nchi yetu tangu Uhuru imekua na sheria nzuri lakini watendaji wabinafsi wamezitumia kufanya walivyotaka wao na wakati mwingi tukawa tunalitia taifa ketu hasara.

Je , nani amethibitisha kwa hakika kuwa kuna madawati 104 yaliyokuwa darasana kisha yakatolewa kwenda kuuzwa kama vyuma chakavu?
Je, ni kweli kuwa hayo madawati yalikua mazima kabisa au yalikua yametupwa nje baada ya kuwa yamekatika au kuchakaa ?
Kama yalichakaa na kutupwatupwa hovyo ,sheria inasemaje kama Mali imetupwa na mmiliki wake hana matumizi nayo halafu mwingine akaiokota sio kwa nia ya kuiiba Bali kwake inamfaa?

Hivi DC hakujifunza kwa Mheshimiwa Rais aliposikia Polisi wameshiriki kuuza vyuma chakavu kule Mlandizi lakini hakuchukua Bunduki,marungu na mapingu na kwenda kuwapiga bali alitoa maelekezo kwa mkuu wa Idara hiyo ambaye ni IGP achukue hatua kwa mujibu wa sheria za nchi na za idara hiyo ? Huo ndio utawala wa sheria.

Na siamini kabisa kuwa Mheshimiwa Rais atakubali kuacha nchi hii iendelee kuchafuliwa na wahuni wachache wanotafuta sifa za ajabu ajabu na kuionyesha dunia kuwa Tanzania ni nchi inayotawaliwa kipori pori ,mwenye nguvu mpishe. Nchi yenye watu na wanyamawatu . Yaani kuna wanaojiona wao ndio wenye kuamua jambo lishughulikiweje na sio sheria za nchi na Utaratibu uliowekwa.!!

Mkuu wa Wilaya na mkuu wa Mkoa ni wawakilishi wa Rais hivyo wanapaswa kusimamia sheria za nchi na kuwa mfano wa Kusimamia na kuonyesha Utawala Bora.

Tumekua tukichafuliwa sana kuwa Taifa letu lina ukiukwaji mkubwa wa Haki za binadamu. Sasa Itakua ni ajabu sana kama Tutaendelea kuwatukuza na kuwakweza watawala wa Aina ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha ambao wamevunja haki za msingi za binadamu tena watoto wadogo !!

Kati ya adhabu za Kikoloni na za kinyama ni pamoja na adhabu ya Kunyonga na Kuchapa watu viboko. Walimu wana mwongozo mwalimu wa kuwadhibu wanafunzi wao kama walezi na sio kama sifa au maonyesho ya kuonyesha kwenye mitandoa.

Kwanza ni makosa makubwa kufanya tendo hilo ambalo ni kinyume cha Sheria za utawala la kuwapiga watoto walioko chini ya walimu ambao ni walezi wao na kuweka kwenye mitandao.

Mh.Rais alionya sana masuala ya kutumia vibaya madaraka kwa kupitia mitandao. Huyu Kijana DC aliamua kutumia nafasi yake vibaya kwa kuweka watu wa kamera wakati akiwa anawanyanyasa watoto wadogo kwa kuwapiga na kitu kizito kwenye makalio yao kinyume cha sheria na mwongozo unaomuongoza kama mkuu wa Wilaya.

Hivi Mkuu wa Wilaya alishindwa kumwelekeza Afisa Elimu achukue hatua za kinidhamu kwa wanafunzi hao na Pia Jeshi la Polisi lichungue ili kubaini kosa la kijinai lililofanywa?

Wakuu wa Wilaya wakiachwa kuendelea kufanya mashindano ya kupiga watu na kuchukua sheria mikononi bila kufuata sheria ipo Siku mkuu wa wilaya atamnyanganya mtu Bunduki na kuamua kumpiga mtu kama anavyoona inafaa.

Yani Mhalifu ameshakamatwa halafu Mkuu wa Wilaya anafunga safari kwenda kumpiga ? Ajabu kabisa !!
Mimi nilifikiri labda aliwakamata wakiwa wanauza ,akaamua kutumia nguvu kuwakamata kumbe walikua wameshakamatwa na wapo shuleni na wengine Polisi !!
Sasa na wale walionunua nao atawafanyaje? Au atakwenda Polisi kuwapiga marungu na kuwavunja miguu.!!?
Nchi hii ina mambo mengi yanayotakiwa kufanywa kwa kutumia maarifa zaidi mana dunia ya sasa inaongozwa na maarifa sio kiki na maigizo.
 
pole mnunua viti, ila ndo hivo tena! Unapaswa kulipa vile viti! inaumiza saaaana, tumehangaika saana! watoto wetu wanakaa chini ,tumepata viti wewe unanunua na kugeuza vyuma chakavuu?? una bahati upo mbali!
 
DC KIHONGOSI wa Arusha amekosea Huku ni ulevi wa madaraka na unyanyasaji wa RAIA walioipa dhamana Serikali

Adhabu ya Viboko (corporal punishment)
ni moja ya Adhabu zilizowekwa na Sheria za Jinai za Tanzania hususani KANUNI YA ADHABU (The Penal Code) Sura ya 16, chini ya Kifungu cha 25 cha Sheria hiyo.

Adhabu ya viboko imewekewe utaratibu namna ya utekelezwaji wake kwa Mtuhumiwa; chini ya Sheria yake Mahsusi inayoitwa The Corporal Punishment Act, baada ya kukutwa na Hatia na Mahakama yenye mamlaka kwa mujibu wa Ibara ya 13 (6) (a & b) ikisomwa sambamba na Ibara ya 107A ya Katiba ya JMT,1977.

Adhabu zilioorodheshwa katika Sheria hiyo ni pamoja na Adhabu ya Kifo kwa Kunyongwa, Kifungo jela, Kulipa faini, n.k.

Kitendo alichofanya DC wa Arusha kuwachapa Viboko watuhumiwa wa wizi; ni Kuwahukumu na Kutekeleza Adhabu ya Viboko bila Kushtakiwa na Kusikiliza katika Mahakama yenye Mamlaka na bila kwanza kutiwa hatiani.

Je, DC akibaini au akimtuhumu Muuaji katika eneo lake la utawala; atamnyonga kwa mkono wake?

Amejichukulia Sheria mkononi. Ni kosa!

DC atapata ujasiri wa kukemea tabia ya Wananchi kujichukulia Sheria mkononi dhidi ya washukiwa na watuhumiwa?

DC amekuwa ni Mlalamikaji mwenyewe, kisha akawa Mshtaki mwenyewe, halafu akajivika Mamlaka ya Mahakama kuwahukumu Adhabu ya Viboko; mwishoni akawa ni Afisa wa Polisi yeye mwenyewe akatekeleza adhabu aliyowahukumu watu hao.

Amekiuka Misingi ya Utoaji Haki.

Amekiuka Misingi ya Mgawanyo wa Madaraka miongoni mwa Mihimili ya Dola. DC ameingilia kazi ya Mahakama, kutoa haki na kuhukumu baada ya kusikiliza kesi kwa ukamilifu wake (Due process of the law).

DC wa Arusha amekosea.

Ahsante

BARAKA TUMAINI KASKASI

Gwata Kisarawe
Utaratibu wa sasa ndio huo...
Tuvumiliane tu maana hakuna namna tena ni kiboko tu
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom